Wimbo wa Kikristo | Unapaswa Kuyaacha Yote Kwa Ajili Ya Ukweli

11/04/2020

Lazima uvumilie mateso kwa ajili ya ukweli,

lazima ujitoe kwa ajili ya ukweli,

lazima uvumilie udhalilishaji kwa ajili ya ukweli,

na kupata ukweli zaidi lazima upate mateso zaidi.

Hili ndilo unalopaswa kufanya. Hili ndilo unalopaswa kufanya.

Msitupilie mbali ukweli kwa ajili

ya maisha ya amani ya familia,

na lazima msiipoteze heshima na uadilifu wa maisha

kwa ajili ya starehe ya muda mfupi.

Unapaswa kufuata yote ambayo ni ya kupendeza na mema,

na unapaswa kufuata njia katika maisha ambayo ni ya maana zaidi.

Kama wewe unaishi maisha ya kishenzi, na wala hufuati malengo yoyote, je,

si huko ni kupoteza maisha Yako?

Ni nini unachoweza kupata kutoka kwa maisha ya aina hii?

Unapaswa kuziacha starehe zote za mwili kwa ajili ya ukweli mmoja,

na hupaswi kutupilia mbali ukweli wote kwa ajili ya starehe ya muda mfupi.

Watu kama hawa hawana uadilifu au heshima;

hakuna maana ya kuwepo kwao!

Unapaswa kuziacha starehe zote za mwili kwa ajili ya ukweli mmoja,

na hupaswi kutupilia mbali ukweli wote kwa ajili ya starehe ya muda mfupi.

Watu kama hawa hawana uadilifu au heshima;

hakuna maana ya kuwepo kwao!

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp