771 Mungu Awalinda Wale Wampendao

1 Majaribu mengi yatakupata siku za usoni—lakini ikiwa leo unampenda Mungu kwa moyo wa dhati, na ikiwa haijalishi ukubwa wa majaribu yaliyo mbele, bila kujali unachokipitia, unaweza kusimama imara katika ushuhuda wako, na kuweza kumridhisha Mungu, basi moyo wako utafarijiwa, na utakuwa jasiri hata majaribu utakayokabiliana nayo siku za usoni yawe makubwa kiasi gani. Hamwezi kuona ni nini kitatendeka siku za usoni; mnaweza tu kuridhisha Mungu katika hali ya leo. Hamwezi kufanya kazi yoyote kubwa, na unafaa kulenga kumridhisha Mungu kwa kuyapitia maneno yake katika maisha halisi, na kuwa na ushuhuda thabiti na mzito ambao unamtia aibu Shetani.

2 Japo mwili wako hautaridhishwa na utateseka, utakuwa umemridhisha Mungu na kumletea aibu Shetani. Ikiwa daima unatenda hivi, Mungu atakufungulia njia mbele yako. Na siku moja, jaribio kubwa likija, wengine wataanguka chini, ila utaweza kuendelea kusimama imara: kwa sababu ya gharama uliyolipa, Mungu atakulinda ili usimame imara na usianguke. Kwa kawaida, ikiwa unaweza kuweka ukweli katika vitendo na kumridhisha Mungu kwa moyo ambao unampenda kweli, kwa hakika Mungu atakulinda wakati wa majaribu ya siku zijazo. Japokuwa wewe ni mpumbavu na mwenye kimo cha chini na usiye mwerevu, Mungu hatakubagua. Inategemea iwapo motisha zako ni za haki.

3 Unaweza kumridhisha Mungu leo, iwapo uko makini na masuala madogo, unamridhisha Mungu kwa mambo yote, una moyo unaompenda Mungu kwa dhati, unampa Mungu moyo wa dhati, na japokuwa kuna baadhi ya mambo ambayo huwezi kuelewa, unaweza kwenda mbele za Mungu kurekebisha motisha zako, na kuyafuata mapenzi ya Mungu, na kufanya kila lipaswalo kumridhisha Mungu. Pengine ndugu na dada zako wataachana nawe, lakini moyo wako utakuwa unamridhisha Mungu, na hutatamani raha za mwili. Ikiwa daima unatenda kwa namna hii, utalindwa majaribu yakikusibu.

Umetoholewa kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 770 Mungu Atumai Kwamba Mwanadamu Ampende Mungu kwa Moyo, Akili na Nguvu Zake Zote

Inayofuata: 772 Kadri Unavyozidi kumridhisha Mungu, Ndivyo Unavyozidi Kubarikiwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp