Ndio Nimeanza Tu Kutembea Njia Sahihi ya Uzima

16/01/2018

Shi Han Mkoa wa Hebei

Nilizaliwa kwa familia maskini ya wakulima. Nimekuwa mwenye busara tangu utotoni, ikimaanisha sijawahi kupigana na watoto wengine na niliwatii wazazi wangu, jambo lililonifanya “msichana mzuri” wa kawaida machoni mwa watu wazima. Wazazi wengine wote walikuwa na wivu sana kwa wazazi wangu, wakisema kuwa walikuwa na bahati kuwa na binti mzuri hivyo. Na hivi tu, nilikua kila siku nikisikiliza sifa kutoka kwa watu waliokuwa karibu nami. Nilipokuwa katika shule ya asili, rekodi yangu ya kitaaluma ilikuwa nzuri hasa, na daima nilipata nafasi ya kwanza katika mitihani. Wakati mmoja, nilipokea alama zote katika mashindano ya insha yaliyofanywa na mji wangu, nikishinda heshima kwa shule yangu. Mwalimu mkuu hakunipa tu tuzo na cheti, lakini pia alinipongeza mbele ya shule nzima na akawaagiza wanafunzi kujifunza kutoka kwangu. Ghafla nikawa “mtu maarufu” wa shule, na wanafunzi wenzangu hata wakanipa jina la utani la “generali wa ushindi milele.” Sifa kutoka kwa walimu wangu, wivu wa wanafunzi wenzangu, na kutunuka kwa wazazi wangu kulinipa hisia ya ukubwa katika moyo wangu, na kwa kweli nilifurahia hisia ya kupendwa na kila mtu. Kwa hivyo, nilisadikisha kabisa kwamba furaha kubwa zaidi katika maisha ilikuwa upendezwaji wa wengine, na kwamba hisia ya furaha ilitoka kwa sifa ya wengine. Nilijiambia kwa siri: Bila kujali jinsi mambo yalivyo magumu na ya kuchosha, ni lazima niwe mtu wa sifa na hadhi, na kamwe kutoangaliwa tena kwa dharau na wengine. Kutoka wakati huo na kwendelea, misemo kama vile “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo” na “Watu daima wanapaswa kujitahidi kuwa bora kuliko watu wao wa hirimu” ikawa miito yangu ya maisha.

Hata hivyo, nilipokuwa na umri wa miaka 13, baba yangu alikuwa mgonjwa sana na akalazwa hospitalini, jambo ambalo liliweka familia yetu iliyokuwa maskini tayari kuwa na deni kubwa. Nilipomwona baba yangu akilia kwa maumivu ya ugonjwa na mama yangu akijichosha kwa ajili ya riziki yetu, nilihisi vibaya sana kiasi kwamba nilitamani kukua haraka ili niweze kushiriki katika huzuni na maumivu yao. Kwa hiyo nilifanya uamuzi mchungu wa kuacha shule, nikifikiri: Hata nisipoenda shule, siwezi kutenda vibaya zaidi kuliko wengine. Nitakuwa mwanamke mwenye nguvu na mwenye mafanikio nitakapokua, na kisha nitaweza kuishi maisha mazuri! Kutokana na ubora wangu wa kitaaluma, nilikuwa kama “mtu mdogo maarufu” katika ujirani wangu. Kwa hiyo, habari za kuacha shule kwangu zilipoenea, wanakijiji wote walianza kuzungumza juu yake, wakisema: “Huyu msichana ni mjinga sana! Kuondoka shuleni kutaharibu maisha yake ya baadaye!” na “Hakuna mtu atakayewaheshimu watu bila elimu. Atapata shida na umaskini maisha yake yote!” Kama mtu aliyekuwa amezoea kupokea sifa tangu utotoni, hisia ya kutia huzuni kwamba “Finiksi aliyeanguka ni duni kuliko kuku” kwa ghafla ilinijia. Niliogopa kwenda nje, nikiogopa kukutana na watu, nikiogopa hisia ya kuangaliwa kwa dharau. Ili kuepuka maumivu kama hayo, ni kwa nadra nilitoka nje ya nyumba yangu kwa miaka miwili mizima, na nilikuwa mnyamavu wakati wote. Wakati huo huo, hamu yangu ya kuwa mwanamke mwenye nguvu na mafanikio ilikua na nguvu hata zaidi, hivyo baada ya miaka miwili mingine, nikatoka kuanza kufanya kazi. Nilifanya kazi kwingi, lakini ningeacha muda mfupi baadaye kwa sababu nilihisi hiyo kazi ilikuwa inachosha na ya dhiki, au mshahara ulikuwa wa chini sana, au bwana hakuwa mzuri. Baada ya kushindwa mara kwa mara, nilivunjika moyo kabisa na kuhisi kwamba ndoto yangu ya kuwa mwanamke mwenye nguvu na mafanikio ilikuwa imeenda mbali sana na ukweli.

Katika mwaka wa 2005, nilikuwa na faida kubwa ya kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Tangu wakati huo, mtindo wa maisha yangu na hata maisha yangu yote yamebadilika kabisa. Niliona katika neno la Mungu: “Majaliwa ya mwanadamu yanadhibitiwa na mikono ya Mungu. Wewe huna uwezo wa kujidhibiti mwenyewe: Licha ya mwanadamu yeye mwenyewe daima kukimbilia na kujishughulisha, anabakia bila uwezo wa kujidhibiti. Kama ungejua matarajio yako mwenyewe, kama ungeweza kudhibiti majaliwa yako mwenyewe, ingekuwa wewe bado ni kiumbe?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu). Maneno ya nguvu ya Mungu yaliugusa sana moyo wangu, yakinifanya kuelewa kwamba jaala ya kila mtu iko mikononi Mwake na kabisa haidhibitiwi na watu wenyewe, na kwamba bila kujali ni wakati gani, watu hawawezi kuepuka ukuu na mipango ya Mungu, na wanapaswa kuwa watiifu chini ya mamlaka ya Mungu. Hii ndiyo njia ya pekee ya watu kuwa na jaala nzuri. Kupitia mwongozo wa maneno ya Mungu, nilitambua kwamba aina ya familia nilimozaliwa, jinsi nilivyostaarabika, kama maisha yangu ni maskini au tajiri—yote haya yameamuliwa na Mungu kabla. Sio jambo ambalo bongo langu au uwezo wangu unaweza kubadilisha. Nilikuwa nimefuatilia kuwa mwanamke wa nguvu kwa nafsi yote, nikiamini kuwa ningetegemea jitihada zangu mwenyewe kubadili majaliwa yangu. Lakini baada ya kupitia matatizo mengi, kuvumilia taabu nyingi, sikuwa nimepata nilichotaka mwishowe. Sasa nilifikiria kuhusu uchungu wote niliokuwa nimepitia; je, haukutokana kwa sababu ya kutojua ukuu wa Mungu na kukazana dhidi ya majaliwa kwa ukaidi? Sasa nilijua kwamba ni kwa kuja mbele ya Mungu na kukubali na kutii utaratibu na mipango Yake tu ndio ningeweza kuhepa uchungu huu wote polepole. Baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, sikukatishwa tamaa tena na uzoefu wangu, na sikujali tena juu ya walichokisema wengine. Badala yake, nikadhamiria kumwamini Mungu na kufuatilia ukweli vizuri, na kuishi maisha yenye maana. Baada ya hapo, nilisisitiza kusoma maneno ya Mungu kila siku, na kuomba, kuimba nyimbo, na kuhudhuria mikutano na ndugu wa kike na wa kiume. Kutokana na ufahamu wangu wa haraka wa ukweli na ukimbizaji wangu wa shauku, niliweza kuthaminiwa na dada aliyekuwa akininyunyizia, jambo lililonifanya kujihisi kupendezwa kote ndani. Baada ya kuingia kanisani, nilisikia viongozi wa kanisa wakisema ni lazima niwe lengo la ukuzaji wao, jambo lililonifanya nione ugumu zaidi kuizuia raha moyoni mwangu na hata likanipa hali ya furaha na kusisimka. Kwa hiyo nikajiambia: Ni lazima nifuatilie kwa moyo wangu wote na nafsi yangu! Siwezi kuwasikitisha viongozi wa kanisa. Hata kama ni kwa ajili ya sifa yangu nzuri, ni lazima nifanye kazi kwa bidii ili nipate kurejesha umaarufu na hadhi vilivyokuwa vimeniepuka katika ulimwengu wa nje. Wakati huo, sikujali kuhusu mapenzi ya Mungu hata kidogo. Jambo la pekee katika akili yangu lilikuwa umaarufu, ustawi, na hadhi mbele yangu tu, kama duara yenye kung’aa daima ikinipungia.

Muda mfupi baadaye, nilifanya kazi ya kuwanyunyizia waumini wapya kanisani. Ili kupata sifa kubwa kutoka kwa ndugu wa kike na wa kiume, na kutimiza kichwa cha maneno “lengo la ukuzaji,” niliamua kufanya kazi yangu kwa uwezo wangu wote. Nilidhani kwamba almradi ndugu wa kike na wa kiume walinikubali, basi Mungu pia angenipenda kikawaida. Kwa sababu ya “bidii na jitihada zangu,” hatimaye niliweza kutimiza nia yangu baada ya muda, nikipapata sifa na kutiwa moyo na ndugu wa kike na wa kiume. Sikuweza kujizuia kufikiri: Kwamba ndugu wengi wa kike na wa kiume wamenikubali ni lazima inamaanisha kuwa mimi ni bora kuwaliko watu wengine. Kama viongozi wa kanisa wanajua jambo hili, hakika watanikuza na kunitia katika nafasi muhimu. Kisha, mustakabali wangu kwa hakika utajazwa na uwezo usio na kikomo. Kwa sababu niliishi katika hali ya kuridhika na majisifu, nilianza kwa akili iliyojificha kutekeleza wajibu wangu kwa njia ya uzembe na nikasimamisha kuwanyunyizia waumini wapya kwa bidii. Kwa sababu hiyo, baadhi ya waumini wapya hawakuweza kupokea unyunyiziaji halisi na waliishi katika uhasi na udhaifu. Nilihisi kuwa na mshtuo sana kama nimekabiliwa na hali hii na kufikiri: Nimetoka mbali kupata “heshima” niliyo nayo leo. Ningewezaje kuwaruhusu waumini wapya kuendelea hivi? Viongozi wa kanisa wakijua, kwa hakika watasema kuwa sina uwezo na hata huenda wakasimamisha wajibu wangu pia. Si yote yatakuwa yameisha kwangu basi? Lazima nifanye kitu ili kugeuza hali hii. Katika siku zilizofuata, nilikwenda nje kila siku ili kuwafadhili waumini wapya. Wakati mwingine, kwa ajili ya mkutano mmoja, ningepanda milima kadhaa na kuchukua saa tatu hadi nne kutembea na kurudi, lakini sikuhisi hasira kabisa. Baada ya mwezi, nilikuwa nimechoka, lakini kwa sababu sikuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, mawasiliano yangu ya neno la Mungu yalikuwa ya kuchusha na yasiyosisimua, na kwa sababu hiyo hali ya waumini wapya haikufaulu kwa wakati ufaao. Nilihisi kuteseka sana juu ya hili kiasi kwamba nilikuwa na maumivu ya kichwa, lakini bado sikutambua kwamba ni lazima nije mbele ya Mungu kujitafakaria. Kutokana na kutofanikiwa kwa kazi yangu kwa muda mrefu, ambako kulisababisha madhara kwa maisha ya waumini wapya, hatimaye nilibadilishwa. Mara nilipofika nyumbani ilikuwa kama kuanguka kutoka angani hadi ardhini. Mwili wangu wote ulihisi kuwa teketeke na dhaifu. Nilifikiria nyuma jinsi ndugu wengi wa kike na wa kiume walivyoniheshimu katika siku za nyuma, lakini sasa nilikuwa nimeanguka kwa kiasi hicho. Je, ndugu wa kike na wa kiume wangeniangaliaje kama wangepata kujua? Jinsi niliyozidi kufikiria ndivyo niliyozidi kuhisi kutoweza kuwakabili ndugu wa kike na wa kiume, kwa hiyo nilikataa kwenda nje kwa mikutano na badala yake nilikaa nyumbani kila siku nikiwa na machozi. Nilikuwa na masumbuko makali ndani. Siku moja, niliona maneno yafuatayo ya Mungu: “Katika kutafuta kwenu, mna dhana, matumaini, na siku za baadaye nyingi sana za kibinafsi. Kazi ya sasa ni ili kushughulikia tamaa yenu ya hadhi na tamaa zenu badhirifu. Matumaini, hadhi, na dhana yote ni mifano bora kabisa ya tabia ya kishetani. … Kwa miaka mingi, mawazo ambayo watu wametegemea kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao yamekuwa yakiharibu mioyo yao hadi kiwango ambapo wamekuwa wadanganyifu, waoga, na wenye kustahili dharau. Hawakosi tu ushupavu na uamuzi, lakini pia wamekuwa walafi, wenye kiburi, na wa kudhamiria. Kabisa wanakosa uamuzi wowote upitao sana ubinafsi, na hata zaidi, hawana ujasiri hata kidogo wa kuondoa shutuma za ushawishi huu wa giza. Fikira na maisha ya watu ni mabovu sana kiasi kwamba mitazamo yao juu ya kuamini katika Mungu bado ni miovu kwa namna isiyovumilika, na hata watu wanaponena kuhusu mitazamo yao juu ya imani katika Mungu haivumiliki kabisa kusikia. Watu wote ni waoga, wasiojimudu, wenye kustahili dharau, na dhaifu. Hawahisi maudhi kwa nguvu za giza, na hawahisi upendo kwa nuru na ukweli; badala yake, wanafanya kila wanaloweza kuvifukuza(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?). Ilikuwa ni kwa njia ya ufunuo mkali wa maneno ya Mungu tu nilipogundua kuwa mtazamo wangu juu ya imani katika Mungu ulikuwa si sahihi tangu mwanzo. Nilitaka kutumia imani yangu kwa Mungu ili kufanikisha umaarufu, ustawi, na hadhi nilizoshindwa kupata duniani, na nikafikiria kipumbavu: Ningechaguliwa na kuwekwa katika nafasi muhimu alimradi nimepata sifa ya ndugu wa kike na wa kiume, na kisha Mungu angenipenda pia na kunisifu. Chini ya mamlaka ya mawazo haya, nilikuwa dhaifu na wa kustahili dharau. Wakati ndugu wa kike na wa kiume walinisifu, ningejaa ujasiri, lakini mara nilipopoteza vitu hivi, mara moja nikawa mwenye kukata tamaa na kufadhaika, hasi na wa kurudi nyuma. Huku kulikuwaje kumwamini Mungu? Yote niliyoamini ilikuwa sifa, ustawi, na hadhi! Nia ya Mungu haikuwa kunifundisha kuwa mfanyakazi mwenye kipaji cha ajabu, na aidha haikuwa kuniruhusu nitumie kutimiza wajibu wangu kwa manufaa yangu kuziridhisha tamaa za kibinafsi. Badala yake, Alitumaini, kwa njia ya kutimiza wajibu wangu, ningetambua dosari zangu na kupata uzoefu wa maneno na kazi ya Mungu, na hivyo kuelewa na kupata ukweli zaidi, na hatimaye kupokea wokovu wa Mungu. Wakati huo huo, pia ilikuwa ili niweze kutumia uzoefu wangu mwenyewe na kuuelewa ukweli ili kuwapa ndugu wa kike na kiume ambao walikuwa waumini wapya katika Mungu, na kuwasaidia kuweka msingi katika njia ya ukweli ili waweze kuingia njia sahihi ya kumwamini Mungu haraka iwezekanavyo. Hata hivyo, sikutafuta nia za Mungu kwa kuwa daima nilikuwa nimejitahidi kwa ajili ya umaarufu na hadhi, na kwa nia zangu binafsi. Hatimaye, sikupokea kazi ya Roho Mtakatifu kabisa, hivyo bila kujali nilijitahidi kiasi gani, sikuweza kuwanyunyizia waamini wapya vizuri. Baada ya kusimamishwa kutimiza wajibu wangu, nikawa hasi kupita kiasi na kuzielewa visivyo nia za Mungu, nikidhani kwamba sikuwa na tumaini la kupokea wokovu wa Mungu. Ilikuwa ni wakati huu ambapo kwa ghafla nilikumbuka maneno ya Mungu: “Sijali jinsi kazi yako ya bidii ni ya kusifiwa, jinsi sifa zako ni za kuvutia, jinsi unavyonifuata Mimi kwa karibu, jinsi ulivyo mashuhuri, au jinsi umeendeleza mwelekeo wako; mradi hujafanya kile ambacho Nimedai, hutaweza kupata sifa Zangu kamwe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu). “Iwapo mtu anatafuta kwa dhati hakuamuliwi na jinsi wengine wanamhukumu ama jinsi wengine karibu wanamwona, lakini kunaamuliwa na iwapo Roho Mtakatifu anamfanyia kazi na iwapo ana uwepo wa Roho Mtakatifu, na kunaamuliwa zaidi na iwapo tabia yake inabadilika na iwapo ana maarifa ya Mungu baada ya kupitia kazi ya Roho Mtakatifu kwa muda fulani …(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja). Katika maneno ya Mungu nilielewa nia na matakwa Yake. Ilibainika kuwa imani yangu ya awali kuwa hadhi ya juu zaidi ilimaanisha mustakabali wa mafanikio na sifa zaidi kutoka kwa Mungu zilikuwa ni kupimia kazi ya Mungu kutoka kwa mtazamo wa kidunia, jambo ambalo lilikuwa lenye makosa zaidi. Jinsi Mungu hupima na kuamua mwisho wa mtu sio kwa kuzingatia hadhi yake, ukubwa, au kiasi cha kazi aliyofanya, lakini ni kama alipata ukweli na kama alifanikisha mabadiliko ya tabia. Kama mtu hajapata ukweli au kufanikisha mabadiliko ya tabia kupitia kazi ya Mungu, basi jinsi hadhi yake ilivyo juu au ni watu wengi wangapi wanaomwidhinisha yote huwa bure. Hatakosa tu kupokea idhini ya Mungu, pia atachukiwa, kukataliwa, na kuhukumiwa na Mungu. Ni kwa kuzingatia tu kujijua mwenyewe na Mungu anapotekeleza wajibu wake, na kutumia uzoefu wake halisi kuwanyunyizia na kuwafadhili ndugu wa kike na wa kiume, atakapoweza kutatua matatizo halisi, kutafuta njia ya kuwaongoza ndugu wa kike na wa kiume, na kuifanya kazi yao iwe ya kufaa. Mtu kama mimi, ambaye hakufuatilia kuingia kwake mwenyewe na mabadiliko kamwe alipokuwa akifanya kazi, lakini badala yake kwa upofu alifuatilia sifa, ustawi, na hadhi, hatimaye akisababisha tu madhara kwa ndugu wa kike na wa kiume zaidi na zaidi, na mwishowe yeye binafsi angeondoshwa. Nilipofikiria hili, nilielewa kuwa kuachishwa wajibu wangu na kanisa kulikuwa ni mazingira yaliyowekwa na Mungu yakizienga nia na tamaa zangu potovu, na pia asili yangu potovu, ili nipate kujitafakaria na kujijua, kubadilisha maoni yangu yasiyo sahihi juu ya ukimbizaji, na kufuata njia sahihi ya kufuatilia ukweli haraka iwezekanavyo. Wakati huo, nilihisi upendo wa Mungu, utunzaji, na fikira, na sikuweza kujizuia kumwomba Mungu: “Ee Mungu! Asante kwa kutoa upendo Wako mkubwa kwangu. Sikuwa nikizielewa nia zako na kufikiri kuwa milki ya umaarufu, ustawi, na hadhi hazingenihakikishia kuthaminiwa na Wewe. Hili lilinifanya kutojali kabisa kuhusu kuingia katika ukweli wakati wa kazi yangu. Yote niliyofanya ni kufuatilia umaarufu na ustawi, jambo ambalo ni kinyume kabisa na matakwa Yako. Kwa nuru ya neno Lako, sasa ninaelewa matakwa Yako. Sitatenda tena kwa uasi wa moja kwa moja na kazi Yako kama nilivyofanya wakati wa nyuma. Nitafuatilia mabadiliko ya tabia na kufuata njia sahihi ya kufuatilia ukweli.”

Muda mfupi baadaye, kanisa tena lilinipangia kuwanyunyizia waumini wapya, na pia lilinitaka niishi na dada mmoja mdogo. Dada huyo mdogo alikuwa na nafsi ya wazi na yenye shauku, kwa hiyo nilifikiria: Kwa kuwa mimi ni mndani na sipendi kuzungumza sana, ilhali dada mdogo ni msondani na husema bila kusita, tunaweza kutumia fursa hii kujifunza kutoka kwa umahiri wa sisi kwa sisi ili kufidia udhaifu wetu. Ingawa nilifikiria jinsi hii, bado kulikuwa na migogoro na kutoelewana katika uingiliano wetu halisi. Ili kubadilisha hali hii, nilianza kuzungumza na kutenda kwa makini zaidi, nikiogopa kuwa kungeweza kuwa na matukio yasiyopendeza zaidi. Dada huyo mdogo mara nyingi alienda kufanya kazi. Kumwona akiwa mwenye mashughuli wakati wote, niliamua kutekeleza kazi zote za nyumbani ili kumuacha na picha nzuri na kusaidia kudumisha uhusiano wetu. Sikuwahi kutarajia kamwe kuwa miezi michache baadaye, uhusiano wetu kwa kweli uligeuka kuwa wa kulazimishwa zaidi, ambao niliuona hasa ukiwa wa kufadhaisha na mchungu. Hata hivyo, sikujipima na kuutambua upotovu wangu na badala yake nililenga uangalifu wangu kwa huyo dada mdogo, nikifikiri kwamba alikuwa mgumu kuelewana naye na pia asiyekuwa na busara mno. Siku moja, huyu dada aliporudi kutoka kazini na akaniona nikifanya kazi za nyumbani, alisema waziwazi kwamba nilikuwa nikifanya hivyo tu kwa sababu ya kuwa na raghba. Baada ya kusikia hili, sikuweza tena kuyazuia machozi yangu ya malalamiko kutiririka. Wakati huo, kwa kweli nilitaka kuondoka mara moja na kutorudi kamwe. Lakini hata hivyo nikafikiria jinsi dada huyo alivyokuwa mdogo kuniliko, na kwamba hakuwa amemwamini Mungu kwa muda mrefu. Kama sikuweza kujiweka kando, na kuendelea kushikilia chuki dhidi yake, basi viongozi wa kanisa na ndugu wengine wa kike na wa kiume wangenionaje? Wangesema kuwa sikuwa na upendo kwa huyu dada mdogo na kwamba sikuwajibika. Ningewezaje kuwakabili basi? Kama nimekabiliwa na hali hiyo, sikujua la kufanya. Kwa maumivu, nilikuja mbele ya Mungu kuomba: “Ee Mungu! Mimi nina maumivu mengi sana. Ni kama kuna majabali mazito yakinigandamizia chini, yakinifanya isiwezekane mimi kuwa na nguvu ya kutoroka. Lakini naamini nia zako njema lazima zipo katika hali hii ambayo imenifika. Ninakuomba tu kuwa Unipe nuru ili niweze kuelewa nia Zako na kujifunza fundisho ambalo napaswa kujifunza.” Mara baada ya maombi, dada mmoja alitukia tu kuja kunitafuta, hivyo nikaufungua moyo wangu na kumwambia kuhusu hali yangu. Baada ya kulisikiliza, huyo dada akasema: “Kazi yote ya Mungu ni kwa ajili ya kuwaokoa wanadamu, na hali zote zinazotufika sote zimekusudiwa kutufunza mafunzo. Ikiwa tuna mambo haya hasi ndani yetu, inamaanisha bado tuna sumu za shetani ndani yetu ambazo zinadharauliwa na Mungu. Mungu atatutakasa na kutubadilisha kupitia hali hizi….” Baada ya huyo dada kuondoka, niligaagaa na kugeukageuka kitandani na sikuweza kulala, nikifikiri: Mungu hutakasa na kubadilisha nini ndani yangu? Kwa hiyo, niliamka na kusoma neno la Mungu: “… unaweza kumaizi asili ya mtu na yeye yu wa nani kutoka kwa maoni yake ya maisha na maadili. Shetani huwapotosha watu kwa kupitia masomo na ushawishi wa serikali za kitaifa na walio mashuhuri na wakuu. Upuuzi wao umekuwa uzima wa mwanadamu na asili. ‘Kila mtu kivyake na ibilisi achukue ya nyuma kabisa’ ni msemo wa kishetani unaojulikana sana ambao umeingizwa ndani ya kila mtu na umekuwa maisha ya watu. Kuna maneno mengine ya falsafa ya kuishi ambayo pia ni kama haya. … Bado kuna sumu nyingi za kishetani maishani mwa watu, katika mienendo yao na shughuli zao na wengine; hawana ukweli wowote hata kidogo. Kwa mfano, falsafa zao za kuishi, njia zao za kufanya vitu, na kanuni zao zote zimejazwa sumu za joka kuu jekundu, na zote zinatoka kwa Shetani. Hivyo, vitu vyote vinavyopita katika mifupa na damu ya watu ni vitu vyote vya Shetani(“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nilipokuwa nikiyatafakari maneno ya Mungu, nilitumbukia katika mawazo: Kwa miezi michache iliyopita, kwa nini nimeishi katika mafadhaiko na maumivu? Ni sumu gani za Shetani zinazoitawala tabia yangu? Chini ya nuru ya Mungu, nilihisi moyo wangu hatua kwa hatua ukichangamka ndani, na kunifanya nitambue kwamba sababu niliyokuwa nikizingatia sana umaarufu na hadhi ilikuwa ni ushawishi na mkanganyo wa sumu za Shetani kama vile “Mtu huliacha jina lake nyuma popote akaapo, kama tu vile bata bukini hutetea popote anapopuruka,” “Kama mti unavyoishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” na “Wanaume wanapaswa kujitahidi kuwa bora kuliko watu wa hirimu yao.” Ulikuwa ni utawala wa sumu hizi ambao ulinifanya nijali sana kuhusu heshima na majivuno, na pia kile ambacho wengine walifikiria kunihusu. Kila kitu nilichokifanya na kukisema kilikuwa ni ili kudumisha picha na hadhi yangu katika mioyo ya watu wengine. Mara tu kitu fulani kilipoathiri heshima yangu au majivuno, ningekuwa na maumivu na mateso. Mateso haya yote na uchungu vilikuwa ni kwa sababu ya Shetani. Nilikumbuka kuwa tangu kuhamia kwa dada huyo mdogo, nilikuwa nimeelewana naye kwa uangalifu ili kuacha picha nzuri, nikiogopa kwamba ningeacha picha mbaya kama ningesema au kutenda kitu kibaya. Kwa hiyo nilikuwa nikiishi kwa kujipendekeza na kutenda kama mpumbavu. Wakati dada huyo mdogo aliponishughulikia, sikutumia fursa hiyo kujijua, lakini nilikuwa na maoni na chuki bila sababu dhidi ya huyo dada kwa sababu sikutaka kuona aibu, na hata nilitaka kuepuka mazingira haya. Ili kutunza picha yangu na kuepuka aibu, sikuthubutu kujidhihirisha kwa huyo dada mdogo hata wakati mwingine nilipomwona akiufichua upotovu kidogo kidogo au kufanya jambo lisilolingana na ukweli, nikiogopa kwamba huenda nikamkosea na kusababisha uhusiano wetu utenganike zaidi na zaidi. ... Sumu hizi za Shetani, hata hivyo, zilinifanya kuwa mnafiki na mwenye hila zaidi na zaidi, jambo lililoyafanya maisha yangu yawe ya kuchosha sana na machungu. Kwa kweli nilitamani niweze kupenya ngome hii ya giza na kuubambua uso wangu bandia, ili niweze kuishi kwa uhuru kamili na faraja. Lakini sikuweza kulifanya peke yangu, hivyo nilipiga magoti mbele ya Mungu na kutoa hisia zangu za siri Kwake: “Ee Mungu! Nilikuwa nikichukulia sifa na umaarufu kama aina ya raha. Sasa ninaona kwamba nilikuwa mwenye makosa. Ukimbizaji wa mambo haya si furaha ya ajabu lakini maumivu, mafadhaiko, utumwa, na vikwazo. Sasa naona wazi kwamba ni falsafa za Shetani ambazo zilinidanganya na kunidhibiti, zikinifanya kufuatilia umaarufu, ustawi, na hadhi, na pia heshima na majivuno. Maumivu yangu yote yameletwa na Shetani. Mungu wangu! Kwa kweli sitaki kuishi na falsafa za Shetani tena. Naomba wokovu Wako; nionyeshe njia sahihi ya matendo, na unipe ujasiri na uwezo wa kupenya mtego wa Shetani na kutenda kulingana na matakwa Yako.” Baada ya sala, nilihisi faraja isiyo na kifani. Wakati huo huo, nilitambua kwamba ningeweza kutatua tu tabia yangu mbaya kupitia ukimbizaji wa ukweli. Baadaye, niliona kifungu kifuatacho cha neno la Mungu: “Iwapo huzingatii uhusiano wako na watu lakini unadumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, ikiwa uko tayari kumpa Mungu moyo wako na ujifunze kumtii, basi kwa kawaida sana, uhusiano wako na watu wote utakuwa wa kawaida. Kwa njia hii, uhusiano huu haujengwi kwa mwili, bali juu ya msingi wa upendo wa Mungu. Kwa kiasi kikubwa hakuna ushirikiano uliojengwa juu ya mwili, lakini katika roho kuna ushirikiano na vilevile upendo, starehe, na kutoleana kwa wenza. Haya yote yanafanywa kwa msingi wa moyo unaomridhisha Mungu. Uhusiano huu haudumishwi kwa kutegemea falsafa ya mwanadamu ya maisha, bali unaundwa kwa kawaida kupitia mzigo wa Mungu. Hauhitaji jitihada zilizofanywa na binadamu. Unahitaji tu kutenda kulingana na maadili ya neno la Mungu. Je, unayo hiari ya kuwa mwenye kufikiria mapenzi ya Mungu? … Je, uko tayari kuutoa moyo wako kwa Mungu kabisa, na kutofikiri kuhusu msimamo wako kati ya watu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu). Maneno ya Mungu yalionyesha njia ya wazi ya matendo kwangu, na hiyo ilikuwa ni kufanya mazoezi ya kuwa mtu mwaminifu na kutojali tena juu ya umaarufu na ustawi au kudumisha picha na hadhi yangu katika mioyo ya watu. Badala yake, napaswa kumpa Mungu moyo wangu, kuyatukuza na kuyashuhudia maneno ya Mungu katika kila kitu, kutenda ukweli, na kumtii Mungu. Kwa njia hiyo, nitaweza kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu. Kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu pia kwa kawaida husababisha uhusiano wa kawaida na watu wengine. Kwa hiyo, niliamua kwa faragha kutenda kulingana na maneno ya Mungu na hatua kwa hatua kuondoa hadhi yangu potovu. Tangu wakati huo, mara kwa mara niliwasiliana kwa utambuzi na dada yule mdogo na kusoma maneno ya Mungu pamoja naye. Iwapo tulikabiliwa na matatizo katika utendaji wa majukumu yetu ambayo hatukuweza kuyatatua, tungemwomba Mungu pamoja na kutafuta majibu katika maneno ya Mungu. Tulielewana vizuri sana. Kabla sijalijua, mzigo uliokuwa kwa mwili wangu na mafadhaiko moyoni mwangu yote yalivukiza, na tabasamu iliyosubiriwa kwa muda mrefu ilijitokeza kwa uso wangu. Kwa kweli nilikuwa nimepitia faraja na furaha iliyoletwa na kutenda maneno ya Mungu. Kwa kweli ninamshukuru Mungu kwa kuniokoa.

Baada ya miezi hii michache ya usafishwaji mchungu, hatimaye nilielewa ni kwa nini Mungu hangetuacha tutumie falsafa za maisha kudumisha uhusiano na watu wengine. Ni kwa sababu falsafa hizo zote za maisha na kile kinachodaiwa kuwa misemo ni sumu ambazo Shetani hutia ndani ya watu, na ni zana zinazotumiwa na Shetani kuwafunga na kuwadhuru watu. Filosofia hizi za shetani zinaweza tu kuwafanya watu kufanyiza mgawanyiko, migogoro, na kifo, na zinaweza tu kuwaletea watu mafadhaiko na maumivu. Hili ni kwa sababu Shetani mwenyewe ni upotovu na mgawanyiko, na ni maneno ya Mungu pekee na yale Anayohitaji kutoka kwa watu yanayowawezesha kufanya amani na kila mmoja. Ni kwa kuishi tu katika maneno ya Mungu na kutenda kwa mujibu wa maneno Yake watu wanapoweza kupenya kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani na kuishi na uhuru kamili na faraja mbele ya Mungu. Wakati huo huo, niliona pia kwamba kuishi kwangu na dada huyu mdogo kulikuwa ni mpango mzuri wa Mungu, ulioanzishwa ili kulenga sumu yenye mizizi imara ya Shetani ndani yangu na mahitaji yangu ya utendaji. Kama Mungu hakuwa amefanya kazi kwa njia hii, singekuwa nimetambua kamwe kiwango cha madhara ya sumu za shetani kama vile “Mtu huliacha jina lake nyuma popote akaapo, kama tu vile bata bukini hutetea popote anapopuruka” na “Kama mti unavyoishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake” zilizokuwa zimenitendea. Bado ningekuwa nimeziabudu sumu hizi kama vitu vyema, jambo ambalo lingekuwa limenifanya kuwa na kiburi zaidi na zaidi na kupotoshwa, na hatimaye kuelekezwa kwa ushushwaji cheo na maangamizi. Hali hizi na majaribu kwa usahihi vilikuwa ni wokovu mkubwa wa Mungu kwangu!

Baadaye, nilichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa. Nilipokabiliwa na masuala mwanzoni, mara nyingi ningeyasikiliza mapendekezo kutoka kwa ndugu wa kike na wa kiume, na sikujali kuhusu jinsi wengine wangenifikiria. Lakini haikuchukua muda mrefu kwa hamu yangu ya kufuatilia umaarufu na ustawi kuanza kupanuka tena. Kwa kuwa nilianza kutekeleza wajibu huu mapema zaidi kumliko yule kiongozi mwingine katika kanisa, ndugu wa kike na wa kiume kwa kawaida wangekuja kwangu zaidi wakati kulipokuwa na hoja. Hatua kwa hatua, nilianza kujisahau na kudhani kwamba bado nilikuwa mkubwa kwa cheo kumliko huyo dada. Tukiwa kwa mikutano na huyo dada, daima ningezungumza juu ya mafundisho fulani yaliyoonekana muhimu ili kujionyesha na kupata utambuzi na upendezwaji kutoka kwa ndugu wa kike na wa kiume, na pia kuwafanya wahisi kuwa mimi ni bora kumliko. Siku moja, wakati wa mkutano wa kikundi kimoja kidogo, wazo fulani lilinijia kwa mawazo yangu huyu dada alipokuwa tu amewasiliana kwa muda mfupi: Ni lazima niwasiliane zaidi, ama sivyo ndugu wa kike na wa kiume watafikiria kuwa mimi si hodari kama yeye. Kwa hiyo, nilijiingiza wakati kulipokuwa na mapumziko na kuanza kuwasiliana bila kusimama. Nilipokuwa tu nikiliingilia, ndugu mmoja wa kiume kando yangu alinikatiza: “Hatuwezi tu kuzungumza tu juu ya mafundisho matupu. Tunapaswa kuwasiliana uzoefu na maarifa ya vitendo ili kuwaruzuku ndugu wa kike na wa kiume.” Baada ya kuyasikiliza maneno ya huyu ndugu, nilihisi kana kwamba nimepigwa kofi hadharani. Uso wangu ukiwa umesisimka, nilifikiria: Mwanzoni nilikusudia kusema maneno machache ya ziada ili ndugu wa kike na wa kiume watanipandisha daraja, lakini sasa limekuwa la kunitahayarisha sana! Wakati huo, nilitaka kupata shimo chini ya sakafu kujifichia. Nilipokuwa tu nikihisi kuteseka ndani, huyo ndugu alisoma kifungu cha neno la Mungu: “… watu wengine hususan humpenda Paulo sana. Wanapenda kwenda na kuhutubu na kufanya kazi, wanapenda kukutana pamoja na kuzungumza; wanapenda watu kuwasikiza, kuwaabudu, na kuwazingira. Wanapenda kuwa na hadhi katika mawazo ya wengine, na wanafurahia wakati wengine wanathamini mifano yao. … Kama kweli wanatenda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa wao ni fidhuli na wenye majivuno. Hawamwabudu Mungu hata kidogo; wanatafuta hadhi ya juu zaidi, na wangependa kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwamiliki, na kuwa na hadhi akilini mwao. Huu ni mfano bora wa Shetani. Vipengele vya asili yao vinavyojitokeza ni ufidhuli na majivuno, kutokuwa radhi kumwabudu Mungu, na tamaa ya kuabudiwa na wengine. Tabia kama hizi zinaweza kupa mtazamo dhahiri sana juu ya asili yao(“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kila neno la hukumu ya Mungu lilikuwa kama sindano ikichoma ndani ya moyo wangu, ikinifanya nihisi aibu hata zaidi. Nilikumbuka kuwa kabla ya kumwamini Mungu, nilifurahia hasa kupendwa na kila mtu, na nilijitahidi kwa moyo wangu na nafsi yangu kujitokeza na kuwa mwanamke mwenye nguvu na mwenye mafanikio. Baada ya ndoto hii kuvunjwa, nilifikiri ningetimiza ndoto yangu ya umaarufu, ustawi, na hadhi katika kanisa. Hasa katika kipindi hiki, nilishindana kwa siri na huyo dada ili kuwafanya ndugu wa kike na wa kiume waniheshimu. Juujuu, nilikuwa nikishindania hadhi dhidi ya mtu mmoja, lakini kwa kiini, nilikuwa nikishindania watu wateule wa Mungu dhidi ya Mungu. Hili ni kwa sababu wale wanaomwamini Mungu wanapaswa kumheshimu sana Mungu, wamwabudu Yeye, na kumpa Mungu mahali katika mioyo yao. Badala yake, nilitaka kuwa na nafasi ndani ya mioyo ya ndugu wa kike na wa kiume, na kuwataka waniheshimu sana na kuniabudu. Si huo ni upinzani dhahiri kwa Mungu? Ni kabla ya ukweli tu nilipoweza kuona kwamba asili yangu ni kinyume cha Mungu. Ikiwa sipitii adabu ya Mungu na hukumu na sifanikishi mabadiliko yoyote katika tabia yangu, basi hata kama mimi naonekana kwa shauku nikitumia kwa utendaji kwa ajili ya Mungu kwa nje, kwa kweli ninafanya maovu na kumpinga Mungu. Wakati huo huo, niliona wazi kwamba Shetani huwapotosha wanadamu kwa kuingiza sumu katika akili zao na roho kwa njia mbalimbali, akiwafanya kushindania umaarufu, ustawi, na hadhi, na kwa njia hii huwasababisha kupotea hatua kwa hatua kutoka kwa Mungu, kumsaliti Mungu, na hatimaye kujikokota hadi kuzimu. Nikifikiria hili, sikuweza kujizuia kuwa na hofu, na pia nilianza kuudharau upofu wangu na upumbavu, upotovu wangu wa kina, na sumu za shetani ambazo zilikuwa zimekita mizizi ndani yangu. Kama singekuwa chini ya utawala wa umaarufu, ustawi, na hadhi, singekuwa chini ya udhibiti wa mtu yeyote, tukio, au kitu, na ningekuwa tu natafuta kumridhisha Mungu kwa kutimiza wajibu wangu kama kiumbe aliyeumbwa. Kama singekuwa nimedhibitiwa na umaarufu, ustawi, na hadhi, ningekuwa, kwa kutimiza wajibu wangu, nimelenga kumtukuza Mungu, kumshuhudia Mungu, na kuwaleta ndugu wa kike na wa kiume mbele Yake. Kama singekuwa nimedhibitiwa na umaarufu, ustawi, na hadhi, singekuwa nimeishi katika mafadhaiko na mateso kila siku, bila kuweza kufurahia faraja na furaha zinazoletwa na ukweli. Kama singekuwa nimedhibitiwa na umaarufu, ustawi, na hadhi, ningekuwa nimeanzisha uhusiano wa kawaida na ndugu wa kike na wa kiume na kufadhiliana na kusaidiana kwa roho, badala ya kutumia sura ya kinafiki kuwadanganya wengine kwa uaminifu wao na upendezwaji. … Haya yote yalikuwa ni kwa sababu ya sumu za Shetani, ambazo zilikuwa zimenidhuru hadi siku iyo hiyo. Shetani kwa kweli ni wa kustahili dharau mno na ni muovu mno. Ni pepo mla roho kabisa! Chini ya nuru na mwongozo wa Mungu, nilikuza ridhaa na ujasiri wa kuunyima mwili wangu na kutenda ukweli. Kwa hiyo nilimwomba Mungu: “Ewe Mungu! Ni madhara ya umaarufu, ustawi, na hadhi ambavyo vimeniweka katika hali ya leo. Kufuatilia mambo haya, niliacha matakwa Yako nyuma, nikikukaidi na kukupinga Wewe tena na tena nikikufanya uwe na huzuni na maudhi. Sasa ninachukia mambo haya kwa dhati. Nitayatelekeza na kuyaacha kabisa. Tafadhali Uniongoze katika njia yangu ya baadaye.” Tangu wakati huo, nimeepuka kujulikana sana, na wakati wa mikutano ningeanza kuzingatia kuzungumza kuhusu uzoefu wangu halisi. Wakati ndugu wa kike na wa kiume walipokuwa na shida, ningewafungulia moyo wangu kwa utambuzi ili kuwasiliana nao kuhusu nyakati ambazo kwa kweli nilipitia matatizo mwenyewe na kupata nuru na mwongozo wa maneno ya Mungu, ili waweze kuelewa nia za Mungu na kuutambua upendo wa Mungu. Nilipotenda kwa njia hii, nilihisi utulivu zaidi na nuru ndani ya moyo wangu, nikiifanya kila siku kuwa ya kufurahisha hasa.

Baada ya kupitia hukumu ya Mungu na kuadibiwa na kushughulikiwa na kupogolewa na Yeye mara kwa mara, nilianza kuwa na maarifa kiasi halisi ya asili yangu ya shetani. Wakati wowote nilipokabiliwa na mambo kama vile umaarufu, ustawi, hadhi, na kukabiliwa nayo tena, ningemwomba Mungu kwa makusudi na kushirikiana na Yeye, na kuunyima mwili wangu na kutenda ukweli. Wakati mmoja, dada fulani katika kanisa jirani hakuwa katika hali nzuri. Baada ya kusikia kuhusu hili, mara nyingi tulikwenda kuwasiliana naye na tukawa na mazungumzo ya ndani. Baada ya muda, hali yake ikawa nzuri zaidi na akaanza kushirikiana kikamilifu na kazi ya injili. Miongoni mwa waumini wapya aliowaingiza, kuna mmoja ambaye kwa kweli alikuwa na njaa ya ukweli na pia alipiga hatua haraka sana. Kwa hiyo, tulinuia kumkuza kama kiongozi wa kanisa kwa waumini wapya. Wakati huu, kanisa jirani lilituandikia barua, likiomba kwamba huyo dada aende huko kutimiza wajibu wake. Nilikuwa sitaki kabisa kwa ndani, lakini hata hivyo nilibadili mawazo: Makanisa ni unganisho mzima. Kile Mungu hutaka ni maonyesho ya shirika. Bila kujali ni kanisa gani muumini mpya huhudhuria, mradi anaweza kutimiza wajibu wake, kitakuwa ni kitu kinachoufariji moyo wa Mungu. Si fikira zangu ya awali zilikuwa kwa ajili ya umaarufu, ustawi, na hadhi? Si nilikuwa bado nimezingatia picha yangu binafsi na uso wangu? Hili lilinikumbusha maneno ya Mungu: “Wanadamu dhalimu! Kuwafumba watu macho na kula njama, kupokonyana na kunyang’anya mmoja kutoka kwa mwingine, kung’ang’ania umaarufu na mali, kuuana—haya yote yataisha lini? Licha ya mamia ya maelfu ya maneno ambayo Mungu amezungumza, hakuna hata mmoja ambaye ameacha kufanya upumbavu. Watu hutenda kwa ajili ya familia zao, watoto wao, kazi zao, matarajio yao ya baadaye, cheo, majivuno, na pesa, kwa sababu ya chakula, mavazi, na mwili. Lakini kuna yeyote ambaye matendo yake kwa kweli ni kwa ajili ya Mungu? Hata miongoni mwa wale ambao wanatenda kwa ajili ya Mungu, kunao wachache tu wanaomfahamu Mungu. Ni watu wangapi ambao hawatendi kwa ajili ya maslahi yao? Ni wangapi wasiowakandamiza na kuwatenga wengine ili kulinda vyeo vyao wenyewe?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Waovu Hakika Wataadhibiwa). Sawa! Angalia mwenendo wangu na tabia. Daima nilikuwa nikifuata umaarufu na ustawi, bila lolote kati ya hayo kuwa la Mungu. Nilikuwa na ubinafsi jinsi gani! Nilifurahia kuinuliwa na Mungu na wema wa Mungu, lakini nilijaribu kwa bidii na kupiga ubongo kila siku ili kupata umaarufu, ustawi, na hadhi. Ingawa nilimwamini Mungu kwa jina, sikutenda kulingana na madhumuni ya Mungu na matakwa, na kimsingi sikumtii Mungu kabisa. Kiwango cha Mungu cha kama mtu humwamini Mungu kwa kweli hakitegemezwi tabia yake ya nje au tathmini ya wengine, lakini ni juu ya kama anaweza kuyakandamiza mambo yaliyo ndani ya moyo wake ambayo hayalingani na malengo ya Mungu wakati mambo yanapomfika, kama anaweza kufikiria kwa maslahi bora mno ya kanisa, na kama anaweza kumridhisha na kumpenda Mungu katika kila kitu. Baada ya kuelewa nia za Mungu, moyo wangu kwa ghafla ulichangamka, na mara moja nikamhamisha muumini huyu mpya kwa kanisa jirani.

Baada ya kupitia kazi ya Mungu kwa miaka kadhaa, nilielewa kwa dhahiri zaidi: Umaarufu, ustawi, na hadhi ni mbinu zinazotumiwa na Shetani kuwadanganya watu na minyororo inayotumiwa kuwafunga watu. Watu wanaoishi chini ya utawala wake wanaweza tu kufungwa na kudanganywa naye, bila uhuru wowote kabisa. Kwa upande mwingine, neno la Mungu ndilo ukweli, njia, na uzima. Watu wanaoishi chini ya neno la Mungu wanaishi katika mwanga na baraka za Mungu. Mtu ataweza kupitia faraja na uhuru wa kuishi mbele ya Mungu mradi atajitahidi kiasi kutimiza matakwa ya Mungu na kutenda ukweli kama Mungu anavyotaka. Nikiangalia nyuma kwa maumivu na mateso ambayo umaarufu, ustawi, na hadhi yameniletea, kisha kwa kazi ya wokovu ambayo Mungu amenifanyia, kwa kweli ninahisi shukurani na deni kwa Mungu. Ili kuniokoa kutoka kwa utumwa wa umaarufu, ustawi, na hadhi, Mungu kwa uangalifu alipanga mazingira mbalimbali, watu, mambo, na matukio, na alinielekeza na kuniongoza hatua kwa hatua akitumia kazi Yake ya vitendo, akaniruhusu niitembee njia sahihi ya maisha. Kila mazingira na kila dhihirisho vyote vilipangwa kwa uangalifu na Mungu, na nyuma ya kila kimoja kuna mapenzi makubwa ya Mungu kwangu. Baada ya kupitia kuadibu na hukumu tena na tena, baadaye hatua kwa hatua niliona uhalisi wa upotovu wangu. Pia nilipata maarifa ya kazi ya Mungu ya vitendo, nikaona utakatifu wa Mungu, ukuu, na kukosa ubinafsi, na nikahisi sana fikira na utunzaji wa Mungu katika kuwaokoa wanadamu. Katika uzoefu wangu wa baadaye, nitakuwa tayari zaidi kukubali kuadibiwa na hukumu ya Mungu, majaribu na usafishwaji Wake, ili upotovu wangu uweze kutakaswa kabisa na kubadilishwa haraka iwezekanavyo, na hivyo nitaweza kwa uhalisi kuishi maisha yenye maana na ya thamani!

Iliyotangulia: Hukumu ni Mwanga

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Masumbuko Makali ya Milele

“Roho zote ambazo zimepotoshwa na Shetani ziko chini ya udhibiti wa miliki ya Shetani. Ni wale tu wanaomwamini Kristo ndio waliotengwa...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp