Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 525

02/10/2020

Mungu humuadibu na kumhukumu mwanadamu kwa sababu inatakiwa vile na kazi Yake, na zaidi ya hayo, kwa sababu yanahitajika na mwanadamu. Mwanadamu anahitaji kuadibiwa na kuhukumiwa, na ni vile tu ndivyo anaweza kufikia upendo wa Mungu. Leo, mmeshawishiwa kikamilifu, lakini wakati mnapokutana na kizingiti kidogo mtakuwa mashakani; kimo chenu bado ni kidogo mno, na nyinyi bado mnahitaji kupata adabu na hukumu hiyo zaidi ili mfikie ufahamu zaidi. Leo, mna heshima kidogo kwa Mungu, na mnamcha Mungu, na mnajua Yeye ni Mungu wa kweli, lakini hamna upendo mkubwa wa Kwake, na bado hamjafikia upendo safi; maarifa yenu ni ya juujuu, na kimo chenu bado hakitoshi. Wakati nyinyi mnapatana na mazingira, bado hamjashuhudia, sehemu ndogo ya kuingia kwenu ndiyo makini, na nyinyi hamjui jinsi ya kufanya mazoezi. Watu wengi ni watazamaji tu na si watendaji; wao humpenda Mungu tu kwa siri katika nyoyo zao, lakini hawana njia ya mazoezi, wala hawafahamu vizuri malengo yao ni nini. Wale ambao wamefanywa wakamilifu hawana tu ubinadamu wa kawaida, lakini wanao ukweli unaozidi vipimo vya dhamiri, na kwamba ni kuu zaidi kuliko viwango ya dhamiri; wao hawatumii tu dhamiri yao kulipia upendo wa Mungu, lakini, zaidi ya hayo, wanajua Mungu, na wameona kwamba Mungu ni mzuri, na Anastahili upendo wa mtu, na kwamba kuna mambo mengi ya upendo katika Mungu ambayo mtu hana budi ila kumpenda Mungu. Upendo wa Mungu wa wale ambao wamekuwa wakamilifu ni kwa ajili ya kutimiza matarajio yao binafsi. Upendo wao ni wa papo hapo, upendo usiouliza chochote, na usio wa kubadilisha na kitu. Wanampenda Mungu kwa sababu ya ufahamu wao Kwake, na sio kwa sababu nyingine. Watu kama hawa hawajali kama Mungu anawapa neema au la, wanaridhishwa na kumridhisha Mungu. Hawabishani na Mungu wapate kitu kwa badala yake, wala kupima upendo wao kwa Mungu na dhamiri: Umenipa, kwa hivyo nitakupenda kwa badala yake; kama Wewe Hunipi, basi sina chochote cha kukupa kwa badala yake. Wale ambao wamekuwa wakamilifu daima huamini kwamba Mungu ni Muumba, kwamba Yeye hufanya kazi Yake juu yao, na kwamba, kwa vile wao wako na fursa hii, na hali, na kufuzu kuwa na uwezo wa kufanywa wakamilifu, azma yao ni kuishi kwa kudhihirisha maisha yaliyo na maana, na wanapaswa kumridhisha Mungu. Ni kama yale aliyopitia Petro: Alipokuwa katika hatua ya udhaifu, alisali kwa Mungu na kusema, “Ee Mungu! Bila kujali wakati au mahali, Unajua kuwa mimi daima hukukumbuka. Haijalishi wakati au mahali, Unajua kuwa mimi nataka kukupenda, lakini kimo changu ni kidogo mno, mimi ni mdhaifu mno na sina nguvu, upendo wangu ni mdogo sana, na uaminifu wangu kwako pia mdogo. Ikilinganishwa na upendo Wako, mimi sifai kuishi. Natamani tu kwamba maisha yangu yasiwe bure, na kwamba nisiweze tu kulipa upendo wako, lakini, kwamba niweze kukukabidhi vyote nilivyo navyo. Kama naweza kukuridhisha, basi kama kiumbe, mimi nitakuwa na amani moyoni, na sitauliza chochote zaidi. Ingawa mimi ni mdhaifu na asiye na nguvu sasa, siwezi kusahau ushauri Wako, na siwezi kusahau upendo Wako. Sasa sifanyi kitu chochote zaidi ya kulipa upendo wako. Ee Mungu, ninahisi kuwa mbaya! Ninawezaje kukupa upendo ulio moyoni mwangu, nitafanyaje yote ninayoweza, na niwe na uwezo wa kutimiza matakwa Yako, na kuwa na uwezo wa kukupa kila nilicho nacho? Unajua udhaifu wa mwanadamu; ninawezaje kuustahili upendo wako? Ee Mungu! Unajua mimi ni wa kimo kidogo, kwamba upendo wangu pia ni mdogo. Jinsi gani niweze kufanya jinsi niwezavyo katika aina hii ya mazingira? Ninajua napaswa kuulipa upendo Wako, najua kwamba napaswa kutoa yote niliyo nayo Kwako, lakini leo kimo changu ni kidogo mno. Naomba kwamba Wewe Unipe nguvu, na kunipa ujasiri, ili niweze kuwa na upendo safi zaidi na kujitoa kwa ajili Yako, na niweze kutoa yote niliyo nayo Kwako; sitaweza kuulipa upendo Wako tu, lakini zaidi nitaweza kupitia adabu Yako, hukumu na majaribu, na hata laana kali zaidi. Umeniruhusu kutazama upendo wako, na sina uwezo wa kutokukupenda Wewe, na ingawa mimi ni mdhaifu na asiye na nguvu leo, inawezekanaje nikusahau Wewe? Upendo wako, adabu na hukumu imenisababisha mimi kujua Wewe, lakini nahisi sina uwezo wa kutimiza upendo Wako kwa hakika, kwa maana Wewe ni Mkuu zaidi. Nitawezaje kutoa yote niliyo nayo kwa Muumba?” Hilo ndilo lilikuwa ombi la Petro, ilhali kimo chake kilikuwa duni. Wakati huu, alijisikia kama kisu kilikuwa kinasukumwa katika moyo wake na alikuwa katika maumivu makali; hakujua cha kufanya katika hali hiyo. Hata hivyo bado aliendelea kuomba: “Ee Mungu! Mwanadamu ni wa kimo cha kitoto, dhamiri yake ni dhaifu, na kitu tu naweza kufikia ni kurejesha upendo Wako. Leo, mimi sijui jinsi ya kukidhi tamaa Yako, au kufanya yote ninayoweza, au kutoa yote niliyonayo, au jinsi ya kukukabidhi yote niliyonayo Kwako. Licha ya Hukumu Yako, licha ya adabu Yako, licha ya yote uliyonipa, licha ya yale Unachukua kutoka kwangu, Niokoe kutokana na aina yoyote ya lalamiko Kwako kutoka kwangu. Mara nyingi, wakati uliniadibu na kunihukumu, nilijinung’unikia, na sikuwa na uwezo wa kufikia usafi, au wa kutimiza matakwa Yako. Ulipaji wangu wa upendo Wako ulizaliwa kutokana na lazima, na katika wakati huu najichukia hata zaidi.” Ilikuwa ni kwa sababu yeye alitaka upendo safi zaidi wa Mungu kwamba Petro aliomba kwa njia hii. Alikuwa akitafuta, na kumwomba, na, zaidi ya hayo, alikuwa akiishtaki nafsi yake, na kukiri dhambi zake kwa Mungu. Alijisikia mdeni kwa Mungu, na aliichukia nafsi yake, ilhali alikuwa pia kwa kiasi fulani mwenye huzuni na asiyeshughulika. Yeye daima aliona hivyo, kama kwamba hakuwa mzuri wa kutosha kwa ajili ya matakwa ya Mungu, na kuwa hakuweza kufanya bora zaidi. Katika hali kama hiyo, Petro bado alifuata imani ya Ayubu. Aliona jinsi imani ya Ayubu ilivyokuwa kubwa, kwa maana Ayubu aliona kwamba yote yalifanywa na Mungu, na ilikuwa ni ya asili ya Mungu kuchukua kila kitu kutoka kwake, na kwamba Mungu angempa yeyote ambaye Angependa kumpa—hivyo ndivyo ilivyokuwa tabia ya haki ya Mungu. Ayubu hakuwa na malalamiko, na bado aliweza kumtukuza Mungu. Petro pia alijua mwenyewe, na katika moyo wake akaomba, “Leo mimi siwezi kuridhika na kulipa upendo Wako kwa kutumia dhamiri yangu na kwa upendo wowote ninaokupa, kwa sababu mawazo yangu yamepotoshwa sana, na kwa sababu mimi sina uwezo wa kukuona Wewe kama Muumba. Kwa sababu mimi bado sifai kukupenda, lazima kukamilisha uwezo wa kutoa yote niliyonayo Kwako, na hivyo nitafanya kwa hiari. Ni lazima nijue yote Uliyofanya, na sina budi, na mimi lazima nitazame upendo Wako, na kuwa na uwezo wa kusema sifa Zako, na kutaja jina lako takatifu, ili Uweze kupata utukufu mwingi kupitia kwangu. Mimi niko tayari kusimama imara katika ushuhuda huu Kwako. Ee Mungu! Upendo wako ni wenye thamani na wa kupendeza; jinsi gani mimi ningetaka kuishi katika mikono ya yule mwovu? Je, mimi sikuumbwa na Wewe? Ningewezaje kuishi chini ya miliki ya Shetani? Ningependa nafsi yangu nzima iishi chini ya adabu Yako. Sitaki kuishi chini ya miliki ya yule mwovu. Kama mimi ninaweza kutakaswa, na ninaweza kutoa yote niliyonayo Kwako, mimi niko tayari kutoa mwili wangu na akili kwa hukumu na adabu Yako, kwa maana mimi nachukizwa na Shetani, na sina nia ya kuishi chini ya uwanja wake. Kupitia hukumu Yako kwangu, umenionyesha tabia Yako ya haki; Nina furaha, na sina malalamiko hata kidogo. Kama mimi nina uwezo wa kutekeleza jukumu la kiumbe, mimi niko tayari kuwa maisha yangu yote yaambatane na hukumu Yako, kwa njia ambayo mimi nitapata kujua tabia Yako ya haki, na kujiondolea ushawishi wa yule mwovu.” Petro aliomba hivyo kila mara, na daima alitaka hivyo, na aliufikia ulimwengu wa juu. Hakuweza tu kuulipa upendo wa Mungu, lakini, la muhimu zaidi, yeye alitimiza wajibu wake kama kiumbe. Hakutuhumiwa tu na dhamiri yake, lakini alikuwa pia na uwezo wa kuvuka viwango vya dhamiri. Maombi yake yaliendelea kwenda mbele za Mungu, hivyo kwamba matarajio yake yalikuwa milele juu, na upendo wake kwa Mungu ulikuwa milele mkuu. Ingawa yeye alipitia maumivu makali, bado hakusahau kumpenda Mungu, na bado alitaka kufikia uwezo wa kuelewa mapenzi ya Mungu. Kwa maombi yake yalitamkwa maneno yafuatayo: Sijatimiza chochote zaidi ya ulipaji wa upendo wako. Sijatoa ushuhuda Kwako mbele ya Shetani, sijajiweka huru mwenyewe kutokana na ushawishi wa Shetani, na bado naishi miongoni mwa umbo la mwili. Ningependa kutumia upendo wangu kumshinda shetani, na kumwaibisha, na hivyo kuridhisha hamu Yako. Ningependa kujitoa mzima kwako, nisijitoe hata kidogo kwa Shetani, kwani Shetani ni adui Wako. Zaidi ya alivyoendelea kwa njia hii, ndivyo alivyozidi kusongeshwa, na ndivyo ujuzi wake wa mambo haya ulivyozidi kukua. Bila kujua, alitambua kwamba anapaswa kujikwamua kutokana na ushawishi wa Shetani, na kujirudisha mwenyewe kabisa kwa Mungu. Huo ndio ulimwengu alioufikia. Alikuwa anauzidi kwa mbali ushawishi wa Shetani, na kujitoa mwenyewe kwenye raha na starehe za mwili, na alikuwa tayari kupitia kwa kina zaidi adabu zote na hukumu ya Mungu. Alisema, “Hata ingawa ninaishi katika adabu Yako, na huku kukiwa na hukumu Yako, bila kujali ugumu unaohusiana na maisha, bado mimi sina nia ya kuishi chini ya miliki ya Shetani, sina nia ya kuteseka na hila za Shetani. Mimi nina furaha kuishi kwenye laana Yako, na ninapata uchungu kwa kuishi katika baraka za shetani. Nakupenda kwa kuishi katika hukumu Yako, na hii huniletea furaha kuu. Adabu Yako na hukumu ni yenye uadilifu na takatifu; ni vyema ukinitakasa, na hata zaidi kuniokoa. Ninapenda niishi maisha yangu yote katika hukumu Yako na kuwa chini ya uchungaji Wako. Sina nia ya kuishi chini ya mamlaka ya Shetani hata kwa dakika moja; Napenda kutakaswa na Wewe, kuteseka kwa ugumu wa maisha, na sina nia ya kutumiwa na kuhadaiwa na shetani. Mimi, kiumbe hiki, nafaa nitumike na Wewe, nijazwe na Wewe, nihukumiwe na Wewe, na kuadibiwa na Wewe. Nafaa hata nipokee laana kutoka Kwako. Moyo wangu hufurahi wakati Uko tayari kunibariki, kwa maana nimeona upendo Wako. Wewe ni Muumba, na mimi ni kiumbe: Sifai kukusaliti Wewe na kuishi chini ya himaya ya Shetani, wala sifai kutumiwa na Shetani. Mimi nafaa kuwa farasi wako, au ng’ombe, badala ya kuishi kwa ajili ya Shetani. Afadhali niishi katika adabu Yako, bila neema ya kimwili, na hii itanipa raha na starehe hata kama ningepoteza neema Yako. Ingawa neema Yako haiko nami, mimi nafurahia kuadibiwa na kuhukumiwa na Wewe; Hii ndiyo baraka Yako nzuri zaidi, neema Yako kuu. Ingawa Wewe daima ni Mkuu na mwenye ghadhabu kwangu, bado mimi siwezi kukuacha, bado sina uwezo wa kukupenda vya kutosha. Ningependelea kuishi katika nyumba Yako, Ningependa kulaaniwa, kuadibiwa, na kuchapwa na Wewe, na sina nia ya kuishi chini ya himaya ya Shetani, wala mimi sina nia ya kukimbilia na kushughulika kwa ajili ya mwili tu, zaidi ya hayo siko tayari kuishi kwa ajili ya mwili.” Upendo wa Petro ulikuwa upendo safi. Huu ni ujuzi wa kufanywa mkamilifu, na ni ulimwengu wa juu wa kufanywa mkamilifu, na hakuna maisha yaliyo na maana zaidi ya haya. Alikubali adabu ya Mungu na hukumu, aliipenda tabia ya Mungu ya haki, na hakuna jambo kuhusu Petro lililokuwa la thamani zaidi ya hili. Alisema, “Shetani ananipa starehe za mwili, lakini mimi sithamini hayo. Adabu ya Mungu na hukumu inakuja juu yangu—na katika hili mimi nimeneemeka, katika hili mimi ninapata starehe, na katika hili mimi nimebarikiwa. Kama si kwa hukumu Yake, mimi singeweza kumpenda Mungu, bado ningeishi chini ya himaya ya Shetani, bado ningedhibitiwa nayo, na ningekuwa naamuriwa nayo. Kama ingekuwa vile, singewahi kuwa binadamu wa kweli, kwa maana singeweza kumtosheleza Mungu, na singejitoa kikamilifu kwa Mungu. Japokuwa Mungu Hanibariki, na kuniacha bila faraja ndani yangu, kana kwamba moto mkuu unachoma ndani yangu, na hakuna amani au furaha, na hata ingawa adabu na nidhamu ya Mungu kamwe iko na mimi, katika adabu ya Mungu na hukumu ninao uwezo wa kuona tabia Yake ya haki. Mimi hupata furaha katika hili; hakuna kitu cha thamani zaidi au cha maana zaidi ya hili katika maisha. Ingawa ulinzi Wake na huduma vimekuwa adabu kali, hukumu, laana na mipigo, bado mimi hupata starehe katika mambo haya, kwani yanaweza kunitakasa bora zaidi, yanaweza kunibadilisha, yanaweza kunileta karibu na Mungu zaidi, yanaweza kufanya niweze kumpenda Mungu zaidi, na yanaweza kufanya upendo wangu kwa Mungu uwe safi zaidi. Hii inanifanya niwe na uwezo wa kutimiza wajibu wangu kama kiumbe, na inanichukua mbele za Mungu na kuniweka mbali na ushawishi wa Shetani, ili nisije tena nikamtumikia Shetani. Wakati siishi chini ya himaya ya Shetani, na ninaweza kutoa kila kitu nilicho nacho na kile ninachoweza kwa ajili ya Mungu, bila kubakisha chochote—hapo ndipo nitakuwa nimeridhika kikamilifu. Ni adabu ya Mungu na hukumu Yake ndiyo iliyoniokoa, na maisha yangu hayawezi kutengwa kutoka kwenye adabu na hukumu ya Mungu. Maisha yangu hapa duniani yamo chini ya himaya ya Shetani, na isingekuwa huduma na ulinzi na adabu ya Mungu na hukumu Yake, ningeliishi daima chini ya himaya ya Shetani, na, zaidi ya hayo, singekuwa na nafasi au njia ya kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Ni wakati tu ambapo adabu ya Mungu na hukumu kamwe hainiachi, ndio nitakapokuwa na uwezo wa kutakaswa na Mungu. Ni kwa maneno makali na tabia ya haki ya Mungu, na hukumu kuu ya Mungu, ndipo nimepata ulinzi mkuu, na kuishi katika mwanga, na kupokea baraka za Mungu. Kuwa na uwezo wa kutakaswa, na kujiweka huru kutokana na Shetani, na kuishi chini ya utawala wa Mungu—hii ndiyo baraka kubwa zaidi katika maisha yangu leo.” Huu ndio ulimwengu wa juu zaidi aliopitia Petro.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp