Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII | Dondoo 169

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII | Dondoo 169

120 |04/08/2020

Mungu aliumba ulimwengu na ni Bwana wake; Yeye ndiye Anausimamia na Anaukimu huku Akiangalia kila neno na tendo. Pia Anatazama kila pembe ya maisha ya mwanadamu. Hivyo Mungu Aliuumba ulimwengu na umuhimu na thamani ya kila kitu na vile vile kazi yake, asili yake, na kanuni zake kwa ajili ya kuendelea kuishi zinaeleweka vizuri Kwake kama kiganja cha mkono wake. Mungu Aliuumba ulimwengu; unadhani Anapaswa kufanya utafiti juu ya kanuni hizi zinazouongoza ulimwengu? Je, Mungu Anahitajika kusoma maarifa au sayansi ya kibinadamu kufanya utafiti na kuyaelewa? (Hapana.) Je, kuna mtu yeyote miongoni mwa binadamu ambaye ana elimu kubwa na hekima ya kutosha kuelewa mambo yote kama Mungu Anavyoelewa? Hakuna. Sio? Je, kuna mamajusi au wanabiolojia ambao wanaelewa kweli jinsi ambavyo vitu vinaishi na kukua? Je, wanaweza kweli kuelewa thamani ya uwepo wa kila kitu? (Hawawezi.) Kwa nini? Vitu vyote viliumbwa na Mungu, na haijalishi ni kwa kiasi kikubwa au kwa kina kiasi gani binadamu anajifunza maarifa haya, au ni kwa muda mrefu kiasi gani wanajitahidi kujifunza, hawataweza kuelewa siri na makusudi ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, hiyo si sahihi? (Ndiyo.) Baada ya kujadili kwa kina hadi sasa, mnahisi kwamba mna uelewa wa juujuu wa maana ya kidokezo cha kirai “Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote”? (Ndiyo.) Nilijua kwamba Nilipojadili mada hii watu wengi wangefikiri kwa haraka juu ya jinsi Mungu ni kweli na namna ambavyo neno Lake linatukimu, lakini wangeifikiria tu katika kiwango hiki. Baadhi hata wangehisi kwamba Mungu kukimu maisha ya binadamu, kutoa chakula na kinywaji cha kila siku na mahitaji yote ya kila siku haihesabiki kama kumkimu mwanadamu. Je, baadhi ya watu hawahisi namna hii? Je, nia ya Mungu haipo wazi katika jinsi ambavyo aliumba kila kitu ili kwamba binadamu awepo na kuishi kwa kawaida? Mungu anadumisha mazingira ambamo watu wanaishi na anatoa vitu vyote ambavyo binadamu huyu anahitaji. Aidha, Anasimamia na kuwa mtawala juu ya vitu vyote. Haya yote yanamfanya binadamu kuishi kwa kawaida na kustawi kwa kawaida; ni kwa njia hii ndipo Mungu Anavikimu vitu vyote na binadamu. Je, watu hahitaji kutambua na kuelewa mambo haya? Pengine baadhi wanaweza kusema, “Mada hii ipo mbali sana na maarifa yetu juu ya Mungu Mwenyewe wa kweli, na hatutaki kujua hili kwa sababu binadamu hawezi kuishi kwa mkate pekee, lakini badala yake anaishi kwa neno la Mungu.” Hili ni sahihi? (Hapana.) Kosa ni lipi hapa? Je, mnaweza kuwa na uelewa kamili juu ya Mungu ikiwa mnaelewa tu vitu ambavyo Mungu amesema? Ikiwa mnakubali tu kazi Yake na hukumu Yake na kuadibu, je, mtakuwa na uelewa kamili juu ya Mungu? Ikiwa mnaelewa sehemu ndogo tu ya tabia ya Mungu, sehemu ndogo ya mamlaka ya Mungu, hiyo inatosha kupata uelewa juu ya Mungu, sio? (Hapana.) Matendo ya Mungu yanaanza na uumbaji Wake wa ulimwengu na yanaendelea leo ambapo matendo yake ni dhahiri muda wote na kila wakati. Ikiwa watu wanaamini kwamba Mungu yupo kwa sababu tu Amewachagua baadhi ya watu ambao kwao Anafanya kazi Yake kuwaokoa watu hao, na kama wanaamini kwamba mambo mengine hayamhusishi Mungu, mamlaka Yake, hadhi Yake, na matendo Yake, je, hiyo inaweza kuchukuliwa kuwa kumfahamu Mungu kweli? Watu ambao wana hayo yanayoitwa maarifa ya Mungu—ambayo yamejikitia katika mtazamo wa upande mmoja kwamba Mungu yupo tu kwenye kundi la watu. Je, haya ni maarifa ya kweli juu ya Mungu? Sio kwamba watu wenye aina hii ya maarifa juu ya Mungu wanakataa uumbaji Wake wa vitu vyote na utawala wao juu Yao? Baadhi ya watu hawatamani kukiri hili, na wanaweza kufikiria: “Sioni utawala wa Mungu juu ya vitu vyote, ni kitu ambacho kipo mbali sana na mimi na sitaki kukielewa. Mungu Anafanya chochote anachotaka na wala hakinihusu. Ninachokiangalia zaidi ni kukubali uongozi wa Mungu na neno Lake na nitafanywa mkamilifu na nitaokolewa na Mungu. Nitazingatia tu mambo haya, lakini sitajaribu kuelewa kitu kingine chochote, au kukiwazia wazo lolote. Kanuni yoyote ambayo Mungu Aliifanya Alipoviumba vitu vyote au chochote ambacho Mungu Anafanya kuvikimu na kumkimu mwanadamu wala hakinihusu.” Haya ni mazungumzo ya aina gani? Hii sio fedheha kabisa? Je, kuna mtu yeyote miongoni mwenu anayefikiri hivi? Ninajua kwamba kuna watu wengi sana wanaofikiri namna hii hata kama hamtasema. Aina ya mtu huyu wa kuamini katika maandiko anaweza kutumia kile kinachoitwa msimamo wao wa kiroho katika namna wanavyotazama kila kitu. Wanataka kumwekea Mungu mipaka katika Biblia, kumwekea Mungu mipaka kwa maneno Aliyoyazungumza, na kumwekea Mungu mipaka katika neno lilikoandikwa. Hawatamani kufahamu zaidi kuhusu Mungu na hawataki Mungu Aweke umakini zaidi katika kufanya mambo mengine. Aina hii ya kufikiri ni ya kitoto na ni ya kidini sana. Je, watu wenye mitazamo hii wanaweza kumjua Mungu? Wanaweza kuwa na wakati mgumu kumjua Mungu. Leo nimesimulia hadithi hizi mbili na nimezungumza juu ya vipengele hivi viwili. Baada ya kuzisikia tu na baada ya kukutana nazo tu, unaweza kuhisi kwamba ni za kina au hata ni za kidhahania kidogo na ngumu kutambua na kufahamu. Inaweza kuwa ni vigumu kuzihusianisha na matendo ya Mungu na Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, matendo yote ya Mungu na yote Aliyoyafanya miongoni mwa vitu vyote na miongoni mwa binadamu wote yanapaswa kueleweka kwa wazi na kwa usahihi kwa kila mtu na kwa kila mmoja ambaye anatafuta kumjua Mungu. Maarifa haya yatakupatia uthibitisho wa imani katika uwepo wa kweli wa Mungu. Pia yatakupatia maarifa sahihi juu ya hekima ya Mungu, nguvu Zake, na jinsi ambavyo anakimu vitu vyote. Itakufanya uelewe kwa wazi kabisa uwepo wa kweli wa Mungu na kuona kwamba siyo hadithi ya kubuni, na sio kisasili. Hii inakufanya uone kwamba si ya kidhahania, na sio tu nadharia, na kwamba Mungu hakika sio tu riziki ya kiroho, lakini ni kweli yupo. Aidha, inakufanya umfahamu Yeye kama Mungu kwa namna ambayo amekimu vitu vyote na binadamu; Anafanya hivi kwa njia Yake mwenyewe na kulingana na wizani Wake mwenyewe. Hivyo mtu anaweza kusema kwamba ni kwa sababu Mungu Aliumba vitu vyote na Akavipatia kanuni kwamba kwa amri Yake kila kimoja kinafanya kazi zake kilizopangiwa, vinatimiza majukumu yao, na kutimiza jukumu ambalo lilipewa kila kimoja. Vitu vyote vinatimiza jukumu lao kwa ajili ya binadamu, na hufanya hivi katika sehemu, mazingira ambamo watu wanaishi. Ikiwa Mungu hangefanya mambo namna hii na mazingira ya binadamu hayangekuwa jinsi yalivyo, imani ya watu kwa Mungu au wao kumfuata Yeye—hakuna ambacho kingewezekana; yangekuwa tu mazungumzo ya bure, hii sio sahihi?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi