Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Tabia ya Mungu na Kile Anacho na Alicho | Dondoo 238

09/11/2020

Kazi Niliyopanga inaendelea kusonga mbele bila kukoma hata kwa muda kidogo. Baada ya kuingia katika Enzi ya Ufalme, na baada ya kukuweka katika ufalme Wangu kama watu Wangu, Nitakuwa na madai mengine ya kuweka dhidi yako; Hiyo ni kusema, Nitaanza kutangaza rasmi na kueneza mbele yako katiba ambayo Nitatumia kuongoza enzi hii:

Kwa sababu mnaitwa watu Wangu, mnapaswa kuwa na uwezo wa kulitukuza jina Langu, kumaanisha, kusimama katika ushuhuda wakati wa majaribio. Mtu yeyote akijaribu kunidanganya na kunificha ukweli, au kushiriki katika shughuli zisizo za heshima nyuma Yangu, bila ubaguzi Nitamfukuza nje, aondolewe kutoka kwa nyumba Yangu awe akisubiri hukumu. Wale ambao hawajakuwa waaminifu na watiifu Kwangu katika siku za mbeleni, na leo hii wanainuka na kunihukumu hadharani, wao pia watafukuzwa kutoka kwa nyumba Yangu. Wale ambao ni watu Wangu lazima wajali kuhusu mizigo Yangu kila mara na vile vile kutafuta kujua maneno Yangu. Ni watu kama hawa tu ndio Nitakaowapa nuru, na wao kwa hakika wataishi chini ya uongozi Wangu na kupata nuru, na kamwe hawatakutana na kuadibu. Wale ambao, kwa kutojali mizigo Yangu, wanamakinika na mipango ya hatima yao wenyewe, yaani, wale ambao hawalengi kwa matendo yao kukidhi Moyo Wangu bali wanataka kuomba omba vya bure, viumbe hawa wanaofanana na waombaji, Ninakataa kata kata kuwatumia, kwa sababu tangu walipozaliwa hawajui chochote kuhusu maana ya kujali mizigo Yangu. Wao ni watu wenye akili isiyokuwa ya kawaida; watu kama hawa wanaugua kutokana na “utapiamlo” wa ubongo, na wanastahili kwenda nyumbani wapate “lishe.” Siwahitaji watu wa aina hii. Miongoni mwa watu Wangu, kila mtu atatakiwa kuzingatia kuwa kunijua ni wajibu unaotakiwa kutekelezwa mpaka mwisho, kama kula, kuvaa, na kulala, mambo ambayo mtu kamwe hawezi kusahau hata kwa muda mfupi, ili kwamba mwishowe kunijua litakuwa jambo la kawaida kama vile kula, jambo ambalo wewe hufanya bila jitihada yoyote, kwa mkono uliozoea. Kuhusu maneno Ninayoyanena, Kila neno lazima lichukuliwe kwa uhakika mkubwa na lichukuliwe kikamilifu; hakuwezi kuwa na hatua nusu za uzembe katika kutimiliza haya. Mtu asiyekuwa makini na maneno Yangu ataonekana kama ananipinga Mimi kwa uwazi; mtu yeyote asiyeyala maneno Yangu, au hatafuti kuyajua, ataonekana kama ambaye hanizingatii, na bila kusita atafagiliwa nje ya mlango wa nyumba Yangu. Kwa maana, kama Nilivyosema zamani, Ninachotaka sio watu wengi ila wateule wachache. Kati ya watu mia, kama mmoja tu ataweza kunijua kupitia maneno Yangu, basi bila kusita Ningewatupilia mbali wengine wote ili Nizingatie kumpa nuru na kumweka katika mwanga mmoja huyu. Kutokana na hili unaweza kuona kuwa si mbali na ukweli kwamba idadi kubwa pekee ndio inaweza kunidhihirisha, kuishi kwa maisha ya Kimungu. Ninachotaka ni ngano (hata ingawa viini vya mbegu havijajaa) na sio vigugu mwitu (hata kama viini vyake vimejaa vya kutosha na ni vya kutamanika). Na kwa wale wasiojali kuhusu kutafuta lakini badala yake kuwa na tabia za kuzembea, wanapaswa kuondoka kwa hiari yao wenyewe; Mimi sitaki kuwaona tena, wasije wakaleta aibu kwa jina Langu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 5

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp