Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 201

27/09/2020

Kazi ya siku za mwisho inavunja kanuni zote, bila kujali kama umelaaniwa au kuadhibiwa, maadamu tu uisaidie kazi Yangu, na una manufaa kwa kazi ya ushindi ya leo, na bila kujali kama wewe ni uzao wa Moabu au kizazi cha joka kuu jekundu, maadamu tu unatekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu katika hatua hii ya kazi, na kufanya kadri unavyoweza, basi matokeo yanayotarajiwa yatatimizwa. Wewe ni kizazi cha joka kuu jekundu, na ni uzao wa Moabu; kwa ujumla, wale wote walio wa mwili na damu ni viumbe wa Mungu, na waliumbwa na Muumba. Wewe ni kiumbe wa Mungu, hupaswi kuwa na chaguo lolote, na huu ndio wajibu wako. Bila shaka, leo kazi ya Muumba imeelekezwa kwa ulimwengu mzima. Bila kujali wewe ni uzao wa nani, zaidi ya yote, nyinyi ni mojawapo wa viumbe wa Mungu, ninyi—uzao wa Moabu—ni sehemu ya viumbe wa Mungu, ni vile tu nyinyi mna thamani ya chini. Kwa kuwa, leo, kazi ya Mungu inatekelezwa miongoni mwa viumbe wote, na imelenga ulimwengu mzima, Muumba yuko huru kuchagua watu, masuala, au vitu vyovyote ili viweze kufanya kazi Yake. Hajali wewe ni uzao wa nani; maadamu tu wewe ni mmoja wa viumbe wake, na maadamu una manufaa katika kazi Yake—kazi ya ushindi na ushuhuda—Ataifanya kazi Yake ndani yako bila haya yoyote. Hili linaharibu kabisa dhana za watu za kitamaduni, ambayo ni kwamba Mungu hatawahi kamwe kufanya kazi miongoni mwa Mataifa, hususan wale ambao wamelaaniwa na ambao ni duni; kwa maana wale ambao wamelaaniwa, uzao wao wa baadaye nao utaendelea kulaaniwa milele, hawatakuwa na nafasi ya wokovu; Mungu hatawahi kamwe kushuka na kufanya kazi katika nchi ya Mataifa, na Hatakanyaga mguu Wake katika nchi yenye uchafu, maana Yeye ni mtakatifu. Dhana hizi zote zimevunjwa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Jua kwamba Mungu ni Mungu wa viumbe vyote, ni mtawala wa mbingu na nchi na vitu vyote, na si Mungu wa watu wa Israeli pekee. Hivyo, kazi hii katika nchi ya Uchina ni ya umuhimu mkubwa, na unadhani haitaenea miongoni mwa mataifa yote? Ushuhuda mkubwa wa siku za usoni hautakomea Uchina tu; ikiwa Mungu angewashinda nyinyi tu, je, mapepo wangeshawishika? Hawaelewi maana ya kushindwa, au nguvu kubwa ya Mungu, na ni pale tu ambapo wateuliwa wa Mungu katika nchi yote watakapoona matokeo ya mwisho ya kazi hii ndipo viumbe wote watakuwa wameshindwa. Hakuna ambao wapo nyuma sana au waovu sana kuliko uzao wa Moabu. Iwapo tu watu hawa wataweza kushindwa—wale ambao ni waovu sana, ambao hawakumtambua Mungu au kuamini kwamba kuna Mungu wameshindwa, na kumtambua Mungu katika vinywa vyao, wakimtukuza, na wanaweza kumpenda—ndipo huu utakuwa ushuhuda wa ushindi. Ingawa wewe si Petro, mnaishi kwa kudhihirisha mfano wa Petro, mnaweza kuwa na ushuhuda wa Petro, na ushuhuda wa Ayubu, na huu ni ushuhuda mkubwa sana. Hatimaye utasema: “Sisi sio Waisraeli, bali ni uzao wa Moabu uliotelekezwa, sisi sio Petro, ambaye hatuwezi kuwa na ubora wa tabia yake, wala sisi sio Ayubu, na hata hatuwezi kujilinganisha na azimio la Paulo la kuteseka kwa ajili ya Mungu na kujitoa kikamilifu kwa Mungu, na sisi tupo nyuma sana, na hivyo, hatustahili kufurahia baraka za Mungu. Mungu bado Ametuinua leo; kwa hiyo tunapaswa kumridhisha Mungu, na ingawa tuna ubora wa tabia au sifa haba, tupo radhi kumridhisha Mungu—tuna azimio hili. Sisi ni uzao wa Moabu, na tulilaaniwa. Hili lilitangazwa na Mungu, na wala hatuwezi kuibadilisha, lakini kuishi kwetu kwa kudhihirisha na maarifa yetu yanaweza kubadilika, na tumeazimia kumridhisha Mungu.” Utakapokuwa na azimio hili, itathibitisha kwamba umeshuhudia kuwa umeshindwa.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp