Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 6
18/05/2020
Imani za Watu Haziwezi Kubadilishwa na Ukweli
Kunao baadhi ya watu wanaoweza kuvumilia ugumu; wanaweza kulipia bei; tabia yao ya nje ni nzuri sana; wanaheshimika sana; na wanatamaniwa na wengine. Mnafikiria nini: Je, tabia kama hii ya nje inaweza kuchukuliwa kama ya kutia ukweli katika matendo? Mnaweza kusema kwamba mtu huyu anatosheleza nia za Mungu? Kwa nini mara kwa mara watu wanamwona mtu wa aina hii na kufikiria kwamba wao wanamtosheleza Mungu, wanafikiria kwamba wanatembelea njia ile ya kutia ukweli katika matendo, kwamba wanatembea katika njia ya Mungu? Kwa nini baadhi ya watu hufikiria kwa njia hii? Upo ufafanuzi mmoja tu kwa haya. Na ufafanuzi huu ni upi? Sababu ni kwamba kwa kiasi kikubwa cha watu, maswali kama kutia ukweli katika matendo ni nini, kutosheleza Mungu ni nini, ni nini kuwa na uhalisia wa ukweli—maswali haya hayako wazi sana. Hivyo basi kunao baadhi ya watu ambao mara nyingi wanadanganywa na wale ambao kwa nje wanaonekana wa kiroho, wanaonekana wa kilodi, wanaonekana kuwa na taswira za ukuu. Kuhusiana na watu hao wanaoweza kuzungumzia barua na falsafa, na ambao hotuba na vitendo vyao vinaonekana kuwa vyenye kustahili uvutiwaji, wale wanaowatamani hawajawahi kuangalia kiini halisi cha vitendo vyao, kanuni zinazoendesha vitendo vyao, shabaha zao ni nini. Na hawajawahi kuangalia kama watu hawa wanatii Mungu kwa kweli, na kama wao ni watu wanaomcha Mungu kwa kweli na kujiepusha na uovu au la. Hawajawahi kutambua kile kiini halisi cha ubinadamu cha watu hawa. Badala yake, kutoka kwenye hatua ya kwanza ya kujua na kuzoeana nao, hatua kwa hatua wanaanza kuwapenda watu hawa, kuwatukuza watu hawa, na hatimaye watu hawa wanakuwa sanamu zao. Aidha, katika akili za baadhi ya watu, sanamu hizi wanazoziabudu, wanaosadiki wanaweza kuacha familia na kazi zao, na kulipa ile bei kwa juujuu—sanamu hizi ndizo ambazo kwa kweli zinatosheleza Mungu, ndizo zile zinazoweza kupokea kwa kweli matokeo mazuri na hatima nzuri. Katika akili zao, sanamu hizi ndizo wale watu ambao Mungu husifu. Ni nini husababisha watu kuwa na aina hii ya kusadiki? Ni nini kiini halisi cha suala hili? Ni nini matokeo hali hii inaweza kuleta? Hebu na tuzungumzie kwanza suala la kiini chake halisi.
Masuala haya kuhusiana na mitazamo ya watu, vitendo vya watu, ni kanuni gani ambazo watu wanachagua kutenda, na kile ambacho kwa kawaida kila mtu anatilia mkazo, kimsingi haya yote hayahusu mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu hata kidogo. Bila kujali kama watu wanazingatia masuala ya juujuu au yale ya kina, wanazingatia barua na falsafa au uhalisia, watu hawatii yale ambayo wanafaa kutii zaidi, na hawajui kile wanachofaa kujua zaidi. Sababu ya hali hii kuwa hivi ni kwamba watu hawaupendi ukweli kamwe. Hivyo basi, watu hawako radhi kutumia muda na jitihada zao katika kutafuta na kuendeleza kanuni katika neno la Mungu. Badala yake, wanapendelea kutumia njia za mkato, na kujumlisha kile wanachoelewa, kile wanachojua, kuwa vitendo vizuri na tabia nzuri. Muhtasari huu nao huwa shabaha yao ya binafsi ya kufuata, unakuwa ukweli wa kutendwa. Athari ya moja kwa moja ya haya yote ni kwamba watu wanatumia tabia nzuri ya kibinadamu kama kisawazisho cha kutia ukweli katika matendo yao, hali ambayo inatosheleza pia matamanio ya watu ili kupata fadhila na Mungu. Hii inawapa watu mtaji wa kushindania ukweli na kutoa sababu ili kumshawishi Mungu na kuingia katika mzozo Naye. Wakati uo huo, watu wanamweka Mungu kando kwa njia za ufidhuli, na kuiweka ile sanamu ya mioyo yao katika nafasi ya Mungu. Kunayo sababu moja tu ya chanzo cha haya ambayo huwafanya watu kuwa na vitendo wasivyovijua, mitazamo wasiyoijua, au mitazamo na vitendo vya upande mmoja, na leo Nitawaelezea kuhusu haya. Sababu ni kwamba ingawa watu wengi wanaweza kumfuata Mungu, kumwomba Yeye kila siku, na kusoma neno la Mungu kila siku, hawaelewi kwa hakika nia za Mungu. Hiki ndicho chanzo cha tatizo. Kama mtu huelewa moyo wa Mungu, huelewa kile anachopenda Mungu, kile humchukiza Mungu, kile anachotaka Mungu, kile anachokataa Mungu, ni mtu wa aina gani ambaye Mungu humpenda, ni mtu wa aina gani ambaye Mungu hampendi, ni kiwango kipi ambacho Mungu hutumia katika kutoa mahitaji Yake kwa binadamu, ni mtazamo gani ambao Anauchukua katika kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, je, mtu huyu anaweza bado kuwa na mawazo yake ya kibinafsi? Wanaweza tu kuenda na kumwabudu mtu mwingine? Mtu wa kawaida anaweza kuwa sanamu yao? Kama mtu anaelewa nia za Mungu, mtazamo wake ni wenye kirazini zaidi kuliko hapo. Hawatamwabudu kama Mungu kiongozi aliyepotoka kiholela, wala hawataweza, huku wakitembea njia ya kutia ukweli katika matendo, kusadiki kwamba kutii kiholela katika sheria au kanuni chache rahisi ni sawa na kutia ukweli katika matendo.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video