Dondoo ya Filamu ya Injili ya 1 Kutoka “Wakati Wa Mabadiliko”: Je, Tutabadili Umbo Mara Moja na Kunyakuliwa Hadi Katika Ufalme wa Mbinguni Wakati Bwana Atarudi?

1082 |03/03/2018

Watu wengine huongozwa na maneno ya Paulo katika suala la kumngoja Bwana ili kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni: “Kwa ghafla, kufumba na kufumbua, wakati wa tarumbeta ya mwisho: kwa maana tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa bila uovu, na tutabadilishwa” (1Kor 15:52). Wanaamini kwamba ingawa bado tunatenda dhambi siku zote bila kujinasua kutoka kwa pingu za asili ya dhambi, Bwana atazibadili taswira zetu mara moja na kutuleta katika ufalme wa mbinguni Atakapokuja. Pia kuna watu wanaoongozwa na neno la Mungu: “Si kila mtu aniitaye, Bwana, Bwana, ataingia katika ufalme wa mbinguni; lakini yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (Mat 7:21). “Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu” (Walawi 11:45). Wanaamini kuwa watu ambao bado wanatenda dhambi siku zote wako mbali na kufikia utakatifu na hawana sifa zinazostahili kabisa kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni. Mjadala wa kustaajabisha hivyo ukaanza….Hivyo, ni watu wa aina gani walio na sifa zinazostahili kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni? Tunakualika utazame video hii fupi.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi