Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 301

24/08/2020

Tabia ya upotovu ya mwanadamu inatokana na hali yake ya kupewa sumu na kukanyagwa na Shetani, kutokana na madhara mabaya sana ambayo Shetani ameweka katika mawazo yake, maadili, ufahamu, na hisia. Ni hasa kwa sababu mambo haya ya msingi ya mwanadamu yamepotoshwa na Shetani, na ni tofauti kabisa na jinsi Mungu aliwaumba kwa asili, kwamba mwanadamu humpinga Mungu na haelewi ukweli. Hivyo, mabadiliko katika tabia za mwanadamu lazima yaanze na mabadiliko katika mawazo yake, ufahamu na hisia ambayo yatabadilisha maarifa yake ya Mungu na maarifa yake ya ukweli. Wale waliozaliwa katika nchi potovu zaidi ndio wasiojua zaidi kumhusu kile Mungu Alicho, au kunamaanisha nini kumwamini Mungu. Jinsi watu walivyo wapotovu zaidi, ndivyo wanavyokosa kujua kuwepo kwa Mungu na ndivyo hisia zao na utambuzi huwa duni. Chanzo cha upinzani wa mwanadamu na uasi dhidi ya Mungu ni kupotoshwa kwake na Shetani. Kwa sababu amepotoshwa na Shetani, dhamiri ya mwanadamu imekuwa bila hisia, yeye ni muovu, mawazo yake yamepotoka, na ana mtazamo duni. Kabla ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu kawaida alimfuata Mungu na alitii maneno yake. Alikuwa kawaida mwenye akili timamu na dhamiri, na wa ubinadamu wa kawaida. Baada ya kupotoshwa na Shetani, hali yake ya awali, dhamiri, na ubinadamu vilidhoofika sana na viliharibiwa na shetani. Hivyo, yeye amepoteza utii wake na upendo kwa Mungu. Akili ya mwanadamu imekuwa potovu, tabia yake imekuwa sawa na ile ya mnyama, na uasi wake kwa Mungu kabisa umekuwa wa mara kwa mara na wa kuhuzunisha zaidi. Hata hivyo mwanadamu bado hajui wala kutambua hili, na kwa upofu anapinga na kuasi. Ufunuo wa tabia ya mwanadamu ni udhihirisho wa hisia zake, utambuzi na dhamiri, na kwa sababu hisia yake na utambuzi si timamu, na dhamiri yake imezidi kuwa ndogo zaidi, hivyo tabia yake ni ya uasi dhidi ya Mungu. Kama hisia ya mwanadamu na utambuzi hauwezi kubadilika, basi mabadiliko katika tabia yake hayawezekani, sawa na kuwa baada ya moyo wa Mungu. Kama hisia ya mwanadamu sio timamu, basi hawezi kumhudumia Mungu na hafai kutumiwa na Mungu. “Hisia za Kawaida” inaashiria kutii na kuwa mwaminifu kwa Mungu, kuwa dhahiri kwa Mungu, na kwa kuwa na dhamiri kwa Mungu. Inamaanisha kuwa na moyo mmoja na akili kwa Mungu, na si kwa kumpinga Mungu kwa makusudi. Wale ambao ni wa akili potovu hawako hivi. Tangu mwanadamu aharibiwe na Shetani, ametunga dhana kuhusu Mungu, na yeye hajakuwa na uaminifu au kumtamani Mungu, pia hana dhamiri kwa Mungu. Mwanadamu kwa makusudi anapinga na huweka hukumu juu ya Mungu, na, zaidi ya hapo, anatupa shutuma Kwake nyuma Yake. Mwanadamu anajua vizuri kuwa Yeye ni Mungu, lakini bado humhukumu nyuma ya mgongo wake, hana nia ya kumtii, na hufanya madai ya kipofu na maombi kwa Mungu. Watu wa aina hii—watu walio na akili potovu—hawana uwezo wa kujua tabia zao za kudharauliwa au ya kujuta uasi wao. Kama watu wana uwezo wa kujijua wenyewe, basi wao wamerudisha kiasi kidogo cha akili zao; Zaidi ya vile watu wanavyomuasi Mungu lakini hawajui wenyewe, ndivyo walivyo zaidi wenye akili isiyo timamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp