Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 203

02/11/2020

Kukamilishwa kuna maana gani? kushindwa kuna maana gani? Ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili apate kushindwa? Na ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili afanywe mkamilifu? Kushinda na kukamilisha yote yanakusudiwa kumkamilisha mwanadamu ili kwamba aweze kurejeshwa katika asili yake, na awe huru na tabia zake potovu za shetani na ushawishi wa Shetani. Huu ushindi huja mapema katika mchakato wa kumfinyanga mwanadamu, ikiwa na maana kwamba ni hatua ya kwanza ya kazi. Kukamilisha ni hatua ya pili, au hitimisho la kazi. Kila mwanadamu ni lazima apitie hali ya kushindwa; la sivyo hataweza kumfahamu Mungu na hawezi kujua kuwa kuna Mungu, yaani, hawezi kumtambua Mungu. Na iwapo mtu hamtambui Mungu, hataweza kufanywa mkamilifu na Mungu kwa sababu hatakuwa na vigezo vya kufanywa mkamilifu. Ikiwa humtambui Mungu, utawezaje kumfahamu? Utawezaje kumtafuta? Aidha, hutaweza kumshuhudia, wala kumtosheleza. Kwa hivyo, kila anayetaka kukamilishwa, hatua ya kwanza lazima iwe kupitia kazi ya kushinda. Hili ndilo sharti la kwanza. Ila, iwe ni kushinda au ukamilifu, kila moja ni lengo la mwanadamu afanyaye kazi na kubadilishwa na kazi hiyo, na kila moja ni kipengele katika kazi ya kusimamia mwanadamu. Hizi hatua mbili ndizo zinahitajika kumgeuza yeyote kuwa mtu mkamilifu; hakuna moja kati yazo inaweza kurukwa. Ni kweli kuwa “kushindwa” hakuonekani kuwa ni jambo zuri, ila ni kweli kuwa mchakato wa kumshinda mtu ni mchakato wa kumbadilisha mwanadamu. Baada ya kushindwa, unaweza kuwa hujapoteza tabia yako mbovu kabisa, ila utakuwa umeijua. Kupitia kazi ya kushinda, utapata kujua uduni wa ubinadamu wako, na vilevile kufahamu utovu wako wa nidhamu. Japo hutaweza kuyaacha haya au kuyabadilisha ndani ya muda mfupi wa kazi ya kushinda, utayajua baadaye. Haya yanaujenga msingi wa ukamilifu wako. Kwa hivyo kushinda na kukamilisha yote yanafanywa kumbadilisha mwanadamu, kumtoa mwanadamu tabia zake mbovu za Kishetani ili ajitolee kikamilifu kwa Mungu. Ni kwamba tu kushindwa ni hatua ya kwanza katika kubadilisha tabia ya mwanadamu na pia hatua ya kwanza ya mwanadamu kujitoa kikamilifu kwa Mungu, hatua iliyo chini ya ukamilifu. Tabia za maisha ya mtu aliyeshindwa hubadilika kiasi kidogo kuliko ya mtu ambaye amepata ukamilifu. Kushindwa na kufanywa mkamilifu ni tofauti kabisa kwa kuwa ni hatua tofauti za kazi na kwa kuwa huhitaji vigezo tofauti kutoka kwa wanadamu, huku ushindi ukiwa na vigezo vya chini na ukamilifu ukiwa na vigezo vya juu. Walio wakamilifu ni wenye haki, watu watakatifu na safi; wao ni udhihirisho wa kazi ya kusimamia wanadamu, au matokeo ya mwisho. Japo si wanadamu wasio na doa, ni watu wanaotaka kuishi maisha ya thamani. Lakini walioshindwa hukiri tu kwa vinywa vyao kuwa Mungu Yupo; wanakiri kuwa Mungu amepata mwili, kwamba neno linaonekana katika mwili, na kwamba Mungu amekuja duniani kufanya kazi ya hukumu na kuadibu watu. Aidha wanakiri kuwa hukumu na kuadibu kwa Mungu na mapigo Yake na usafishaji Wake ni faida kwa mwanadamu. Yaani, wameanza kuwa na sifa za ubinadamu, na wana ufahamu mdogo kuhusu maisha ila si bayana. Kwa maneno mengine, wameanza tu kuwa na ubinadamu. Haya ni matokeo ya kushindwa. Watu waingiapo katika njia ya ukamilifu, tabia zao za zamani zaweza kubadilishwa. Aidha, maisha yao huendelea kukua na taratibu hujitosa zaidi katika ukweli. Wanaweza kuchukia dunia na kuwachukia wale wote ambao hawafuati ukweli. Hususan hujichukia wao wenyewe, na hata zaidi ya hayo, wanajitambua vyema. Wana hiari kuishi kulingana na ukweli na hulenga kufuata ukweli. Hawako radhi kuishi katika mawazo ya bongo zao, na huchukia kujitukuza, kujisifu, na kujiinua kwa mwanadamu. Wananena kwa adabu ya hali ya juu, wanafanya mambo kwa utambuzi na hekima, ni waaminifu na watiifu kwa Mungu. Wakipitia kuadibu na hukumu, wao hawakuwi wanyonge au wasioonyesha hisia tu, bali hutoa shukrani kwa ajili ya kuadibu na hukumu zitokazo kwa Mungu. Wanaamini hawawezi kuishi bila kuadibu na hukumu ya Mungu; wanaweza kupata ulinzi Wake kupitia haya. Hawafuati imani ya amani na furaha na ya kutafuta mkate wa kuwashibisha. Wala hawafuati raha za muda za kimwili. Hili ndilo wakamilifu huwa nalo. Baada ya watu kushindwa, wao hukubali kwamba kuna Mungu. Lakini matendo yo yote ambayo huja na kukubali kuweko kwa Mungu, matendo haya ni machache ndani yao. Neno kuonekana katika mwili lina maana gani kwa kweli? Kupata mwili kuna maana gani? Ni nini ambacho Mungu mwenye mwili amefanya? Ni nini lengo na umuhimu wa kazi Yake? Baada ya kupitia kazi Yake nyingi sana, kupitia matendo Yake katika mwili, umepata nini? Ni baada tu ya kufahamu mambo haya yote ndiyo utakuwa mtu aliyeshindwa. Kama wewe utasema tu kwamba unakubali kuwa kuna Mungu, lakini huwachi kile unachopaswa kuwacha na kukosa kuacha raha za mwili ambazo unapaswa kuacha, lakini badala yake uendelee kutamani maliwazo ya mwili kama ulivyofanyadaima, na ikiwa huwezi kuachilia ubaguzi wowote dhidi ya ndugu, na kuhusu utendaji mwingi rahisi huwezi kulipa stahili yako kutimiza matendo hayo, basi hilo linathibitisha wewe bado hujashindwa. Kwa hiyo, hata kama unaelewa mengi, yote itakuwa bure. Walioshindwa ni watu ambao wametimiza mabadiliko fulani ya mwanzo na kuingia kwa mwanzo. Kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu huwasababisha kuwa na maarifa ya mwanzo ya Mungu na ufahamu wa mwanzo wa ukweli. Hata kama kuhusu ukweli mwingi wa kina, na wa chembechembe zaidi huwezi kuingia kabisa katika uhalisi wake, unaweza kutia katika vitendo ukweli mwingi wa mwanzo katika maisha yako halisi, kama vile unaohusu raha zako za mwili au hali yako binafsi. Yote haya, bila shaka, ni kile kinachotimizwa ndani ya wale wanaopitia kushinda. Mabadiliko fulani katika tabia yanaweza pia kuonekana ndani ya walioshindwa. Kwa mfano, mavazi na unadhifu wao na maisha yao—haya yanaweza kubadilika. Mtazamo wao kuhusu kumwamini Mungu hubadilika, wao hupata uwazi kuhusu chombo cha ukimbizaji wao, na matamanio yao huongezeka. Wakati wa kushindwa, tabia yao ya maisha inaweza pia kubadilika kwa kukubaliana. Sio kwamba wao hawabadiliki kabisa. Ni vile tu mabadiliko yao ni ya juujuu, ya mwanzo, na madogo zaidi kuliko mabadiliko katika tabia na chombo cha ukimbizaji ambayo yangeonekana baada ya mtu kukamilishwa. Kama wakati wa kushindwa, tabia ya mtu haibadiliki kabisa na hapati hata ukweli kidogo, basi mtu wa aina hii huwa tu kipande cha takataka na ni bure kabisa! Watu ambao hawajashindwa hawawezi kukamilishwa! Na kama mtu hutafuta tu kushindwa, hawezi kufanywa kuwa kamili kwa ukamilifu, hata kama tabia yake ilionyesha mabadiliko fulani ya kukubaliana wakati wa kazi ya kushinda. Yeye pia atapoteza ukweli wa mwanzo aliopata. Kuna tofauti kubwa mno kati ya kiasi cha mabadiliko ya tabia ndani ya walioshindwa na waliokamilishwa. Lakini kushindwa ni hatua ya kwanza katika mabadiliko; ni msingi. Kukosa mabadiliko haya ya mwanzo ni thibitisho kwamba mtu kwa kweli hamjui Mungu kabisa kwa sababu ufahamu huu hutoka kwa hukumu, na hukumu hii ni kipengee kikuu katika kazi ya kushinda. Kwa hiyo, kila mtu aliyekamilishwa amepitia kushindwa. Ama sivyo, hangeweza labda kukamilishwa.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp