Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Tatizo Zito Sana: Usaliti (2) | Dondoo 362

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Tatizo Zito Sana: Usaliti (2) | Dondoo 362

40 |02/09/2020

Nafsi zote zilizopotoshwa na Shetani zimeshikwa mateka katika miliki ya Shetani. Ni wale tu wanaomwamini Kristo ndio waliotengwa, waliookolewa kutoka katika kambi ya Shetani, na kuletwa ndani ya ufalme wa leo. Watu hawa hawaishi tena chini ya ushawishi wa Shetani. Hata hivyo, asili ya mwanadamu bado imekita mizizi katika mwili wa mwanadamu, yaani, ingawa nafsi zenu zimeokolewa, asili yenu bado ni kama ilivyokuwa awali, na uwezekano kwamba mtanisaliti unabaki kuwa asilimia mia moja. Hii ndiyo sababu kazi Yangu hudumu kwa muda mrefu sana, kwa kuwa asili yenu haiwezi kudhibitiwa kwa urahisi. Sasa, ninyi nyote mnapitia shida kadri ya uwezo wenu mnapotimiza wajibu wenu, ilhali kila mmoja wenu anaweza kunisaliti na kurudi katika miliki ya Shetani, kambini mwake, na kurudia maisha yenu ya zamani—huu ni ukweli usiopingika. Wakati huo, haitawezekana kwenu kudhihirisha chembe ya ubinadamu au mfano wa binadamu, kama mnavyofanya sasa. Katika hali mbaya zaidi, mtaangamizwa, na zaidi ya hayo, mtahukumiwa milele, mwadhibiwe vikali, msizaliwe upya kamwe. Hii ndiyo shida iliyowekwa mbele yenu. Ninawakumbusha kwa njia hii, kwanza, ili kazi Yangu isiwe imekuwa bure, na pili, ili ninyi nyote mweze kuishi katika siku za nuru. Kwa kweli, kama kazi Yangu ni bure si tatizo la muhimu sana. Kilicho cha muhimu sana ni kwamba mnaweza kuwa na maisha yenye furaha na mustakabali mzuri sana. Kazi Yangu ni kazi ya kuziokoa nafsi za watu. Nafsi yako ikianguka mikononi mwa Shetani, mwili wako hautaishi kwa amani. Ikiwa Ninaulinda mwili wako, hakika nafsi yako pia itakuwa chini ya uangalizi Wangu. Nikikuchukia sana, mwili na nafsi yako vitaanguka mikononi mwa Shetani mara moja. Je, unaweza kukisia hali yako wakati huo? Ikiwa, siku moja mtayapuuza maneno Yangu, basi Nitawakabidhi nyote kwa Shetani, ambaye atawatesa sana hadi hasira Yangu itakapoisha kabisa, au Mimi binafsi Nitawaadhibu ninyi wanadamu wasioweza kuokoleka, kwa kuwa mioyo yenu inayonisaliti haitakuwa imewahi kubadilika.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi