Ukweli Kuhusu Mateso ya Kikatili ya CCP Dhidi ya Wakristo | Rekodi ya Ukweli ya Mateso ya Kikatili ya CCP Dhidi ya Wakristo (Sehemu ya 1)
CCP, chama cha Kimaksi kinachomkana Mungu, kimetawala kwa zaidi ya miaka 70. Katika kipindi hiki, kila kiongozi wa chama ameitesa imani ya kidini bila kuchoka, na itikadi hii imesalia kuwa thabiti sana. Wao hutunga sera za kikatili kila mara na kutoa nyaraka zisizohesabika za siri. Wanatawala vyombo vya dola ili kutekeleza sera ya serikali kuu ya kuangamiza imani ya kidini. Hii imesababisha mauaji na mateso ya mamilioni ya waumini wa dini.
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?