Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 198

05/10/2020

Leo, Ninafanya kazi miongoni mwa watu wateule wa Mungu walio Uchina kufichua tabia zao zote za uasi na kuufunua ubaya wao wote, na hili linatia muktadha wa kusema kila Ninachotaka kusema. Baadaye Nitafanya hatua nyingine ya kazi ya kuushinda ulimwengu wote. Nitatumia hukumu Yangu kwenu kuhukumu udhalimu wa kila mtu duniani kote kwa sababu ninyi watu ndio wawakilishi wa waasi miongoni mwa wanadamu. Wasiojikakamua watakuwa foili na vyombo vya kuhudumu tu, ila watakaojikakamua watatumika vizuri. Ni kwa nini Ninasema watakuwa foili? Ni kwa sababu maneno na kazi Yangu ya sasa vinalenga usuli wenu na kwa sababu mmekuwa wawakilishi na vielelezo vya uasi miongoni mwa wanadamu. Baadaye Nitapeleka maneno haya yanayowashinda kwa nchi za kigeni na kuyatumia kuwashinda watu wa huko, ila hutakuwa umeyafaidi. Je, hilo halitakufanya foili? Tabia potovu za wanadamu wote, matendo ya uasi wa mwanadamu, maumbile na sura mbaya za mwanadamu, zimeratibiwa zote katika maneno yanayotumiwa kuwashinda nyinyi. Baadaye Nitayatumia maneno haya kuwashinda watu wa kila taifa na kila dhehebu kwa sababu nyinyi ni mfano, kigezo. Hata hivyo, Sikupanga kuwaacha kwa makusudi; ukikosa kufanya vizuri katika utafutaji wako na kwa hivyo unathibitisha kuwa asiyeponyeka, hautakuwa tu chombo cha huduma na foili? Wakati mmoja Nilisema kwamba hekima Yangu hutumiwa kutegemea njama za Shetani. Kwa nini Nilisema hilo? Je, huo si ukweli unaounga mkono Ninachosema na kufanya wakati huu? Kama huwezi kuchukua hatua, kama hujakamilishwa lakini badala yake unaadhibiwa, je, hutakuwa foili? Labda umeteseka sana katika wakati wako, lakini sasa bado huelewi chochote; hujui kila kitu kuhusu uzima. Ingawa umeadhibiwa na kuhukumiwa, hujabadilika kamwe na ndani yako kabisa hujapata uzima. Wakati wa kutathmini kazi yako utakapofika, utapitia majaribio makali kama moto na hata majonzi makuu zaidi. Moto huu utageuza nafsi yako yote kuwa majivu. Kama mtu asiyekuwa na uzima, mtu asiye na aunsi ya dhahabu safi ndani yake, mtu ambaye bado amekatalia tabia potovu ya kale, na mtu asiyeweza hata kufanya kazi nzuri ya kuwa foili, ni jinsi gani hutaweza kuondoshwa? Kazi ya kushinda ina faida gani kwa mtu aliye na thamani ya chini kuliko peni na asiyekuwa na uzima? Wakati huo ufikapo, siku zenu zitakuwa ngumu zaidi kuliko za Nuhu na Sodoma! Maombi yenu hayatawasaidia wakati huo. Mara tu kazi ya wokovu ikiisha, utaanzaje tena kutubu? Mara tu kazi ya wokovu itakuwa imefanywa, hakutakuwa tena na kazi ya wokovu. Kitakachokuwepo ni mwanzo wa kazi ya kuadhibu uovu. Wewe hupinga, huasi, na hufanya mambo unayojua ni maovu. Je, wewe sio shabaha ya adhabu kali? Ninakuelezea hili wazi leo. Ukichagua kutosikia, wakati maafa yakufike baadaye, je, hautakuwa umechelewa kama utaanza wakati huo tu kuhisi majuto na kuanza kuamini? Nakupa nafasi ya kutubu leo, lakini wewe hauko radhi kufanya hivyo. Unataka kungoja kwa muda gani? Mpaka siku ya kuadibu? Sikumbuki dhambi zako za zamani leo; Nakusamehe tena na tena, kugeuka kutoka upande wako mbaya kutazama tu upande wako mzuri, kwa sababu maneno na kazi Yangu yote ya sasa yanatakiwa kukuokoa wewe na sina nia mbaya kwako. Lakini unakataa kuingia; huwezi kutambua mema kutoka kwa mabaya na hujui namna ya kufurahia wema. Je, mtu wa aina hii hanuii tu kungoja ile adhabu na malipo yenye haki?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp