Filamu za Kikristo “Karamu ya Ufalme wa Mbinguni” (Trela)

02/10/2023

Chen Mingde ni kasisi wa Kikatoliki. Anaona kwamba Kanisa Katoliki linazidi kuwa lenye ukiwa na giza, na kwamba hata maaskofu na mapadre wengine wameungana na serikali kwa kujiunga na Kanisa la Kanuni Tatu za Binasi. Jambo hili ni chungu sana na la kusikitisha kwake. Huku akitafuta juu na chini kanisa ambalo lina kazi ya Roho Mtakatifu, bila kutarajia anasikia injili ya Mwenyezi Mungu. Baada ya kusoma maneno mengi ya Mwenyezi Mungu, anatambua kwamba ni sauti ya Mungu na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, na anamkubali kwa furaha. Lakini kwa mshangao wa Chen Mingde, baada ya maaskofu na mapadre wengine kugundua hilo, wanafanya kila wawezalo kumshutumu na kumzuia asimkubali Mwenyezi Mungu. Wanatuma hata watu kuharibu kanisa analolisimamia, kwa kujaribu kumlazimisha atoke kwenye njia ya kweli. Chen Mingde anaona nyuso zinazochukia ukweli, zinazopinga Mungu, za kishetani za maaskofu na mapadre, na anaacha nafasi yake kama kasisi, anaondoka katika kanisa Katoliki, na anaanza kueneza na kushuhudia kwa bidii injili ya ufalme wa Mungu. Anaongoza watu wengi kumgeukia Mwenyezi Mungu na anaanza kujidai sana, mara kwa mara anaonyesha ni kiasi gani amefanya na jinsi amepitia mateso mengi ili kupata pongezi za akina ndugu. Tabia yake ya kiburi inaongezeka zaidi na zaidi—anawakaripia wengine kwa kiburi, anajitungia sheria, na hasikizi ushauri wowote. Matokeo yake, anaishia kukamatwa kwenye mkutano. Anaanza kujitafakari baada ya kupitia mateso ya kikatili ya Chama cha Kikomunisti na kutiwa kasumba. Kupitia ufunuo wa maneno ya Mungu, anaona kwamba yeye ni mwenye kiburi cha ajabu na hana akili, kwamba amekuwa akitafuta nafasi katika mioyo ya wengine, na kwamba yuko kwenye njia ya mpinga Kristo. Bila hukumu, kuadibu, na nidhamu ya Mungu, bila shaka angeangamia kwa kumpinga Mungu. Chen Mingde anajifunza ukweli fulani kupitia hukumu na utakaso wa maneno ya Mungu, na anapata utakaso na mabadiliko fulani katika tabia yake potovu. Anahisi kwamba amepata mengi sana, na kwamba kwa kweli anahudhuria karamu ya ufalme wa mbinguni.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp