Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 7

20/05/2020

Kunayo Maoni Mengi Yanayohusu Kiwango Ambacho Mungu Hutumia Kuasisi Matokeo ya Binadamu

Kwa sababu kila mmoja anajali matokeo yake, je, mnajua namna ambavyo Mungu huamua matokeo hayo? Na ni kwa njia gani ambayo Mungu huanzisha matokeo ya mtu? Na ni kiwango gani ambacho Mungu hutumia kuasisi matokeo ya mtu? Na wakati ambapo matokeo ya mtu yangali bado hayajaasisiwa, ni nini anachofanya Mungu ili kufichua matokeo haya? Je, yupo anayejua haya? Kama Nilivyosema tu, kunao baadhi ambao tayari wamefanyia uchunguzi neno la Mungu kitambo sana. Watu hao wanatafuta dalili fulani kuhusu matokeo ya mwanadamu, kuhusu kategoria ambazo matokeo haya yamegawanywa, na kuhusu matokeo tofauti yanayosubiria aina tofauti ya watu. Wanataka pia kujua namna neno la Mungu linavyoanzisha matokeo ya binadamu, aina za kiwango ambacho Mungu hutumia, na njia ambayo Yeye huasisi matokeo ya binadamu. Ilhali mwishowe watu hawa hawafanikiwi kupata chochote. Kwa hakika, yapo mambo machache yenye thamani yanayozungumzwa kuhusu suala hili miongoni mwa neno la Mungu. Kwa nini hali iko hivi? Ili mradi matokeo ya binadamu yangali hayajafichuliwa, Mungu hataki kumwambia yeyote kuhusu kile kitakachofanyika mwishowe, wala Hataki kumfahamisha yeyote kuhusu hatima yao kabla ya wakati kufika. Sababu ya kufanya hivi ni kwamba Mungu kufanya hivyo hakutaleta manufaa yoyote kwa binadamu. Sasa hivi, Nataka kuwaambia tu kuhusu namna Mungu huasisi matokeo ya binadamu, kuhusu kanuni Anazotumia katika kazi Yake ili kuyaasisi matokeo ya binadamu, na kuonyesha matokeo haya, pamoja na kiwango Anachotumia ili kuanzisha kama mtu ataweza kuishi au la. Hiki sicho kile ambacho mnajali zaidi kuhusu? Hivyo basi, ni vipi ambavyo watu hufahamu njia ambayo Mungu anaanzisha matokeo ya binadamu? Mlizungumzia kidogo kuhusu suala hili muda mfupi uliopita. Baadhi yenu mlisema kwamba ni swali la kutenda wajibu wao kwa uaminifu, kugharamika kwa ajili ya Mungu; baadhi ya watu walisema kumtii Mungu na kutosheleza Mungu; baadhi ya watu walisema kudhibitiwa na Mungu; na baadhi ya watu walisema kuishi maisha ya hadhi ya chini…. Wakati mnapotia ukweli huu katika matendo, wakati mnapotenda kanuni za kufikiria kwenu, je mnajua kile Mungu anachofikiria? Mmewahi kufikiria kama kuendelea hivi ni kutosheleza nia za Mungu au la? Kama kunatilia maanani kiwango cha Mungu? Kama kunatilia maanani mahitaji ya Mungu? Ninasadiki kwamba watu wengi zaidi hawalifikirii suala hili kwa undani. Wanatumia tu bila kutilia maanani sehemu ya neno la Mungu, au sehemu ya mahubiri, au viwango vya watu fulani wa kiroho ambao wanawaabudu, na kujilazimisha kufanya hivi na vile. Wanasadiki kwamba hii ndiyo njia sahihi, na hivyo basi wanaendelea kuitii, kuifanya, liwalo liwe hatimaye. Baadhi ya watu hufikiria: “Nimesadiki kwa miaka mingi siku zote nimetenda mambo kwa njia hii; nahisi kuwa nimemtosheleza kabisa Mungu; ninahisi pia kuwa nimejifunza mengi kutoka kwa haya. Kwani nimekwishaelewa ukweli mwingi katika kipindi hiki, na nimeelewa mambo mengi ambayo sikuyaelewa awali—hasa, wingi wa fikira na mitazamo yangu imebadilika, maadili ya maisha yangu yamebadilika sana, na ninao uelewa mzuri sana wa ulimwengu huu.” Watu kama hao wanasadiki kwamba haya ni mavuno, na ndiyo matokeo ya mwisho ya kazi ya Mungu kwa binadamu. Kwa maoni yenu, kwa viwango hivi na vitendo vyenu nyote vimewekwa pamoja—je, mnatosheleza nia za Mungu? Baadhi ya watu watasema kwa uhakika wote: “Bila shaka! Tunatenda kulingana na neno la Mungu; tunatenda kulingana na kile ambacho ndugu alihubiri na kushiriki nasi; siku zote tunafanya wajibu wetu, siku zote tunamfuata Mungu, hatujawahi kumwacha Mungu. Hivyo basi tunaweza kusema kwa imani kamili kwamba tunamtosheleza Mungu. Haijalishi ni kiasi kipi tunachoelewa kuhusu nia za Mungu, haijalishi ni vipi tunavyoelewa neno la Mungu, siku zote tumekuwa kwa njia ya kutafuta kuweza kutangamana na Mungu. Kama tutachukua hatua kwa usahihi, na kutenda kwa usahihi, basi matokeo yatakuwa sahihi.” Je, mnafikiria nini kuhusu mtazamo huu? Je, ni kweli? Pengine wapo wale wanaosema: “Sijawahi kufikiria kuhusu mambo haya awali. Mimi nafikiria tu kwamba nikiendelea kutimiza wajibu wangu na kuendelea kutenda kulingana na mahitaji ya neno la Mungu, basi nitasalia. Sijawahi kufikiria swali la kama ninaweza kutosheleza moyo wa Mungu, na sijawahi kufikiria kama ninatimiza kiwango kinachohitajika na Yeye. Kwa sababu Mungu hajawahi kuniambia, wala kunipatia maagizo yoyote kwa uwazi, ninasadiki kwamba mradi tu niendelee kupiga hatua mbele, Mungu atatosheka na Yeye hafai kuwa na mahitaji yoyote ya ziada kwangu mimi.” Je, kusadiki huku ni sahihi? Kulingana na Ninavyojua, njia hii ya kutenda, njia hii ya kufikiria, na mitazamo hii—yote yanakuja na madoido fulani na kiasi kidogo cha upofu. Ninaposema hivi, pengine wapo baadhi yenu mnaohisi kuvunjika moyo: “Yaani upofu? Kama ni ‘upofu,’ basi tumaini letu la wokovu, tumaini letu la kuishini dogo mno, na halina uhakika, hapo ni kweli? Je, wewe kulitamka hivyo lilivyo si sawa na kutumwagilia maji baridi?” Haijalishi kile mnachosadiki, mambo Ninayoyasema na kufanya hayanuii kukufanya ninyi kuhisi kama mnamwagiliwa maji baridi. Badala yake, yananuia kuboresha uelewa wenu wa nia za Mungu, na kuboresha ung’amuzi wenu kuhusu kile ambacho Mungu anafikiria, kile ambacho Mungu anataka kukamilisha ni mtu wa aina gani ambaye Mungu anapenda, nini kinachukiza Mungu, nini Mungu anadharau, ni mtu wa aina gani ambaye Mungu anataka kumpata, na ni mtu wa aina gani ambaye Mungu anatupilia mbali. Yananuia kupatia akili zenu uwazi, kuwasaidia kujua wazi ni kiwango kipi vitendo na fikira za kila mmoja wenu yamepotea kutoka kwa kiwango kinachohitajika na Mungu. Je, inahitajika kuzungumzia mada hii? Kwa sababu Ninajua mmesadiki kwa muda mrefu, na mmesikiliza mahubiri mengi, lakini kwa hakika haya ndiyo mambo yanayokosekana zaidi. Mmerekodi kila ukweli katika daftari zenu, mmerekodi pia kile ambacho nyie wenyewe mnasadiki kibinafsi kuwa muhimu katika akili zenu na katika mioyo yenu. Na mnapanga kukitumia kumridhisha Mungu mnapotenda, kukitumia wakati mnahitaji usaidizi, au kukitumia kupitia nyakati ngumu zilizo mbele yenu, au mnaacha ukweli huu uandamane na ninyi mnapoishi maisha yenu tu. Lakini kulingana na Ninavyojua, iwapo mnatenda tu, namna mnavyotenda hasa si muhimu. Nini, basi, ndicho kitu cha muhimu sana? Ni kwamba wakati unatenda, moyo wako hujua kwa uhakika wote kama kila kitu unachofanya, kila kitendo, ndicho kile anachotaka Mungu au la; kama kila kitu unachofanya ni sahihi au la, kila kitu unachofikiria ni sahihi au la, na matokeo na shabaha katika moyo wako yanatosheleza nia za Mungu au la, kama yanatilia maanani mahitaji ya Mungu au la, na kama Mungu anayaidhinisha au la. Haya ni mambo muhimu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp