Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 165

30/07/2020

Kila hatua ya kazi ya Mungu hufuata mkondo mmoja na sawa, na hivyo katika mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, kila hatua imefuatwa kwa karibu na ifuatayo, kutoka msingi wa dunia hadi leo. Kama hakungekuwa na mtu wa kupisha njia, hakungekuwa na mtu wa kuja baadaye; Kwani kuna wale wanaokuja baadaye, kuna wale wanaopisha njia. Kwa njia hii kazi imepitishwa chini, hatua kwa hatua. Hatua moja inafuata ingine, na bila mtu wa kufungua njia, haitawezekana kuanza kazi, na Mungu angekosa namna ya kupeleka kazi Yake mbele. Hakuna hatua inayopingana na nyingine, na kila hatua inafuata nyingine katika mlolongo kuunda mkondo; hii yote inafanywa na Roho Yule Yule. Lakini bila kujali iwapo mtu atafungua njia, ama kuendeleza kazi ya mwingine, hii haiamui utambulisho wake. Hii si sawa? Yohana aliifungua njia, na Yesu akaendeleza kazi yake, hivyo hii inathibitisha kwamba utambulisho wa Yesu ni chini kuliko wa Yohana? Yehova alifanya kazi Yake kabla Yesu, hivyo unaweza kusema kuwa Yehova ni mkubwa kumliko Yesu? Iwapo waliopasha njia ama kuendeleza kazi za wengine sio muhimu; kilicho muhimu ni kiini cha kazi zao, na utambulisho unaowakilishwa. Hii si sawa? Kwa vile Yesu alinuia kufanya kazi miongoni mwa wanadamu, ilimbidi Awainue wale ambao wangefanya kazi ya kupasha njia. Yohana alipoanza tu kuhubiri, alisema, “Itayarisheni ninyi njia ya Bwana, yafanyeni mapito yake kuwa nyoofu. Ninyi tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni uko karibu.” Aliongea hivi tangu mwanzoni, na mbona aliweza kuyasema maneno haya? Kwa suala la utaratibu ambao maneno haya yalisemwa, ni Yohana aliyezungumzia kwanza injili ya ufalme wa mbinguni, na Yesu aliyezungumza baadaye. Kulingana na dhana za mwanadamu, ni Yohana aliyeifungua njia mpya, na bila shaka Yohana alikuwa mkubwa kumliko Yesu. Lakini Yohana hakusema yeye ni Kristo, na Mungu hakumshuhudia kama Mwana mpendwa wa Mungu, lakini Alimtumia tu kufungua na kuandaa njia ya Bwana. Alimpisha Yesu njia, lakini hangefanya kazi kwa niaba ya Yesu. Kazi zote za mwanadamu pia zilidumishwa na Roho Mtakatifu.

Katika enzi ya Agano la Kale, ni Yehova aliyeongoza njia, na kazi ya Yehova iliwakilisha enzi nzima ya Agano la Kale, na kazi zote zilizofanywa Israeli. Musa tu alizingatia hizi kazi duniani, na kazi zake zinahesabika kama ushirikiano uliotolewa na mwanadamu. Wakati huo, Yehova ndiye aliyezungumza, na Akamwita Musa, na kumlelea miongoni mwa watu wa Israeli, na kumfanya Musa kuwaongoza nyikani hadi Kanaani. Hii haikuwa kazi ya Musa mwenyewe, lakini hiyo iliyoagizwa kibinafsi na Yehova, na hivyo Musa hawezi kuitwa Mungu. Musa pia aliiweka chini sheria, lakini sheria hii iliamrishwa kibinafsi na Mungu aliyeifanya izungumzwe na Musa. Yesu pia alitengeneza amri, na kuondoa sheria ya Agano la Kale na kuweka amri ya enzi jipya. Mbona Yesu ni Mungu Mwenyewe? Kwa sababu haya si mambo sawa. Wakati huo, kazi aliyoifanya Musa haikuwakilisha enzi, wala haikufungua njia mpya; alielekezwa mbele na Yehova, na alikuwa tu anatumiwa na Mungu, Yesu alipokuja, Yohana alikuwa amefanya hatua ya kazi ya kupisha njia, na alikuwa ashaanza kueneza injili ya ufalme wa mbinguni (Roho Mtakatifu alikuwa ameanza hii). Yesu alipojitokeza, Alifanya moja kwa moja kazi Yake Mwenyewe, lakini kulikuwa na tofauti kubwa kati ya kazi Yake na kazi na matamshi ya Musa. Isaya pia alizungumzia unabii mwingi, lakini mbona yeye hakuwa Mungu Mwenyewe? Yesu hakuzungumzia unabii mwingi lakini mbona Alikuwa Mungu Mwenyewe? Hakuna anayethubutu kusema kwamba kazi zote za Yesu wakati huo zilitoka kwa Roho Mtakatifu, wala hathubutu kusema zote zilitoka kwa matakwa ya mwanadamu, ama zilikuwa kabisa kazi za Mungu Mwenyewe. Mwanadamu hana njia yoyote ya kuchambua mambo haya. Inaweza kusemwa kwamba Isaya alifanya kazi kama hiyo, na kuzungumzia unabii huo, na yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu; hayakutoka moja kwa moja kwa Isaya mwenyewe, lakini yalikuwa ufunuo kutoka kwa Yehova. Yesu hakufanya kazi nyingi sana, na Hakusema maneno mengi sana, wala Hakuzungumzia unabii mwingi. Kwa mwanadamu, mahubiri Yake hayakuonekana hasa ya kupandishwa cheo, lakini alikuwa Mungu Mwenyewe, na mwanadamu hawezi kueleza haya. Hakuna aliyewahi kumwamini Yohana, ama Isaya, ama Daudi, wala hakuna aliyewahi kuwaita Mungu, ama Daudi Mungu ama Yohana Mungu, hakuna aliyewahi kuzungumza hivi, na ni Yesu tu aliyewahi kuitwa Kristo. Uainishaji huu umefanywa kulingana na ushahidi wa Mungu, kazi Aliyoifanya, na huduma Aliyoifanya. Kuhusu watu wakuu wa Biblia—Ibrahimu, Daudi, Yoshua, Danieli, Isaya, Yohana na Yesu—kupitia kazi waliyoifanya, unaweza kusema ni nani aliye Mungu Mwenyewe, na ni watu wapi walio manabii, na ni wapi walio mitume. Ni nani aliyetumiwa na Mungu, na nani aliyekuwa Mungu Mwenyewe, inatofautishwa na kuamuliwa na asili na aina za kazi walizozifanya. Iwapo huwezi kusema tofauti, basi hii inadhihirisha kwamba hujui maana ya kumwamini Mungu. Yesu ni Mungu kwa sababu Alizungumza maneno mengi, na kufanya kazi nyingi hasa maonyesho Yake ya miujiza nyingi. Vivyo hivyo, Yohana, pia alifanya kazi nyingi, na kuzungumza maneno mengi, Musa pia; mbona hawakuitwa Mungu? Adamu aliumbwa moja kwa moja na Mungu; mbona hakuitwa Mungu, badala tu ya kuitwa kiumbe? Mtu akikwambia, “Leo, Mungu amefanya kazi nyingi sana, na kuzungumza maneno mengi; Yeye ni Mungu Mwenyewe. Basi, vile Musa alivyozungumza maneno mengi, lazima yeye pia ni Mungu Mwenyewe!” inapaswa uwarudishie swali, “Wakati huo, mbona Mungu alimshuhudia Yesu, na sio Yohana, kama Mungu Mwenyewe? Je, Yohana hakumtangulia Yesu? Ni ipi iliyokuwa kubwa, kazi ya Yohana ama Yesu? Kwa mwanadamu, Yohana anakaa mkubwa kumliko Yesu, lakini mbona Roho Mtakatifu alimshuhudia Yesu, na sio Yohana?” Hiki kitu kimoja kinafanyika leo! Mwanzoni, Musa alipowaongoza watu wa Israeli, Yehova alimwongelesha kutoka miongoni mwa mawingu. Musa hakuzungumza moja kwa moja lakini badala yake aliongozwa moja kwa moja na Yehova. Hii ilikuwa kazi ya Israeli ya Agano la Kale. Ndani ya Musa hamkuwa na Roho, ama nafsi ya Mungu. Hangeweza kufanya kazi hiyo, na hivyo kuna tofauti kubwa kati ya aliyoifanya na Yesu. Na hiyo ni kwa sababu kazi walizozifanya zilikuwa tofauti! Iwapo mtu anatumiwa na Mungu, ama ni nabii, mtume, ama Mungu Mwenyewe, unaweza kubainishwa na asili ya kazi yake, na hii itakomesha mashaka yenu, Kwa Biblia, imeandikwa kwamba Kondoo peke yake ndiye anayeweza kuivunja mihuri saba. Kupitia zama zote kumekuwa na wachambuzi wengi wa maandiko miongoni mwa watu wakuu, na hivyo unaweza kusema kwamba wote ni Kondoo? Unaweza kusema kwamba maelezo yao yote yalitoka kwa Mungu? Walikuwa tu wachambuzi; hawana utambulisho wa Kondoo. Wanastahilije kuivunja mihuri saba? Ni ukweli kwamba “Kondoo peke yake anaweza kuivunja mihuri saba,” Lakini Hakuji tu kuivunja mihuri saba; hakuna umuhimu wa kazi hii, inafanywa kwa bahati. Yeye yu wazi kabisa kuhusu kazi Yake Mwenyewe; ni muhimu Kwake kutumia muda mwingi kutafsiri maandiko? Ni lazima “enzi ya Kondoo ya kuitafsiri maandiko” iongezwe kwa kazi ya miaka elfu sita? Anakuja kufanya kazi mpya, lakini pia Anatoa ufunuo kadhaa kuhusu kazi za nyakati za zamani, kufanya watu waelewe ukweli wa kazi ya miaka elfu sita. Hakuna haja ya kueleza vifungo vingi kutoka Biblia; kazi ya leo ndiyo iliyo kuu, hiyo ni muhimu. Unapaswa kujua kwamba Mungu haji hasa kuivunja muhiri saba, ila kufanya kazi ya wokovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp