Swali la 7: Miili miwili ya Mungu ilishuhudia kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima. Tunapaswaje kuelewa Kristo kuwa ukweli, njia na uzima?

Jibu:

Kama waumini wanaweza kutambua kweli kwamba Kristo ni ukweli, njia, na uzima, hili ni lenye thamani kweli, na linaonyesha kwamba waumini kama hao wana ufahamu wa kweli kuhusu kiini cha Kristo. Mtu kama huyo pekee ndiye anaweza kusemekana kwamba anamjua Mungu kwa kweli. Kristo ni Mungu wa vitendo mwenye mwili. Wale tu wanaomtambua Kristo na wanaweza kumtii ndio wanamjua Mungu kwa kweli kwa sababu ukweli, njia, na uzima vyote vinatoka kwa Mungu, vyote vinatoka kwa maonyesha ya Kristo mwenye mwili. Isipokuwa Kristo, hakuna mtu anayeweza kusemekana kuwa ukweli, njia, na uzima, watu wachache sana ndio wanalielewa hili. Mungu anatumia uwezo wa mwanadamu kutambua kupata mwili kwa Mungu kama kiwango ambacho Anamjaribia mwanadamu. Wale tu wanaofikia kiwango hiki katika imani yao ndio wanaweza kupata sifa ya Mungu. Wale wote wanaokubali na kutii kupata mwili kwa Mungu ndio washindi ambao wananyakuliwa mbele za Mungu kukamilishwa kwanza. Wale ambao hawawezi kumkubali na kumtii Kristo watatumwa kustahimili mateso ya maafa kwa sababu hawatambui kupata mwili kwa Mungu na wanafikiriwa kuwa wanawali wapumbavu. Kama vile tu Bwana Yesu alipokuja, Aliwaleta juu ya mlima wale waliopenda ukweli na wale waliolikubali neno Lake na waliomfuata kweli, Akiwaongoza na kuwafundisha mwenyewe, huku Akikosa kuwazingatia hata kidogo wale wa ulimwengu wa dini na wale waliomwamini Mungu kwa ajili ya manufaa yao wenyewe kwa sababu walimwamini tu Mungu asiye yakini wa mbingu za juu na hawakukubali kupata mwili kwa Mungu. Walikuwa wasio fahamu katika kutoweza kwao kumtambua Mungu. Kwa hiyo wale tu wanaomkubali na kumtii Kristo mwenye mwili ndio watapokea sifa za Mungu na kukamilishwa na Yeye. Ni kwa nini Kristo pekee ndiye ukweli, njia, na uzima? Hebu tusome kifungu cha neno la Mwenyezi Mungu. “Njia ya maisha si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kumiliki, wala si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kufikia kwa urahisi. Hii ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama kubwa ili mtu aweze kupata uzima, kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ni njia ambayo kwayo mtu hufufuliwa” (“Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Tayari nilishasema Mungu pekee ndiye maisha yasiyobadilika, na Mungu tu ndiye aliye na njia ya maisha. Kwa kuwa maisha Yake ni imara, hivyo ni ya milele; kwa kuwa Mungu tu ndiye njia ya maisha, basi Mungu Mwenyewe ni njia ya uzima wa milele” (“Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu tunaona kwamba ukweli, njia, na uzima vyote vinatoka kwa Mungu. Mungu Mwenyewe pekee Ndiye anamiliki njia ya uzima. Biblia inasema, “Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu” (Yohana 1:1). Neno ni Mungu, Neno ni neno la Mungu. Neno ni ukweli, njia, na uzima. Neno kuwa mwili inahusu Roho wa Mungu aliyetokea katika mwili, yaani, ukweli, njia, na uzima vyote vimekuja katika mwili. Kama vile tu Mwenyezi Mungu anasema, “Neno limepata mwili na Roho wa ukweli amepatikana katika mwili—kwamba ukweli wote, njia, na uzima umekuja katika mwili, Roho wa Mungu hakika amewasili duniani na Roho amekuja katika mwili kwa kweli” (“Utendaji (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kupata mwili kwa Mungu kuwili kunashuhudia ukweli kwamba Yeye ni ukweli, njia, na uzima. Hili lilimpa mwanadamu ufunuo mkuu, lilimwonyesha kwamba Kristo pekee ndiye ukweli, njia, na uzima Maneno na kazi ya Mungu, chote ambacho Anacho na Alicho ni ukweli, njia, na uzima. Hiki ni kiini cha Kristo. Wakati Kristo anaonyesha neno la Mungu, Anafanya hivyo kama Mungu Mwenyewe Akiifanya kazi ya Mungu, Akihitimisha enzi ya awali na kuianzisha mpya, Akifanya kazi ya enzi nzima kwa ajili ya wanadamu wote. Neno la Mungu ambalo Kristo anaonyesha ni ukamilifu wa neno Lake katika hatua moja ya kazi hiyo. Kweli ni maonyesho ya tabia ya Mungu, chote ambacho Mungu anacho na Alicho, siri ya mpango wa usimamizi wa Mungu, na matakwa na kusudi la Mungu kwa wanadamu. Neno lote Lake ni ukweli. Haliwezi tu kufanyiza maisha ya mwanadamu, lakini pia linaweza kumpa mwanadamu uzima. Kama tu wakati Bwana Yesu alikuja, Alionyesha ukweli wote ambao mwanadamu alihitaji katika Enzi ya Neema, Akimruhusu mwanadamu kukiri dhambi zake, kutubu na kurudi mbele za Mungu, Akimfanya mwanadamu kustahili kuomba kwa Mungu na kuja mbele za Mungu kufurahia neema Yake, na kuona huruma na upendo Wake. Hili ni tokeo lililotimizwa na kazi ya ukombozi. Kazi ya Bwana Yesu iliruhusu dhambi za mwanadamu kusamehewa, ikiwakomboa wanadamu kutoka kwa dhambi. Bwana Yesu alitekeleza hatua ya kazi ya kuwakomboa wanadamu, Akiianzisha Enzi ya Neema na Akihitimisha Enzi ya Sheria. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho aliyepata mwili amekuja, Ameonyesha ukweli wote unaotakasa na kuwakomboa wanadamu, na Ametekeleza kazi ya hukumu akianza kwa nyumba ya Mungu, Akimruhusu mwanadamu aone tabia yenye haki na uweza na hekima ya Mungu, Akitakasa na kubadilisha tabia ya maisha ya mwanadamu, ili mwanadamu aweze kumcha Mungu na kuepuka maovu, na ajipokonye kabisa kutoka kwa ushawhisi wa Shetani, arudi mbele za Mungu na apatwe na Mungu. Kazi ya Mwenyezi Mungu inaanzisha Enzi ya Ufalme na inahitimisha Enzi ya Neema. Hili linatuonyesha kwamba yote ambayo Kristo anasema, Anafanya, Anaonyesha na kudhihirisha yote ni ukweli. Kristo pekee ndiye anaweza kumwelekeza mwanadamu kwa njia sahihi, na kumpa mwanadamu ruzuku ya maisha na wokovu, hakuna mwanadamu anayemiliki au anayeweza kuonyesha vitu hivi. Kristo ni kijito cha uzima wa mwanadamu, Yeye ni kuonekana kwa Mungu. Yeye ni ukweli, njia, na uzima, ukombozi na wokovu pekee wa Mungu. Isipokuwa Kristo, hakuna mwanadamu anayemiliki ukweli, na njia, na uzima, ukweli huu ni dhahiri kuona!

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Iliyotangulia: Swali la 6: Katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili na alitumika kama dhabihu ya dhambi kwa ajili ya wanadamu, akiwakomboa kutoka kwa dhambi. Mungu amepata mwili tena katika siku za mwisho na ametamka ukweli na kufanya kazi ya hukumu, akiwatakasa kikamilifu na kuwaokoa wanadamu. Kwa nini Mungu anahitaji kupata mwili mara mbili ili kufanya kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu? Ni nini umuhimu wa kweli wa Mungu kujipatia mwili Mwenyewe mara mbili?

Inayofuata: Swali la 8: Unashuhudia kwamba Mungu kujipatia mwili Mwenyewe katika siku za mwisho kumeanza Enzi ya Ufalme, kuimaliza enzi nzee ya utawala wa Shetani. Tunachotaka kuuliza ni, kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho imemaliza vipi enzi ya giza ya imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini, na ya utawala wa Shetani? Tafadhali shiriki ushirika wenye maelezo.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

2. Sababu ya Mungu kulibariki tu kanisa ambalo huikubali na kuitii kazi Yake, na kwa nini dunia ya kidini imelaaniwa na Mungu

Dhihirisho la wazi zaidi wa kazi ya Roho Mtakatifu ni kwa kuyakumbatia ya sasa, sio kushikilia ya zamani. Wale ambao hawajiendelezi na kazi ya leo, na wale ambao wametengwa na utendaji wa leo, ni wale wanaopinga na hawaikubali kazi ya Roho Mtakatifu. Watu kama hao wanaipinga kazi ya Mungu ya sasa. Ijapokuwa wanashikilia nuru ya zamani, hili halimaanishi kwamba inaweza kukanwa kwamba hawajui kazi ya Roho Mtakatifu. … Walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu daima hudhani wako sahihi, lakini kwa hakika, kazi ya Mungu ndani yao ilisita zamani na kazi ya Roho Mtakatifu haimo ndani yao. Kazi ya Mungu imeshahamishiwa kwa kundi jingine la watu, kundi ambalo kwalo Anapania kukamilishia kazi Yake mpya. Kwani walio katika dini hawawezi kuikubali kazi mpya ya Mungu, na kushikilia tu kazi kongwe za zamani, hivyo Mungu amewaacha watu hawa na anafanya kazi Yake mpya kwa watu wanaoikubali kazi hii mpya. Hawa ni watu wanaoshiriki katika kazi Yake mpya, na usimamizi Wake utatimilika kwa njia hii tu.

3. Waumini lazima waweze kutambua wachungaji wa uwongo na wapinga Kristo ili kwamba kuiacha dini na kurudi kwa Mungu

Wowote wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu ni wale wanaompinga Mungu, na hata zaidi ya hayo ni wale waliofahamu madhumuni ya kazi ya Mungu lakini bado hawatafuti kumridhisha Mungu. Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?

8. Jinsi ambavyo Mungu anatamatisha enzi ya giza ya utawala wa Shetani katika siku za mwisho

Mungu Anakuja miongoni mwa wanadamu siku ya leo kwa kusudi la kubadilisha mawazo na roho zao, na taswira ya Mungu katika mioyo yao ambayo wamekuwa nayo kwa maelfu ya miaka. Kupitia fursa hii, Atamfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Yaani, kupitia maarifa ya mwanadamu, Atabadilisha namna wanavyomfahamu na mitazamo yao Kwake, ili kwamba maarifa yao juu ya Mungu, yaweze kuanza katika rekodi safi, na mioyo yao itakuwa imesafishwa upya na kubadilishwa.

2. Tofauti muhimu kati ya kuokolewa na kufikia wokovu kamili

Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki