Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 155

21/07/2020

Katika mchakato wa mwanadamu kujifunza maarifa, Shetani atatumia mbinu zozote, iwe kufafanua hadithi, akimpa tu kipande kimoja cha maarifa, au kumruhusu aridhishe tamaa zake au aridhishe mawazo Je, uko wazi kuhusu njia hasa anayotaka Shetani kukuongoza? Watu wanafikiri kwamba hakuna chochote kibaya na kujifunza maarifa, kwamba ni mkondo wa kiasili. Kuisema bila kutia chumvi, kukuza mawazo ya juu ama kuwa na matarajio ni kuwa na hamu ya kupata, na hii inapaswa kuwa njia sawa katika maisha. Iwapo watu wanaweza kufanikisha mawazo yao wenyewe, ama kuwa na kazi maishani mwao—je, si ni adhimu zaidi kuishi namna hii? Sio tu kuheshimu babu za mtu kwa njia hiyo bali pia ikiwezekana kuacha alama yako katika historia—hili si jambo zuri? Hili ni jambo zuri katika macho ya watu wa kidunia na kwao linapaswa kuwa la kufaa na njema. Je, Shetani, hata hivyo, na malengo yake husuda, anawapeleka tu watu kwa njia ya aina hii na kisha kuamua amemaliza? Bila shaka la. Kwa kweli, haijalishi jinsi yalivyo juu mawazo ya mwanadamu, haijalishi matamanio ya mwanadamu ni ya uhalisi jinsi gani ama jinsi yote yanaweza kuwa ya kufaa, yote ambayo mwanadamu anataka kufikia, yote ambayo mwanadamu anatafuta yameunganishwa bila kuchangulika na maneno mawili. Haya maneno mawili ni muhimu sana kwa maisha ya kila mtu, na haya ni mambo ambayo Shetani ananuia kuingiza ndani ya mwanadamu. Maneno haya mawili ni yapi? Moja ni “umaarufu” na nyingine ni “faida”: Ni umaarufu na faida. Shetani anatumia njia ya hila sana, njia ambayo iko pamoja sana na dhana za watu; si aina ya njia kali. Katikati ya kutoelewa, watu wanakuja kukubali njia ya Shetani ya kuishi, kanuni zake za kuishi, kuanzisha malengo ya maisha na mwelekeo wao katika maisha, na kwa kufanya hivyo wanakuja pia bila kujua kuwa na mawazo katika maisha. Haijalishi mawazo haya yanaonekana kusikika kuwa ya juu kiasi gani katika maisha, ni kisingizio tu ambacho kinahusiana kwa kutochangulika kwa umaarufu na faida. Mtu yeyote aliye mkubwa ama maarufu, watu wote kwa hakika, chochote wanachofuata maishani kinahusiana tu na haya maneno mawili: “umaarufu” na “faida.” Sivyo? Watu hufikiri kwamba punde tu wanapata umaarufu na faida, wanaweza basi kuyatumia kwa faida yao kufurahia hadhi ya juu na utajiri mwingi, na kufurahia maisha. Baada ya wao kuwa na umaarufu na faida, wanaweza basi kuyatumia kwa faida yao katika kutafuta kwao raha na kufurahia kwao kwa fidhuli mwili. Watu kwa hiari, lakini bila kujua, wanachukua miili na akili zao na vyote walivyonavyo, siku zao za baadaye, na kudura zao na kuzikabidhi zote kwa Shetani ili kupata umaarufu na faida wanayotaka. Watu kweli hufanya hivi kamwe bila kusita kwa muda, kamwe bila kujua haja ya kupata tena yote. Je, watu bado wanaweza kujidhibiti baada ya wao kumkimbilia Shetani na kuwa mwaminifu kwake kwa njia hii? Bila shaka, la. Wanadhibitiwa na Shetani kikamilifu na kabisa. Pia kikamilifu na kabisa wamezama katika bwawa na hawawezi kujinusuru. Baada ya mtu kukwama katika umaarufu na faida, hatafuti tena kile kilichong’aa, kile chenye haki ama yale mambo ambayo ni mazuri na mema. Hii ni kwa sababu nguvu za ushawishi ambazo umaarufu na faida yanayo juu ya watu ni kubwa mno, na vinakuwa vitu vya watu kutafuta katika maisha yao yote na pia milele bila kikomo. Hili si ukweli? Watu wengine watasema kwamba: “Kujifunza maarifa si chochote zaidi ya kusoma vitabu ama kujifunza mambo kadhaa ambayo hatujui tayari, ili wasiwe nyuma ya nyakati ama wasiwachwe nyuma na dunia. Maarifa yanafunzwa tu ili tuweze kuweka chakula mezani, kwa sababu ya siku zetu za baadaye ama kwa sababu ya mahitaji ya kimsingi.” Sasa unaweza kuniambia iwapo kuna mtu yeyote ambaye atastahimili mwongo wa kusoma kwa bidii kwa mahitaji ya kimsingi tu, ili kutatua swala la chakula tu? (La, hakuna.) Hakuna watu kama hawa. Kwa hivyo ni nini anatesekea matatizo haya na kutesekea miaka hii yote? Ni kwa sababu ya umaarufu na faida: Umaarufu na faida yanamngoja mbele, yanamwita, na anaamini tu kwa kupitia bidii yake mwenyewe, matatizo na mapambano ndiyo anaweza kufuata ile njia na hivyo kupata umaarufu na faida. Lazima ateseke matatizo haya kwa sababu ya njia yake ya siku za baadaye, kwa sababu ya raha yake ya siku za baadaye na kwa sababu ya maisha bora. Mnaweza kuniambia—haya maarifa kwa hakika ni nini? Si kanuni za kuishi iliyoingizwa kwa watu na Shetani, iliyofundishwa kwao na Shetani katika kujifunza kwao maarifa? Je, si mawazo ya juu ya maisha yaliyoingizwa kwa mwanadamu na Shetani? Chukua, kwa mfano, mawazo ya watu wakubwa, uadilifu wa watu maarufu ama roho jasiri ya watu mashujaa, ama chukua uungwana na wema wa nguli na wenye panga katika riwaya za kareti. (Ndiyo, ni kweli.) Mawazo haya yanashawishi kizazi kimoja baada ya kingine, na watu wa kila kizazi wanaletwa kuyakubali mawazo haya, kuishi kwa sababu ya mawazo haya na kuyafuata bila kikomo. Hii ndiyo njia, mbinu, ambayo Shetani anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu. Kwa hivyo baada ya Shetani kuwaongoza watu kwa njia hii, inawezekana wao kumwabudu Mungu? (La, haiwezekani.) Je, maarifa na fikira zilizoingizwa kwa mwanadamu na Shetani zina yoyote kuhusu kumwabudu Mungu? Zina fikira yoyote ya ukweli? (La, hazina.) Je, zina uhalisi wowote wa kumcha Mungu na kuepuka uovu. (La, hazina.) Mnaonekana kuongea bila uhakika kidogo, lakini haijalishi. Alimradi mtambue kwamba “umaarufu” na “faida” ni maneno mawili muhimu ambayo Shetani hutumia kuwashawishi watu kuingia njia ya uovu, basi hilo limetosha.

Acha turejelee tena kwa ufupi: Shetani hutumia nini kuendelea kumfungia mwanadamu na kumdhibiti? (Umaarufu na faida.) Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarifa na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kwa ajili ya umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana. Pingu hizi zinabebwa na watu, na hawana nguvu ama ujasiri wa kuzirusha mbali. Kwa hivyo watu kamwe wanatembea kwenda mbele kwa ugumu mkubwa, wakibeba pingu hizi bila kujua. Kwa ajili ya umaarufu huu na faida hii, binadamu humwepuka Mungu na kumsaliti, na wanazidi kuwa waovu zaidi na zaidi. Kwa njia hii, hivyo kizazi kimoja baada ya kingine kinaharibiwa katika umaarufu na faida ya Shetani. Tukiangalia sasa vitendo vya Shetani, nia zake husuda ni za kuchukiza? (Ndiyo.) Pengine leo bado hamwezi kuona kupitia nia husuda za Shetani kwa sababu mnafikiri hakuna maisha bila umaarufu na faida. Mnafikri kwamba, iwapo watu wataacha umaarufu na faida nyuma, basi hawataweza tena kuona njia mbele, hawataweza tena kuona malengo yao, siku zao za baadaye zawa giza, zilizofifia na za ghamu. Lakini, polepole, nyote siku moja mtatambua kwamba umaarufu na faida ni pingu za ajabu ambazo Shetani hutumia kumfunga mwanadamu. Hadi ile siku utakuja kutambua hili, utapinga kabisa udhibiti wa Shetani na utapinga kabisa pingu anazoleta Shetani kukufunga. Wakati utakapofika wa wewe kutaka kutupilia mbali vitu vyote ambavyo Shetani ameingiza ndani yako, utakuwa basi umejiondoa kwa Shetani na pia utachukia kwa kweli vyote ambavyo Shetani amekuletea. Hapo tu ndipo utakuwa na upendo na shauku ya kweli kwa Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp