Kipindi 04, Ukweli Kuhusu Mateso ya Kikatili ya CCP Dhidi ya Wakristo: Mnamo 2020, CCP Ilianzisha "Vita vya Jumla" vya Miaka Mitatu kwa Lengo la Kuliangamiza Kabisa Kanisa la Mwenyezi Mungu

29/01/2026

Kwa miaka mingi, CCP kimelikandamiza na kulitesa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Ili kuliangamiza na kulimaliza kabisa Kanisa, mnamo Septemba 2020, CCP kiliitisha kongamano la siri ili kuzindua "Vita vya Jumla" vya miaka mitatu vya kitaifa dhidi ya Kanisa, kikifanya ukandamizaji na mateso dhidi ya Kanisa kuwa kipaumbele cha juu katika uchukuliaji wake hatua kali imani za kidini. Wakristo wa Kanisa, hasa viongozi wa ngazi zote na washiriki wakuu, walilengwa kama shabaha kuu za kukamatwa. Wakati wa "Vita vya Jumla," mawimbi mengi ya ukamataji ulioratibiwa yalitekelezwa nchini kote. Watu 38,607 walikamatwa; 17,160 kati yao waliteswa au kutiwa kasumba kwa lazima; 6,115 walihukumiwa; na angalau Wakristo 46 waliteswa hadi kufa. Wengine wengi wasiohesabika walitoweka, mawasiliano na wao yalipotea, au walilazimika kutoroka. Ripoti hii itatoa muhtasari wa "Vita vya Jumla," ikifichua ukandamizaji wa umwagaji damu wa CCP dhidi ya Wakristo katika miaka hii mitatu.

00:17 Mnamo 2020, CCP Ilianzisha "Vita vya Jumla" vya Miaka Mitatu kwa Lengo la Kuliangamiza Kabisa Kanisa la Mwenyezi Mungu

05:09 "Vita vya Jumla" vya Miaka Mitatu vya CCP Kulikandamiza Kanisa la Mwenyezi Mungu:Septemba hadi Desemba 2020— Angalau Wakristo 4,093 walikamatwa

09:33 "Vita vya Jumla" vya Miaka Mitatu vya CCP Kulikandamiza Kanisa la Mwenyezi Mungu: 2021—Angalau Wakristo 11,156 Walikamatwa

14:41 "Vita vya Jumla" vya Miaka Mitatu vya CCP Kulikandamiza Kanisa la Mwenyezi Mungu: 2022—Angalau Wakristo 10,895 Walikamatwa

19:52 "Vita vya Jumla" vya Miaka Mitatu vya CCP Kulikandamiza Kanisa la Mwenyezi Mungu: 2023—Angalau Wakristo 12,463 Walikamatwa

24:17 Mnamo 2020, CCP Ilianzisha "Vita vya Jumla" vya Miaka Mitatu kwa Lengo la Kuliangamiza Kabisa Kanisa la Mwenyezi Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp