Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Mawazo ya Kidini | Dondoo 290

13/08/2020

Kwa kuwa mwanadamu anamwamini Mungu, ni sharti afuate kwa ukaribu nyayo Zake, hatua kwa hatua; anapaswa “kumfuata Mwanakondoo popote Aendapo.” Hawa tu ndio watu wanaotafuta njia ya kweli, na wao ndio wanafahamu kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wanaofuata tu nyaraka na mafundisho ya dini kiutumwa ni wale ambao wameondolewa na kazi ya Roho Mtakatifu. Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu angeshikilia ukweli kwamba “Yehova ni Mungu” na “Yesu ni Kristo,” ukweli ambao unazingatiwa kwa kipindi kimoja, basi mwanadamu hataweza kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya, mwanadamu anafaa kufuata bila shaka lolote, na afuate kwa ukaribu. Kwa jinsi hii basi itakuwaje mwanadamu aondolewe na Roho Mtakatifu? Bila kujali kile anachofanya Mungu, kama mwanadamu ana uhakika ni kazi ya Roho Mtakatifu, na kushirikiana katika kazi ya Roho Mtakatifu bila mashaka yoyote, na kujaribu kufikia mahitaji ya Mungu, basi ataadhibiwaje? Kazi ya Mungu kamwe haijasimama, hatua Zake hazijakwama na kabla kukamilisha kazi Yake ya usimamizi, siku zote Mungu amekuwa mwenye kazi nyingi, na kamwe hajasimama. Lakini mwanadamu ni tofauti: Kutokana na kupata kiwango cha chini cha nguvu za Roho Mtakatifu, yeye huchukulia kwamba hakuna chochote kitakachobadilika; baada ya kupata ufahamu kidogo, hajipi msukumo wa kufuata nyayo za kazi mpya ya Mungu; licha ya kwamba ameona kiasi kazi ya Mungu, yeye anamchukulia Mungu kama kifaa, aina fulani ya umbo la sanamu ya mti, na anaamini kwamba Mungu atasalia kuwa hivyo daima kwani hali imekuwa hii tangu hapo awali na hata katika siku zijazo; akiwa amepata ufahamu wa kijuujuu, mwanadamu ni mwenye kiburi hivi kwamba hujisahau na kuanza kutangaza kwa fujo tabia ya Mungu na hali ya Mungu ambayo haipo; na akiwa amejifunga katika hatua moja ya Roho Mtakatifu, pasi kujali ni mtu wa aina gani ambaye anatangaza kazi mpya ya Mungu, mwanadamu huwa haikubali. Hawa ni watu ambao hawawezi kuikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu; ni watu wenye kushikilia ukale sana, na hawawezi kukubali mambo mapya. Watu kama hawa ni watu wanaomwamini Mungu lakini wakati uo huo wanamkataa Mungu. Mwanadamu anaamini kwamba wana wa Israeli walikosea “tu kumuamini Yehova na kukosa kumuamini Yesu,” huku watu wengi wakiiga jukumu ambapo “humwamini Yehova tu na kumkataa Yesu” na “kusubiri kwa hamu kurejea kwa Masihi lakini wanamkataa Masihi ambaye ni Yesu”. Ndiyo maana, basi, watu wengi bado wanaishi chini ya mamlaka ya Shetani baada ya kukubali hatua moja tu ya Roho Mtakatifu na bado hawapokei baraka za Mungu. Je, si hii ni kutokana na uasi wa mwanadamu? Wakristo ulimwenguni kote ambao hawajazingatia kazi mpya ya sasa wote wameshikilia imani kwamba wao ni wenye bahati na kwamba Mungu atawatimizia kila mojawapo ya malengo yao. Lakini hawawezi kueleza mbona Mungu atawapeleka katika mbingu ya tatu na wala hawafahamu jinsi Yesu atakavyokuja juu ya wingu jeupe na kuwachukua, wala kusema kwa uhakika kamili kama kweli Yesu atawasili akiwa juu ya wingu jeupe siku ambayo wanaiwaza. Wote wana wasiwasi, na kukanganywa; wao wenyewe hata hawafahamu kama Mungu atachukua kila mmoja wao, watu wachache sana, wanaotoka katika madhehebu yote. Kazi ambayo Mungu anafanya kwa sasa, enzi ya sasa, mapenzi ya Mungu—ni vitu ambavyo watu hawavifahamu, na hawana cha kufanya bali kusubiri na kuhesabu siku katika vidole vyao. Ni wale tu wanaofuata nyayo za Mwanakondoo hadi mwisho kabisa ndio wanaoweza kufaidi baraka za mwisho, huku wale “watu werevu,” ambao hawawezi kumfuata hadi mwisho ilhali wanaamini wamepata yote, ndio wasiokuwa na uwezo wa kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Wote huamini wao ndio werevu zaidi duniani, na wanasitisha maendeleo ya kazi ya Mungu bila sababu yoyote kabisa, na huonekana kuamini pasi na shaka kwamba Mungu atawachukua mbinguni, wao “wenye uaminifu wa juu zaidi kwa Mungu, humfuata Mungu, na hutii neno la Mungu”. Hata ingawa wana “uaminifu wa hali ya juu” kwa maneno yaliyozungumzwa na Mungu; maneno yao na matendo yao bado hukera kwa sababu wao huipinga kazi ya Roho Mtakatifu, na kufanya uongo na uovu. Wale wasiofuata hadi mwisho kabisa, ambao hawazingatii kazi ya Roho Mtakatifu, na ambao wanashikilia kazi ya zamani hawajakosa tu kupata uaminifu kwa Mungu, bali kwa kinyume, wamekuwa wale wanaompinga Mungu, wamekuwa wale ambao wamekanwa na enzi mpya, na watakaoadhibiwa. Kuna wa kuhurumiwa zaidi kuliko wao? Wengi hata wanaamini kuwa wale wanaokana sheria ya zamani na kukubali kazi mpya hawana dhamiri. Watu hawa, ambao huongea tu kuhusu “dhamiri,” na hawajui kazi ya Roho Mtakatifu, hatimaye watapata kuwa matarajio yao yamekatizwa na dhamiri yao yenyewe. Kazi ya Mungu haizingatii mafundisho, na ingawa ni kazi Yake Mwenyewe, bado Mungu haishikilii. Kile kinachopaswa kukataliwa kinakataliwa, kile kinachopaswa kuondolewa kinaondolewa. Lakini mwanadamu anajiweka kwenye uadui wa Mungu kwa kushikilia sehemu moja ndogo ya kazi ya usimamizi wa Mungu. Si huu ndio upuuzi wa mwanadamu? Si huu ndio ujinga wa mwanadamu? Kadri watu wanakuwa waoga na wenye tahadhari sana kwa sababu wanachelea kutopata baraka za Mungu, ndivyo wanavyopungukiwa zaidi na uwezo wa kupata baraka zaidi, na wa kupata ile baraka ya mwisho. Watu wale wanaoshikilia kiutumwa sheria huwa wanadhihirisha uaminifu wa hali ya juu kwa sheria, na kadri wanavyodhihirisha uaminifu jinsi hiyo kwa sheria, ndivyo wanavyokuwa waasi wanaompinga Mungu. Kwa kuwa sasa ni Enzi ya Ufalme na wala si Enzi ya Sheria, na kazi ya leo haiwezi kulinganishwa na kazi ya zamani wala kazi ya zamani haiwezi kulinganishwa na kazi ya sasa. Kazi ya Mungu imebadilika, na vitendo vya mwanadamu pia vimebadilika; si kushikilia sheria au kuubeba msalaba. Basi, uaminifu wa watu kwa sheria na msalaba hautapata kibali cha Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp