Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatua Tatu za Kazi | Dondoo 2
13/06/2020
Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika awamu tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Awamu hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, ambayo ni kusema, ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu ambaye ameharibiwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati huo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani. Hivyo, kama ilivyo kazi ya wokovu imegawanywa katika awamu tatu, kwa hivyo pia vita dhidi ya Shetani vimegawanywa katika awamu tatu, na vipengele hivi viwili vya kazi ya Mungu vinafanywa sawia. Vita dhidi ya Shetani ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, na kwa kuwa kazi ya wokovu wa wanadamu sio jambo linaloweza kukamilishwa kwa mafanikio katika awamu moja, vita dhidi ya Shetani pia vimegawanywa katika awamu na vipindi, na vita vya kupigana na Shetani vinaambatana na mahitaji ya mwanadamu na kiwango cha kupotoshwa kwa mwanadamu na Shetani. Pengine, katika mawazo ya mwanadamu, anaamini kuwa katika vita hivi Mungu atachukua silaha dhidi ya Shetani, katika njia sawa na vile ambavyo majeshi mawili yatapigana. Hili ni jambo ambalo akili ya mwanadamu ina uwezo wa kukisia, na lisilo dhahiri kupita kiasi na azimio lisiloweza kutendeka, na bado ndilo mwanadamu anaamini. Na kwa sababu Nasema hapa kuwa njia ya wokovu wa mwanadamu ni kupitia vita na Shetani, mwanadamu anawaza ya kwamba hivi ndivyo vita vinavyoendeshwa. Katika kazi ya wokovu wa mwanadamu, awamu tatu zimefanywa, ambayo ni kusema kuwa vita na Shetani vimegawanyika katika awamu tatu kabla ya kushindwa kabisa kwa Shetani. Na bado ukweli wa ndani wa kazi yote ya vita dhidi ya Shetani ni kwamba matokeo yake yanatimizika kupitia kuzawadia mwanadamu neema, na kuwa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, kuzisamehe dhambi za mwanadamu, kumshinda mwanadamu, na kumfanya mwanadamu awe kamili. Kama jambo la kweli, vita na Shetani sio kuchukua silaha dhidi ya Shetani, bali ni wokovu wa mwanadamu, kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kubadilishwa kwa tabia ya mwanadamu ili kwamba aweze kuwa na ushahidi wa Mungu. Hivi ndivyo Shetani anashindwa. Shetani anashindwa kwa kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Wakati Shetani ameshindwa, yaani, wakati mwanadamu ameokolewa kabisa, basi Shetani aliyeaibika atafungwa kabisa, na kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kiini cha wokovu wa mwanadamu ni vita dhidi ya Shetani, na vita na Shetani vitajitokeza kimsingi katika wokovu wa mwanadamu. Awamu ya siku za mwisho, ambapo mwanadamu atashindwa, ni awamu ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na pia kazi ya wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa utawala wa Shetani. Maana ya ndani ya ushindi wa mwanadamu ni kurudi kwa mfano halisi wa Shetani, mtu ambaye amepotoshwa na Shetani, kwa Muumba baada ya ushindi wake, kwa njia ambayo atamwacha Shetani na kurejea kabisa kwa Mungu. Kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni kazi ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na awamu ya mwisho ya kazi ya Mungu ya usimamizi kwa ajili ya kushindwa kwa Shetani. Bila kazi hii, wokovu kamili wa mwanadamu hatimaye haungewezekana, kushindwa kikamilifu kwa Shetani kusingewezekana, na mwanadamu kamwe hangekuwa na uwezo wa kuingia kwenye hatima ya ajabu, ama kuwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kwa hivyo, kazi ya wokovu wa mwanadamu haiwezi kukamilika kabla vita dhidi ya Shetani havijahitimishwa, kwa kuwa msingi wa kazi ya Mungu wa usimamizi ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Mwanadamu wa kwanza kabisa alikuwa kwa mikono ya Mungu, lakini kwa sababu ya majaribu ya Shetani na upotovu wake, mwanadamu alifungwa na Shetani na kuanguka katika mikono ya yule mwovu. Kwa hivyo, Shetani akakuwa mlengwa wa kushindwa katika kazi ya Mungu ya usimamizi. Kwa sababu Shetani alichukua umiliki wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu ndiye kiini cha kazi yote ya Mungu ya usimamizi, kama mwanadamu ni wa kuokolewa, basi ni lazima anyakuliwe kutoka mikononi mwa Shetani, ambayo ni kusema kuwa mwanadamu ni lazima achukuliwe baada ya kuwa katika mateka ya Shetani. Shetani anashindwa kupitia mabadiliko ya tabia ya mwanadamu ya zamani ambayo hurejesha hisia zake za awali, na kwa njia hii, mwanadamu, ambaye amechukuliwa mateka, anaweza kunyakuliwa kutoka mikononi mwa Shetani. Kama mwanadamu anawekwa huru kutokana na ushawishi wa Shetani na utumwa wake, Shetani ataaibika, mwanadamu hatimaye atarejeshwa, na Shetani atakuwa ameshindwa. Na kwa sababu mwanadamu ameachiliwa kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, mwanadamu atakuwa mabaki ya vita hivi vyote, na Shetani atakuwa ndiye mlengwa ambaye ataadhibiwa punde tu vita hivi vitakapokamilika, baada ya kuwa kazi nzima ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu
God’s Three Stages of Work Have Utterly Saved Man
I
The 6,000 years of God's work are divided in three stages: the Age of Law, the Age of Grace, and the Age of Kingdom. All to save corrupt man and battle Satan, both divided into three stages of work. This battle with Satan is for mankind's salvation, which can't succeed in one stage, so the battle is in phases. The war is waged upon Satan according to the needs of man and the extent of Satan's corruption. The work of man's salvation is divided in three stages, and so is the battle with Satan. But the result of the battle comes through giving grace to man, becoming man's sin offering, conquering and perfecting man.
II
God doesn't battle Satan with weapons, but works man's life and saves him, changing man's disposition, so man can bear witness for Him. And this is how Satan will be defeated and shamed. When it is bound, man will be saved.
III
The substance of man's salvation is battle waged with Satan, the war with Satan shown in salvation of man. The stage of the last days when man will be conquered is the last stage of battle, saving man fully from Satan. If man's freed from Satan's grasp, Satan will be shamed. Man will be taken back, Satan will be finished. Man will be spoils and Satan will be punished. The work of saving man will be fully accomplished. The work of man's salvation is divided in three stages, and so is the battle with Satan. But the result of the battle comes through giving grace to man, becoming man's sin offering, conquering and perfecting man, conquering and perfecting man, conquering and perfecting man.
from Follow the Lamb and Sing New Songs
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video