Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 8

18/05/2020

Tembea katika Njia ya Mungu: Mche Mungu na Kuepuka Maovu

Kunao msemo ambao mnafaa kutilia maanani. Ninasadiki msemo huu ni muhimu sana, kwa sababu kwangu Mimi unakuja akilini mara nyingi kila siku. Kwa nini hivyo? Kwa sababu kila wakati Ninapokumbana na mtu, kila wakati Ninaposikia hadithi ya mtu, kila wakati Ninaposikia kile alichopitia mtu au ushuhuda wake wa kusadiki Mungu, siku zote Ninatumia msemo huu kuweza kupima kama mtu huyu binafsi ni mtu wa aina ambayo Mungu anataka au la, mtu wa aina ambayo Mungu anapenda. Hivyo msemo huu ni upi, basi? Sasa nyinyi nyote mnasubiri kwa hamu. Nitakapoufichua msemo huu, pengine mtakasirika kwa sababu wapo baadhi yenu ambao mmekuwa mkijifanya kuwa mnakubaliana nao kwa miaka mingi. Lakini Kwangu Mimi, Sijawahi kujifanya kuwa nakubaliana nao. Msemo huu umo moyoni Mwangu. Hivyo basi msemo huu ni upi? Msemo ni “tembea katika njia ya Mungu: mche Mungu na kuepuka maovu.” Je, huoni kwamba kauli hii ni rahisi kupindukia? Ilhali ingawa msemo huu unaweza kuwa rahisi, mtu ambaye anao uelewa wa ndani na wa kweli wa msemo huu atahisi kwamba ni wenye uzito mkubwa; kwamba unao thamani nyingi ya kutenda; kwamba ni lugha ya uzima iliyo na uhalisia wa ukweli; ambayo ni lengo la maishani katika kulenga wale wanaotafuta kutosheleza Mungu; na hiyo ni njia ya maisha marefu itakayofuatwa na mtu yeyote anayejali nia za Mungu. Hivyo basi mnafikiria nini: Je, msemo huu ni ukweli? Je, unao aina hii ya umuhimu? Pengine wapo baadhi ya watu wanaofikiria kuhusu msemo huu, wakijaribu kuuelewa, na wapo baadhi ambao bado wanautilia shaka. Je, msemo huu ni muhimu sana? Je, ni muhimu sana? Unahitajika sana na unastahili kutiliwa mkazo? Pengine wapo baadhi ya watu ambao hawapendi sana msemo huu kwa sababu wanafikiria kwamba kuchukua njia ya Mungu na kuitiririsha ndani ya msemo huu mmoja ni urahisishaji wa kupindukia. Kuyachukua yale yote ambayo Mungu alisema na kuyafanya yawe msemo mmoja—je, hivi si kumfanya Mungu kuwa yule asiyekuwa na umuhimu sana? Hivi ndivyo ilivyo? Inaweza kuwa kwamba wengi wenu nyinyi hamwelewi kabisa maana kuu ya maneno haya. Ingawa mmeyanakili na kuyatilia maanani, hamnuii kuuweka msemo huu katika mioyo yenu; mnaunakili tu, na kuudurusu tu, na kuufikiri katika muda wenu wa ziada. Wapo baadhi ya watu ambao hata hawatashughulika kuutia kwenye kumbukumbu msemo huu, sikuambii hata kujaribu kuutumia vizuri. Lakini kwa nini Nikauzungumzia msemo huu? Licha ya mtazamo wenu, au kile mtakachofikiria, lazima Nizungumzie msemo huu kwa sababu unafaa ajabu namna ambavyo Mungu huasisi matokeo ya binadamu. Bila kujali kama uelewa wenu wa sasa wa msemo huu upo, namna mnavyouchukulia, bado Nitawaeleza: Kama mtu anaweza kuutenda msemo huu kwa njia bora na kutimiza kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, basi atahakikishiwa kuishi, kisha atahakikishiwa kuwa mtu mwenye matokeo mazuri. Kama huwezi kutimiza kiwango kilichowekwa wazi katika msemo huu, basi inaweza kusemekana kwamba matokeo yako hayajulikani. Hivyo basi Ninaongea kwenu kuhusu msemo huu kwa matayarisho yenu ya kiakili, na ili mjue ni kiwango aina gani ambacho Mungu anatumia kuwapima.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp