Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 22

23/05/2020

Tangu kuwepo kwa usimamizi wa Mungu, siku zote amejitolea kabisa katika kutekeleza kazi Yake. Licha ya kuficha nafsi Yake kutoka kwao, siku zote Amekuwa katika upande wa binadamu, akiwafanyia kazi, akionyesha tabia Yake, akiongoza binadamu wote na kiini Chake, na kufanya kazi Yake kwa kila mmoja kupitia nguvu Zake, hekima Yake, na mamlaka Yake, hivyo akiileta Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na sasa Enzi ya Ufalme katika uwepo. Ingawaje Mungu huificha nafsi Yake kutoka kwa binadamu, tabia Yake, uwepo Wake na miliki Yake, na mapenzi Yake kwa binadamu yanafichuliwa bila wasiwasi wowote kwa binadamu kwa minajili ya kuona na kupitia hali hiyo. Kwa maneno mengine, ingawaje binadamu hawawezi kumwona au kumgusa Mungu, tabia na kiini cha Mungu ambacho binadamu wamekuwa wakigusana nacho ni maonyesho kabisa ya Mungu Mwenyewe. Je, hayo si kweli? Licha ya ni mbinu gani au ni kutoka katika mtazamo gani Mungu hufanya kazi Yake, siku zote Anawakaribisha watu kulingana na utambulisho Wake wa kweli, akifanya kile ambacho Anafaa kufanya na kusema kile Anachofaa kusema. Haijalishi ni nafasi gani Mungu anazungumzia kutoka—Anaweza kuwa amesimama kwenye mbingu ya tatu, au amesimama akiwa mwili Wake, au hata kama mtu wa kawaida—siku zote Anaongea kwa binadamu kwa moyo Wake wote na kwa akili Zake zote, bila uongo na bila ufichaji wowote. Wakati Anapotekeleza kazi Yake, Mungu huonyesha neno Lake na tabia Yake, na huonyesha kile Anacho na alicho, bila kuficha chochote. Anamwongoza mwanadamu na maisha Yake na uwepo Wake na miliki yake. Hivi ndivyo binadamu alivyoishi katika Enzi ya Sheria—enzi asilia ya binadamu—akiongozwa na Mungu asiyeonekana na asiyegusika.

Mungu alipata mwili kwa mara ya kwanza baada ya Enzi ya Sheria, hali ya kupata mwili iliyodumu kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Kwa mwanadamu, miaka thelathini na mitatu na nusu ni muda mrefu? (Si mrefu sana.) Kwa sababu urefu wa maisha ya mwanadamu ni mirefu kuliko miaka thelathini na fulani, huu si muda mrefu kwa mwanadamu. Lakini kwa Mungu mwenye mwili, miaka hii thelathini na mitatu na nusu ilikuwa mirefu mno. Aligeuka na kuwa mtu—mtu wa kawaida aliyetekeleza kazi na agizo la Mungu. Hii ilimaanisha kwamba lazima angefanya kazi ambayo mtu wa kawaida asingeweza kufanya, huku akivumilia mateso ambayo binadamu wa kawaida hawezi kuvumilia. Kiwango cha mateso aliyovumilia Bwana Yesu katika Enzi ya Neema, kuanzia mwanzo wa kazi Yake hadi wakati Aliposulubishwa kwenye msalaba, huenda kisiwe ni kitu watu wa leo wangeweza kushuhudia wao binafsi, lakini mnaweza angaa kutambua kiasi kupitia hadithi zilizo kwenye Biblia? Licha ya ni maelezo mangapi yaliyopo kwenye ukweli huu uliorekodiwa, kwa ujumla, kazi ya Mungu katika kipindi hiki kilijaa ugumu na mateso. Kwa mwanadamu aliyepotoka muda wa miaka thelathini na mitatu na nusu si mrefu; mateso kidogo si jambo la kutisha. Lakini kwa Mungu mtakatifu asiye na doa, ambaye lazima avumilie dhambi zote za binadamu, na kula, kulala na kuishi na watenda dhambi, maumivu haya ni mengi mno. Yeye ndiye Muumba, Bwana wa viumbe vyote na Mtawala wa vitu vyote, lakini Alipokuja duniani alilazimika kuvumilia unyanyasaji na ukatili wa wanadamu waliopotoka. Ili kuikamilisha kazi Yake na kuokoa binadamu kutoka kwa taabu, Alilazimika kushutumiwa na binadamu, na kuvumilia dhambi za wanadamu wote. Kiwango cha mateso aliyopitia hakiwezi kwa kweli kueleweka au kutambulika na watu wa kawaida. Mateso haya yanawakilisha nini? Yanawakilisha Mapenzi ya Mungu kwa wanadamu. Yanasimamia udhalilishaji Alioteseka na gharama Aliyolipia kwa sababu ya wokovu wa binadamu, kukomboa dhambi zake, na kukamilisha awamu hii ya kazi Yake. Yanamaanisha binadamu angekombolewa kutoka katika msalaba na Mungu. Hii ndiyo gharama iliyolipwa kwa damu, kwa maisha, gharama ambayo viumbe walioumbwa hawawezi kumudu. Ni kwa sababu Anacho kiini cha Mungu na Amejihami na kile Mungu anacho na alicho, ndiyo maana Anaweza kuvumilia aina hii ya mateso na aina hii ya kazi. Hili ni jambo ambalo hakuna kiumbe aliyeumbwa anaweza kufanya badala Yake. Hii ni kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema na ufunuo wa tabia Yake. Je, hii inafichua chochote kuhusu kile Mungu anacho na alicho? Je, wanadamu wanastahili kuijua?

Katika enzi hiyo, japokuwa mwanadamu hakuiona nafsi ya Mungu, alipokea sadaka ya Mungu dhidi ya dhambi zake na akakombolewa kutoka kwenye msalaba na Mungu. Huenda mwanadamu awe amezoeana na kazi aliyofanya Mungu katika Enzi ya Neema, lakini yupo yeyote aliyezoeana na tabia na mapenzi yalionyeshwa na Mungu katika kipindi hiki? Binadamu anajua tu kuhusu maudhui ya kazi ya Mungu katika enzi tofauti katika vipindi mbalimbali, au anajua hadithi zinazohusiana na Mungu zilizofanyika kwa wakati mmoja na ule Mungu alikuwa akitekeleza kazi Yake. Maelezo haya na hadithi ni kwa ukweli zaidi taarifa fulani tu au hadithi za kumbukumbu kuhusu Mungu, na vyote hivi havina chochote kuhusiana na tabia na kiini cha Mungu. Hivyo haijalishi ni hadithi ngapi watu wanajua kuhusu Mungu, haimaanishi kwamba wanao uelewa wa kina na maarifa kuhusu tabia ya Mungu au kiini Chake. Kama hali ilivyokuwa katika Enzi ya Sheria, ingawaje watu kutoka Enzi ya Neema walikuwa wamepitia mtagusano wa karibu sana na wa kikweli na Mungu wa mwili, maarifa yao kuhusu Mungu na kiini cha Mungu yalikuwa kweli mambo yasiyokuwepo.

Katika Enzi ya Ufalme, Mungu akawa mwili tena, kwa njia sawa na ile Aliyotumia mara ya kwanza. Katika kipindi hiki cha kazi, Mungu angali anaonyesha bila kusita neno Lake, anafanya kazi anayofaa kufanya na kuonyesha kile Anacho na alicho. Wakati huohuo, Anaendelea kuvumilia na kustahili na kutotii na kutojua kwa binadamu. Je, Mungu hafichui kila wakati tabia Yake na kuonyesha mapenzi yake katika kipindi hiki cha kazi pia? Hivyo basi, kuanzia uumbaji wa binadamu hadi sasa, tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki Zake, na mapenzi Yake, siku zote yamekuwa wazi kwa kila mmoja. Mungu hajawahi kuficha kimakusudi kiini Chake, tabia Yake au mapenzi Yake. Ni vile tu mwanadamu hajali kuhusu kile ambacho Mungu anafanya, mapenzi Yake ni yapi—ndio maana uelewa wa binadamu kumhusu Mungu ni finyu mno. Kwa maneno mengine, wakati Mungu anaficha nafsi Yake, Yeye pia Anasimama kando ya mwanadamu kila wakati, akionyesha waziwazi mapenzi Yake, tabia Yake na kiini chake halisi siku zote. Kimsingi, nafsi ya Mungu pia iko wazi kwa watu, lakini kutokana na upofu na kutotii kwa binadamu, siku zote hawawezi kuuona kuonekana kwa Mungu. Hivyo kama hali iko hivyo, basi si kuelewa tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe kunafaa kuwa rahisi mno kwa kila mmoja? Hili ni swali gumu sana kujibu, sivyo? Mnaweza kusema ni rahisi, lakini wakati watu wengine wanatafuta kumjua Mungu, hatimaye hawamjui Yeye au kupata uelewa wa wazi kumhusu Yeye—siku zote ni jambo lililojaa ukungu na lisiloeleweka. Lakini mkisema si rahisi, hilo si sahihi vilevile. Baada ya kuwa mlengwa wa kazi ya Mungu kwa muda mrefu, kila mmoja anafaa, kupitia uzoefu wake, kuwa amepitia kwa kweli mambo mbalimbali na Mungu. Anafaa kuwa amehisi Mungu angaa kwa kiwango fulani katika moyo wake au awali amegongana na Mungu katika kiwango cha kiroho, hivyo anafaa angalau kuwa na ufahamu kiasi tambuzi kuhusu tabia ya Mungu au kupata uelewa fulani kumhusu Yeye. Kuanzia wakati binadamu alianza kumfuata Mungu hadi sasa, mwanadamu amepokea mengi mno, lakini kutokana na sababu za aina zote—uhodari wa kimasikini ya kibinadamu, kutojua, uasi, na nia mbalimbali—wanadamu wamepoteza mambo mengi mno. Je, Mungu hajampatia mwanadamu mali ya kutosha? Ingawaje Mungu huficha nafsi Yake kutoka kwa wanadamu, Anawatosheleza mahitaji yao kwa kile Anacho na alicho, na hata maisha Yake; maarifa ya binadamu ya Mungu hayafai kuwa vile yalivyo tu sasa. Ndiyo maana Nafikiri inahitajika kuwa na ushirika zaidi na nyinyi kuhusu mada ya kazi ya Mungu, kuhusu tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Kusudio ni ili miaka elfu ya utunzaji na fikira ambayo Mungu amemwagia binadamu isije ikaisha bure bilashi, na ili mwanadamu aweze kuelewa kwa dhati na kutambua mapenzi ya Mungu kwake. Ni ili watu waweze kusonga mbele kwenye hatua mpya ya maarifa yao kumhusu Mungu. Itaweza pia kumrudisha Mungu katika nafasi Yake inayofaa kwenye mioyo ya watu yaani kumfanyia Yeye haki.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp