Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Mawazo ya Kidini | Dondoo 291

20/07/2020

Kusudi la kukushinda leo ni kukufanya utambue kuwa Mungu ni Mungu wako, na Mungu wa wengine, na muhimu zaidi ni Mungu wa wote wanaompenda, na Mungu wa viumbe wote. Ni Mungu wa Israeli na Mungu wa Misiri. Ni Mungu wa Waingereza na Mungu wa Wamarekani. Si Mungu wa Adamu na Hawa tu, bali pia Mungu wa kizazi cha Adamu na Hawa. Ni Mungu wa kila Kitu mbinguni na duniani. Familia ya Waisraeli na familia zote za Mataifa zimo mikononi mwa Mungu. Hakufanya kazi katika nchi ya Israeli pekee kwa miaka elfu kadhaa na kuzaliwa Uyahudi, ila leo Anashuka Uchina, nchi hii ambapo joka kuu jekundu limejikunja. Ikiwa kuzaliwa Uyahudi kunamfanya Mfalme wa Wayahudi, basi si kushuka kwake miongoni mwenu leo kunamfanya Mungu wenu? Aliwaongoza Waisraeli na alizaliwa Uyahudi na vilevile amezaliwa katika nchi ya Mataifa. Je, kazi Yake yote si ya wanadamu wote Aliowaumba? Je, Anawapenda Waisraeli mara mia moja na kuwachukia Mataifa mara elfu moja? Je, hayo siyo mawazo yenu? Ni ninyi ambao hamtambui Mungu; si kwamba Mungu Hakuwa Mungu wenu. Ni ninyi mnaomkataa Mungu; si kwamba Mungu hapendi kuwa Mungu wenu. Ni nani kati ya walioumbwa hayuko mikononi mwa mwenye Uweza? Kwa kuwashinda leo, je, lengo si kuwafanya mtambue kuwa Mungu ni Mungu wenu? Iwapo bado mnashikilia kuwa Mungu ni Mungu wa Waisraeli tu, na kuendelea kushikilia kuwa nyumba ya Daudi huko Israeli ni asili ya uzao wa Mungu na kuwa hakuna taifa tofauti na Israeli limewezeshwa “kumzaa” Mungu, na hata zaidi kuwa hakuna familia ya Mataifa yenye uwezo wa kupokea kazi ya Yehova—ikiwa bado unafikiria hivi, je, haikufanyi kuwa mshikiliaji wa ukaidi? Usikazie macho Israeli kila wakati. Mungu Yuko hapa miongoni mwenu leo. Vilevile msitazamie mbingu tu. Acheni kutamani Mungu wenu Aliye mbinguni! Mungu ametua miongoni mwenu, basi Anawezaje kuwa mbinguni? Hujaamini katika Mungu kwa muda mrefu, ilhali una mawazo mengi kuhusu Mungu, kiasi kwamba unathubutu kutofikiri hata kwa sekunde moja kuwa Mungu wa Israeli Anaweza kukutunukia na uwepo wake. Wala hamthubutu kufikiri jinsi mnavyoweza kumwona Mungu Akijitokeza binafsi, ikitiliwa maanani jinsi mlivyo wachafu. Aidha hamjawahi kufikiri jinsi Mungu anavyoweza kushuka miongoni mwa Mataifa. Anapaswa kushuka juu ya Mlima Sinai au Mlima wa Mizeituni na kuonekana kwa Waisraeli. Je, si watu wa Mataifa (yaani watu wa nje ya Israeli) ndio walengwa wa chuki Yake? Anawezaje kufanya kazi miongoni mwao? Haya yote ni mawazo yaliyokita mizizi ndani yenu ambayo mmeyakuza kwa miaka mingi. Kusudi la kuwashinda leo ni kuyaharibu haya mawazo yenu. Kwa njia hiyo mmeweza kumwona Mungu akijionyesha Mwenyewe miongoni mwenu—si katika Mlima Sinai au Mlima wa Mizeituni, bali miongoni mwa watu ambao Hajawahi kuwaongoza hapo awali. Baada ya Mungu kufanyia hatua mbili za kazi Yake Israeli, Waisraeli na watu wa Mataifa walishikilia wazo hili: Japo ni kweli Mungu aliumba viumbe wote, yuko radhi kuwa Mungu wa Waisraeli tu, si Mungu wa Mataifa. Waisraeli wanaamini yafuatayo: Mungu anaweza tu kuwa Mungu wetu, sio Mungu wenu Mataifa, na kwa sababu humchi Yehova, Yehova—Mungu wetu—Anawachukia. Zaidi, Wayahudi hao huamini hili: Bwana Yesu alichukua sura yetu Wayahudi na ni Mungu aliye na alama ya Wayahudi. Mungu anafanyia kazi miongoni mwetu. Sura ya Mungu na sura zetu zinafanana; sura zetu na sura ya Mungu zinakaribiana. Bwana Yesu ni Mfalme wetu Wayahudi; watu wa Mataifa hawajawezeshwa kupokea wokovu mkubwa kiasi hicho. Bwana Yesu ni sadaka ya dhambi kwetu Wayahudi. Ni kwa misingi ya hatua hizi mbili za kazi ndipo Waisraeli na Wayahudi walijijengea haya mawazo mengi. Wanamdai Mungu kuwa wao tu, bila kukubali kwamba Mungu vilevile ni Mungu wa Mataifa. Kwa njia hii, Mungu alikuwa pengo katika mioyo ya watu wa Mataifa. Hii ni kwa sababu kila mtu aliamini kuwa Mungu hataki kuwa Mungu wa watu wa Mataifa na kuwa Anawapenda tu Waisraeli—Wateule wake—na Anawapenda Wayahudi hasa wafuasi waliomfuata. Je, wajua kuwa kazi aliyoifanya Yehova na Yesu ilikuwa ni kwa ajili ya uzima wa wanadamu wote? Je, sasa unatambua kuwa Mungu ni wa wale wote waliozaliwa nje ya Israeli? Je, Mungu Hayumo miongoni mwenu leo? Hii haiwezi kuwa ndoto, ama vipi? Je, hamkubali uhalisi huu? Mnathubutu kutoamini au kulifikiria. Licha ya jinsi mnavyolitazama, je, Mungu hayumo miongoni mwenu? Je, bado mnaogopa kuyaamini maneno haya? Kuanzia leo, je, wote walioshindwa, na wale wote wanaotaka kuwa wafuasi wa Mungu, si wateule wa Mungu? Je, nyote mlio wafuasi leo, si wateule nje ya Israeli? Je, nafasi yenu si sawa na ya Waisraeli? Je, hili silo mnalopaswa kutambua? Je, hili si lengo la kazi ya kukushinda? Kwa kuwa mwaweza kumwona Mungu, basi Atakuwa Mungu wenu milele, tangu mwanzo hadi siku za baadaye. Hatawaacha, mradi tu nyinyi nyote mko radhi Kumfuata na kuwa viumbe Wake waaminifu na watiifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp