Swahili Christian Video "Bahati na Bahati Mbaya" | Mshukuru Mungu kwa Neema Yake ya Ajabu

30/04/2018

Kwa sababu yeye alitoka katika familia iliyo masikini, tangu akiwa na umri mdogo Du Juan alikusudia kutengeneza pesa nyingi sana apate kuishi maisha mazuri. Ili kufikia lengo hili, aliacha shule mapema zaidi kwenda kufanya kazi ya mikono, chochote angeweza kufanya ili apate pesa. Yeye hakulalamika wakati kazi ilikuwa ngumu na ya kuchokesha. Hata hivyo, yeye hakupata matokeo aliyotaka. Bila kujali jinsi alivyofanya kazi kwa bidii, hakuweza kupata yale maisha aliyojitakia mwenyewe. Mwaka wa 2008, bado akiwa na ndoto ya kutengeneza pesa nyingi, yeye na mumewe walikwenda Japan kufanya kazi. Baada ya miaka michache, shinikozo la kazi nzito na saa nyingi za kazi zilimsababisha kuanguka kutokana na uchovu mwingi. Matokeo ya uchunguzi wa hospitali yalifanya hisia zake kushuka chini zaidi kuliko wakati mwengine ule, lakini ili aweze kufikia njozi yake, Du Juan hakuwa tayari kukata tamaa. Aliendelea kufanya kazi, akiubeba ugonjwa wake, akili yake ikiwa imelenga kuendelea kujitahidi. Hatimaye, mateso ya hali yake yalisababisha kusimamisha juhudi zake za kutafuta pesa. Katikati ya uchungu wake, alianza kutafakari: Kwa nini baada ya yote mtu anaishi maisha haya? Je, ina thamani gani kuhatarisha maisha yako mwenyewe kwa sababu ya pesa? Je, ni ukweli kwamba maisha ya pesa ni maisha ya furaha? Mashaka haya siku zote yalizunguka akili yake. Muda mfupi baadaye, wokuvu wa Mwenyezi Mungu wa zile siku za mwisho ukaja kwake. Kutokana na maneno ya Mwenyezi Mungu, yeye alikuja kujua chanzo cha maisha ya mwanadamu ya uchungu, na pia alielewa kile ambacho mwanadamu alipaswa kuishi kwa ajili yake, na jinsi ya kuishi kabla aweze kupata maisha yenye maana kwa binadamu....Wakati wowote alipofikiria kuhusu tukio hilo, Du Juan alishusha pumzi kwa hisia: Hili pigo la ugonjwa kwa kweli lilimfanya apate baraka kutoka kwa majonzi!

Baadhi ya taarifa katika video hii zinatoka kwa: https://stockfootage.com/

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp