Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu | Dondoo 145

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu | Dondoo 145

119 |18/06/2020

Haijalishi unatafuta kwa njia gani, unapaswa kuelewa kazi ambayo Mungu anaifanya leo, na uapaswa kuelewa umuhimu wa kazi hii. Unapaswa kuelewa na kujua ni kazi gani ambayo Mungu anaileta, Atakapokuja katika siku za mwisho, tabia Anayoileta, na kile kitakachofanywa kikamilifu kwa mwanadamu. Ikiwa hujui au huielewi kazi ambayo Amekuja kuifanya katika mwili, basi unawezaje kutafuta mapenzi Yake, na unawezaje kuwa mwandani wake? Kwa kweli, kuwa mwandani wa Mungu si vigumu, lakini pia si rahisi. Ikiwa mwanadamu anaweza kuelewa maana, basi anaweza kutekeleza, na hivyo si ngumu; ikiwa mwanadamu hawezi kuelewa maana, basi inakuwa vigumu zaidi, na zaidi, mwanadamu ataangukia kwenye dhana za kufikirika. Ikiwa, katika kumtafuta Mungu, mwanadamu hana msimamo wake wa kusimamia, na hajui ni ukweli gani anapaswa kuufuata, basi ina maana kwamba hana msingi, na hivyo si rahisi kwake kusimama imara. Leo, kuna wengi ambao hawauelewi ukweli, ambao hawawezi kutofautisha kati ya wema na uovu au kipi cha kupenda na kipi cha kuchukia. Watu kama hawa ni vigumu kusimama imara. Kitu cha msingi katika imani kwa Mungu ni kuwa na uwezo wa kuweka ukweli katika matendo, kujali mapenzi ya Mungu, kujua kazi ya Mungu kwa mwanadamu anapokuja katika mwili na kanuni ambazo kwazo Anazungumza; usifuate wengi, na unapaswa kuwa na kanuni katika kile unachokiingia, na unapaswa kuzisimamia. Kuyashikilia imara mambo ambayo yameangaziwa na Mungu kwako ni msaada kwako. Ikiwa hutafanya hivyo, leo utakwenda njia hii, kesho utakwenda nyingine, na hutapata kitu chochote halisi. Kuwa hivi hakuna manufaa yoyote katika maisha yako. Wale ambao hawauelewi ukweli siku zote wanawafuata wengine. Ikiwa watu wanasema kwamba hii ni kazi ya Roho Mtakatifu, basi, wewe pia utasema ni kazi ya Roho Mtakatifu; ikiwa watu watasema ni kazi ya roho mchafu, basi wewe pia utatilia mashaka, au utasema ni kazi ya roho mchafu. Siku zote unakuwa kama kasuku kwa maneno ya wengine, na huwezi kutofautisha kitu chochote wewe mwenyewe, wala huwezi kufikiri kwa ajili yako mwenyewe. Huyu ni mtu ambaye hana msimamo, ambaye hana uwezo wa kutofautisha—mtu wa aina hiyo ni masikini asiyejitambua. Watu kama hao siku zote wanarudia maneno ya wengine: Leo inasemwa kuwa hii ni kazi ya Roho Mtakatifu, lakini kuna uwezekano siku moja mtu atasema si kazi ya Roho Mtakatifu, na si chochote bali matendo ya mwanadamu—halafu huwezi kuelewa, na utakaposhuhudia watu wengine wanasema hivyo, nawe pia unasema kitu kile kile. Kwa kweli ni kazi ya Roho Mtakatifu, lakini unasema ni kazi ya mwanadamu; hujawa mmoja wa wale wanaoikufuru kazi ya Roho Mtakatifu? Katika hili, hujampinga Mungu kwa sababu huwezi kutofautisha? Nani ajuaye, siku moja mtu atatokea na kusema “hii ni kazi ya roho mchafu,” na utakaposikia maneno haya utapotea, na kwa mara nyingine tena unafungwa na maneno ya wengine. Kila wakati mtu anachochea usumbufu huwezi kusimama katika msimamo wako, na hii ni kwa sababu huna ukweli ndani yako. Kuamini katika Mungu na kutafuta maarifa ya Mungu si jambo rahisi. Hayawezi kupatikana kwa kukusanyika pamoja na kusikiliza mahubiri, na huwezi kukamilishwa kwa kupenda tu. Lazima upitie uzoefu, na ujue, na kuongozwa na kanuni katika matendo yako, na kupata kazi za Roho Mtakatifu. Utakapopitia katika uzoefu, utakuwa na uwezo wa kutofautisha mambo mengi—utakuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya jema na baya, kati ya haki na uovu, kati ya kile ambacho ni cha mwili na damu na kile ambacho ni cha kweli. Unapaswa kuwa na uwezo wa kutofautisha mambo haya yote, na kwa kufanya hivyo, haijalishi ni mazingira gani, hutapotea kamwe. Hiki ndicho kitakuwa kimo chako halisi.

Umetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi