Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatima na Matokeo | Dondoo 592

10/10/2020

Wakati mtu anafanikiwa kupata maisha ya ukweli ya mwanadamu duniani, vikosi vizima vya Shetani vitafungwa, na mwanadamu ataishi kwa urahisi katika ardhi. Mambo hayatakuwa magumu kama yalivyo sasa: Mahusiano ya binadamu, mahusiano ya kijamii, mahusiano changamani ya kifamilia…, haya ni ya kusumbua, machungu mno! Maisha ya mwanadamu hapa ni duni! Punde tu mwanadamu anaposhindwa, moyo wake na akili yake vitabadilika: atakuwa na moyo unaomcha Mungu na moyo ambao unampenda Mungu. Punde tu wote walio ulimwenguni ambao wanatafuta upendo wa Mungu wanaposhindwa, ambayo ni kusema, punde tu Shetani anaposhindwa, na punde tu Shetani—nguvu zote za giza—zimekwisha fungwa, basi maisha ya mwanadamu duniani yatakuwa yasiyotaabishwa, na ataweza kuishi huru duniani. Kama maisha ya mwanadamu hayana mahusiano ya kimwili, na hayana changamani za mwili, basi itakuwa rahisi mno. Mahusiano ya kimwili ya mwanadamu ni changamani mno, na kwa mwanadamu kuwa na mambo kama hayo ni thibitisho kuwa yeye bado hajajikomboa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kama ungekuwa na uhusiano sawa na ndugu na dada, kama ungekuwa na uhusiano sawa na familia yako ya kawaida, basi hungekuwa na wasiwasi, na hungekuwa na haja ya kuhofia kuhusu mtu yeyote. Hakuna kitakachoweza kuwa bora zaidi, na kwa njia hii mwanadamu atapunguziwa nusu ya mateso yake. Kuishi maisha ya kawaida ya binadamu duniani, mwanadamu atakuwa sawa na malaika; ingawa atakuwa bado na mwili, atakuwa sawa na malaika. Hii ni ahadi ya mwisho, ni ahadi ya mwisho ambayo mwanadamu amezawadiwa. Leo mwanadamu anapitia kuadibu na hukumu; Je, unafikiri matukio kama haya ya mwanadamu hayana maana? Je, kazi ya kuadibu na kuhukumu inaweza kufanywa bila sababu. Hapo awali ilisemekana kuwa kuadibu na kuhukumu mwanadamu ni kumweka katika shimo lisilo na mwisho, ambayo ina maana ya kuchukua majaliwa na matarajio. Hii ni kwa ajili ya jambo moja: utakasaji wa mwanadamu. Mwanadamu hawekwi kwenye shimo lisilo na mwisho kimakusudi, ambapo baadaye Mungu hukata tamaa juu yake. Badala yake, ni ili kushughulika na uasi ndani ya mwanadamu, ili hatimaye mambo ndani ya mwanadamu yaweze kutakasika, ili aweze kuwa na ufahamu wa kweli wa Mungu, na awe kama mtu mtakatifu. Iwapo hii itafanywa, basi yote yatakuwa yametimia. Kwa kweli, wakati mambo hayo ndani ya mwanadamu ambayo yanapaswa kushughulikiwa yameshughulikiwa, na mwanadamu anakuwa na ushuhuda wa mwangwi, Shetani pia atashindwa, na hata ingawa kunaweza kuwa na mambo machache ambayo awali ndani ya mwanadamu hayakuwa yametakasika kabisa, punde tu Shetani ameshindwa, Shetani hawezi tena kusababisha taabu, na wakati huo mwanadamu atakuwa ametakaswa kabisa. Mwanadamu hajawahi kupitia maisha kama haya, lakini wakati Shetani anashindwa, yote yatakuwa yametulizwa na mambo hayo pumbavu ndani ya mwanadamu yatatatuliwa yote; matatizo mengine yote yataisha punde tu tatizo kuu litakapokuwa limetatuliwa. Wakati wa kupata kwa mwili kwa Mungu duniani, wakati Yeye binafsi anafanya kazi miongoni mwa watu, kazi yote ambayo Yeye hufanya ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na Yeye atamshinda Shetani kupitia kumshinda mwanadamu na kuwafanya kamili. Wakati nyinyi mtakuwa na ushuhuda wa ajabu, hii, pia, itaonyesha kushindwa kwa Shetani. Kwanza mwanadamu anashindwa na hatimaye anafanywa kamili kabisa ili kumshinda Shetani. Kwa kiini, hata hivyo, pamoja na kushindwa kwa Shetani hii pia vilevile ni wokovu wa wanadamu wote kutoka kwa shimo la bahari hii ya mateso. Bila kujali kama kazi hii inatendeka katika ulimwengu mzima au katika nchi ya China, yote ni kwa ajili ya kumshinda Shetani na kuleta wokovu kwa wanadamu wote ili mwanadamu aweze kuingia pahali pa kupumzika. Unaona, mwili wa kawaida wa Mungu mwenye mwili ni kwa usahihi kwa ajili ya kumshinda Shetani. Kazi ya Mungu mwenye mwili ni kuleta wokovu kwa wale wote walioko chini ya mbingu wanaompenda Mungu, ni kwa ajili ya kushinda wanadamu wote, na, zaidi ya hayo, kwa ajili ya kumshinda Shetani. Msingi wa kazi yote ya Mungu ya usimamizi haitengani na kushindwa kwa Shetani ili kuleta wokovu kwa watu wote. Kwa nini, katika mengi ya kazi hii, daima inasemekana kwenu kuwa na ushuhuda? Na ushuhuda huu unaelekezewa nani? Je, si unaelekezwa kwa Shetani? Ushuhuda huu unafanyiwa Mungu, na unafanywa ili kushuhudia kuwa kazi ya Mungu imetimiza matokeo yake. Kuwa na ushuhuda inahusiana na kazi ya kumshinda Shetani; kama hakungekuwa na vita dhidi ya Shetani, basi mwanadamu hangetakiwa kuwa na ushuhuda. Ni kwa sababu kwamba Shetani lazima ashindwe, kwa wakati huo huo kama kuokoa mwanadamu, Mungu anataka kwamba mwanadamu awe na ushuhuda wake mbele ya Shetani, ambao Yeye hutumia kufanya vita na Shetani. Kwa hivyo, mwanadamu ni mlengwa wa wokovu na chombo cha kumshinda Shetani, na kwa hivyo mwanadamu yumo katika msingi wa usimamizi mzima wa Mungu, na Shetani ni mlengwa wa uharibifu, adui. Unaweza kuhisi kuwa haujafanya kitu chochote, lakini kwa sababu ya mabadiliko katika tabia yako, umekuwa na ushuhuda, na ushuhuda huu unaelekezwa kwa Shetani na haufanywi kwa mwanadamu. Mwanadamu hajafaa ili afurahie ushuhuda kama huu. Je, jinsi gani yeye ataweza kuelewa kazi inayofanywa na Mungu? Mlengwa wa vita vya Mungu ni Shetani; mwanadamu, wakati huo huo, ni mlengwa wa wokovu. Mwanadamu ana tabia potovu ya kishetani, na hana uwezo wa kuelewa kazi hii. Hii ni kwa sababu ya kupotoshwa na Shetani. Sio kwa asili ya ndani ya mtu, bali inaelekezwa na Shetani. Leo, kazi kuu ya Mungu ni kumshinda Shetani, yaani, kumshinda mwanadamu kabisa, ili kwamba mwanadamu awe na ushuhuda wa mwisho wa Mungu mbele ya Shetani. Kwa njia hii, mambo yote yatatimika. Kwa matukio mengi, kwa macho yako pekee inaonekana kwamba hakuna chochote ambacho kimefanyika, lakini kwa kweli, kazi tayari imekamilika. Mwanadamu anahitaji kwamba kazi yote iliyokamilika iwe ya kuonekana, bali bila kuifanya inayoonekana wazi kwako, Nimemaliza kazi yangu, kwa kuwa Shetani ametii, ambayo ina maana kuwa yeye ameshindwa kabisa, ya kuwa busara yote ya Mungu, nguvu na mamlaka yamemshinda Shetani. Huu ndiyo ushuhuda mahsusi ambao ni lazima mtu awe nao, na ingawa haijidhihirishi kwa uwazi katika mwanadamu, ingawa haionekani kwa macho pekee, Shetani tayari ameshindwa. Ujumla wa kazi hii lazima uelekezwe dhidi ya Shetani, na inafanyika kwa ajili ya vita dhidi ya Shetani. Kwa hivyo, kuna mambo mengi ambayo mwanadamu haoni kuwa ni mafanikio, lakini ambayo, machoni pa Mungu, yalikuwa na mafanikio kwa muda mrefu uliopita. Hii ni moja ya ukweli wa ndani wa kazi yote ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

God Became Flesh to Defeat Satan and Save Man

I

During this incarnation of God on earth, He does His work among man. All of this work has one purpose: to defeat the devil Satan. He will defeat Satan through conquering man, also through making you complete. When you bear resounding testimony, this, too, will be a mark of Satan’s defeat. God is incarnated just to defeat Satan and save all mankind.

II

In order for Satan to be defeated, man is first conquered, then made complete. But in substance, while defeating Satan, God saves man from the world of pain. No matter if this work is carried out in China or throughout the universe, it’s all to defeat Satan and save mankind, so that man can enter the place of rest. Refrain God is incarnated just to defeat Satan and save all mankind.

III

The incarnation of God in the ordinary flesh is precisely for the sake of defeating Satan. The work of this God of flesh is to save all those who love God beneath heaven. It’s for the sake of conquering all mankind, and also for the sake of defeating Satan. The core of all God’s work is inseparable from defeating Satan for mankind’s salvation. God is incarnated just to defeat Satan and save all mankind. God is incarnated just to defeat Satan and save all mankind, save all mankind. He’s saving all mankind.

from Follow the Lamb and Sing New Songs

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp