966 Mungu ni Mwenye Haki kwa Kila Mtu

1 Kuhusu jinsi watu humtafuta na jinsi wanavyomweleka Mungu, mitazamo ya watu ni ya umuhimu wa kimsingi. Usimwache Mungu kana kwamba yeye ni fungu la hewa kavu tu linaloelea karibu na nyuma ya kichwa chako. Usikose kumjali Mungu ni kana kwamba Yeye ni hewa tupu nyuma ya kichwa chako. Siku zote fikiria kuhusu Mungu wa imani yako kama Mungu hai, Mungu halisi. Yeye hayupo kule juu kwenye mbingu ya tatu bila chochote cha kufanya. Badala yake, siku zote bila kusita Anaangalia kwenye mioyo ya kila mmoja, Akiangalia ni nini unachofanya, akichunguza kila neno dogo na kila tukio dogo, akiangalia mwenendo wako na mwelekeo wako kwa Mungu.

2 Kama uko radhi kujitolea kwa Mungu au la, tabia yako yote na fikira zako na mawazo yako ya ndani zaidi ziko mbele ya Mungu, na yanaangaliwa na Yeye. Ni kulingana na tabia yako, kulingana na vitendo vyako, na kulingana na mwelekeo wako kwa Mungu, ambapo maoni Yake kwako, na mwenendo Wake kwako, vinaendelea vikibadilika. Mungu ni mwenye haki katika kutendea kila mtu. Anakabiliana na kazi ya ushindi wa wanadamu na wokovu kwa bidii. Huo ndio usimamizi Wake.

3 Anashughulikia kila mmoja kwa umakinifu, na wala si kama kiumbe cha kufugwa cha kucheza nacho. Upendo wa Mungu kwa binadamu si ule wa kudekeza au kupotosha; rehema na uvumilivu Wake kwa wanadamu si dokezi au ya kutotilia maanani. Upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wa kutunza, kusikitikia, na kuheshimu maisha; rehema na uvumilivu Wake vyote vinaonyesha matarajio Yake kwa binadamu; rehema na uvumilivu Wake ndivyo ambavyo binadamu anahitaji ili kuishi.

4 Mungu yuko hai, na kwa hakika Mungu yupo; mwelekeo Wake kwa wanadamu unafuata kanuni, si yenye kutangazwa kama imani ya dini, na unaweza kubadilika. Mapenzi Yake kwa binadamu yanabadilika kwa utaratibu na kurekebishwa kwa muda, hali na mwelekeo wa kila mtu. Kwa hiyo, unafaa kujua rohoni mwako na uwazi wote kwamba kiini halisi cha Mungu hakibadiliki, na kwamba tabia Yake itajitokeza katika nyakati tofauti, na muktadha tofauti.

Umetoholewa kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 965 Kweli Unaijua Tabia ya Mungu ya Haki?

Inayofuata: 967 Kiini cha Mungu ni kitakatifu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp