Filamu ya Kikristo | “Imani Katika Mungu 3 – Inukeni, Wale Msiokubali Kuwa Watumwa” (Trela)
14/05/2020
Meng Changlin, mfanyakazi mwenza wa Kanisa la Kanuni Tatu za Binafsi, hapo awali alidhani kwamba kumwamini Bwana katika Kanisa la Kanuni Tatu za Binafsi kungemuepusha na mateso ya CCP. Hata hivyo, baada ya Xi Jinping kuingia madarakani, CCP kinazidisha mateso yake kwa imani ya kidini, na hata Kanisa linaloendeshwa na serikali la Kanuni Tatu za Binafsi linaanza kuathiriwa na ukandamizaji na mateso; misalaba yao mingi inabomolewa na makanisa kubomolewa, na CCP hata kinaanza kuyalazimisha makanisa yapeperushe bendera ya taifa, yaimbe wimbo wa taifa, na kutundika picha ya Mwenyekiti Xi…. Katika makabiliano na mateso haya ya CCP, mchungaji wake hawaongozi waumini katika kuomba ili kutafuta mapenzi ya Mungu, lakini badala yake anakitii CCP katika mambo yote. Meng Changlin anaamini kuwa hayo yanakiuka kabisa njia ya Bwana, na kwamba wamezama na kuwa watumwa wa Shetani, mfalme wa ibilisi. Anamsihi mchungaji wake aondoke katika Kanisa la Kanuni Tatu za Binafsi na achukue njia ya kanisa la nyumbani, lakini mchungaji wake anamkemea na kumzuia. Ni katika wakati huu ndipo anakutana na Xiang Zhiheng, Mkristo katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kupitia kutafuta na ushirika, Meng Changlin anaweza kuona kwa dhahiri zaidi kuliko hapo awali kuwa sera ya Kanisa la Kanuni Tatu za Binafsi bila shaka ni hila ya CCP ya kutafuta muda zaidi wa kupanga mpango wake wa kuondoa kabisa imani ya kidini; anaona kwamba wachungaji na wazee wanapowaongoza waumini kukitii CCP, wanampinga na kumsaliti Mungu, na kwamba wote ni wachungaji wa uwongo wanaomhudumia Shetani. Wakati huo huo, Meng Changlin anakuja kuelewa umuhimu wa kupitia mateso na shida kama sehemu ya imani katika Bwana, na anaona waziwazi kuwa imani katika Mungu chini ya mfumo wa utawala wa kishetani wa CCP inahitaji mtu kuhatarisha maisha yake ili kumfuata Mungu. Anakuja kuelewa kwamba kumwamini Mungu kunahitaji kusikiliza maneno ya Mungu na kumtii Mungu, na kwamba mtu hawezi kuwasikiliza au kuwatii watu badala ya Mungu. Meng Changlin na wale wengine, kupitia kutafuta na kuchunguza, wanaona kwamba maneno yote ya Mwenyezi Mungu ni ukweli na ni sauti ya Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi! Wanabubujikwa na furaha tele, na mwishowe wanaondokana na utumwa na vikwazo vya mfumo wa utawala wa kishetani wa CCP na vya wachungaji wa uwongo na wapinga Kristo katika ulimwengu wa dini. Wanarudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video