817 Matamanio ya Pekee ya Mungu

1 Kile utakachoona siku hii ni utukufu wa Yehova, ukombozi wa Yesu na matendo Yangu yote ya siku hii. Umesikia pia maneno ya Roho Yangu, hekima Yangu teule, na ukaja kujua kuhusu maajabu Yangu, na umeweza kujifunza kuhusu tabia Yangu. Nimeweza pia kukuambia kuhusu mpango Wangu wa usimamizi. Kile ambacho umeona si tu Mungu mwenye upendo na huruma, lakini yule aliyejawa na haki. Umeiona kazi Yangu ya maajabu na kujua kwamba Nimejawa na hasira na adhama. Aidha, umejua kwamba Niliwahi kuzishusha hasira Zangu katika nyumba ya Israeli, na kwamba leo hii, umeshushiwa wewe. Umeelewa zaidi kuhusu mafumbo Yangu kule mbinguni kuliko vile alivyoelewa Isaya pamoja na Yohana; unajua zaidi kuhusu uzuri Wangu na kustahiwa Kwangu kuliko watakatifu wote wa vizazi vilivyotangulia.

2 Kile ulichopokea si ukweli Wangu tu, njia Yangu, maisha Yangu, lakini maono na ufunuo ambavyo ni vikubwa zaidi kuliko vile vya Yohana. Umeelewa mafumbo mengine mengi zaidi na pia umeona sura Yangu kamili; umekubali mengi kuhusu hukumu Yangu na tabia Yangu ya haki. Kwa hivyo, ingawaje ulizaliwa kwenye siku za mwisho, uelewa wako ni ule wa siku za awali na za kale; umeweza pia kupitia ni nini kilichomo kwenye siku hii, na kile kilichotimizwa na mkono Wangu. Kile Ninachokuomba kinawezekana, kwani kile Nilichokupa ni kingi mno na ni mengi ambayo umeona Kwangu mimi. Kwa hivyo, Ninakuomba kunishuhudia Mimi kama vile watakatifu wa awali walivyofanya na hili ndilo tamanio tu la moyo Wangu.

Umetoholewa kutoka katika “Unajua Nini Kuhusu Imani?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 816 Kutoa Ushahidi kwa Mungu Ni Wajibu wa Mwanadamu

Inayofuata: 818 Uko Tayari Kuwa Mtu Anayemshuhudia Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp