156 Mungu Aonyesha Roho ni Nini

1 Anatambua vizuri asili ya mwanadamu, Anaweza kufunua aina za matendo yote yanayohusiana na kila aina ya watu. Ni mzuri hata katika kufunua tabia ya dhambi ya mwanadamu na tabia yake ya uasi. Haishi miongoni mwa watu wa kidunia, lakini Anatambua asili ya watu wenye mwili wa kufa na upotovu wote wa watu wa duniani. Hicho ndicho Alicho. Ingawa Hashughuliki na dunia, Anajua kanuni za kushughulika na dunia, kwa sababu Anaielewa vizuri asili ya mwanadamu.

2 Anajua kuhusu kazi ya Roho ambayo jicho la mwanadamu haliwezi kuiona na kwamba masikio ya mwanadamu hayawezi kusikia, wanadamu wa leo na wanadamu wa enzi zote. Hii inajumuisha hekima ambayo sio falsafa ya kuishi na makuu ambayo ni ngumu kwa watu kuelewa. Hiki ndicho Alicho, kuwekwa wazi kwa watu na pia kufichika kwa watu. Kile Anachoonyesha sio kile ambacho mwanadamu asiye wa kawaida alicho, bali ni tabia za asili na uungu wa Roho.

3 Hasafiri ulimwenguni mzima lakini anajua kila kitu kuhusu ulimwengu. Anawasiliana na “sokwe” ambao hawana maarifa au akili, lakini Anaonyesha maneno ambayo ni ya kiwango cha juu kuliko maarifa na juu ya watu wakubwa duniani. Anaishi miongoni mwa kundi la wanadamu wapumbavu na wasiojali ambao hawana ubinadamu na ambao hawaelewi mila na desturi za ubinadamu na maisha, lakini Anaweza kumwambia mwanadamu kuishi maisha ya kawaida, na kwa wakati uo huo kufichua ubinadamu duni na wa chini wa binadamu. Haya yote ndiyo kile Alicho, mkuu kuliko vile ambacho mwanadamu yeyote wa damu na nyama alicho.

4 Kumweka wazi na kumhukumu wanadamu sio maonyesho wa uzoefu wa mwili Wake; ni kufichua vile mwanadamu asivyokuwa na haki baada ya kufahamu kutotii kwa mwanadamu na kuchukia upotovu wa mwanadamu. Kazi yote Anayoifanya ni kufichua tabia Yake kwa mwanadamu na kuonyesha asili Yake. Ni Yeye tu ndiye anayeweza kuifanya kazi hii, sio kitu ambacho mtu mwenye mwili na damu anaweza kukipata.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 155 Mwili na Roho ya Mungu ni Sawa Kiasili

Inayofuata: 157 Mwana wa Adamu Mwenye Mwili ni Mungu Mwenyewe

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp