Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu | Dondoo 519

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu | Dondoo 519

56 |04/09/2020

Mwanadamu humtambua Mungu, anapata kujijua mwenyewe, anajitoa katika tabia yake potovu, na kutafuta kukua katika maisha yote kwa ajili ya kumjua Mungu. Ukitafuta kujijua mwenyewe tu na kujishughulisha tu na tabia yako potovu, na huna ufahamu ni kazi gani Mungu Anafanya kwa mwanadamu, kuhusu jinsi wokovu Wake ulivyo mkuu, au jinsi unavyomjua Mungu na kushuhudia matendo ya Mungu, basi matukio yako hayana maana. Iwapo unafikiri kuwa kuweza kuuweka ukweli katika matendo, na kuwa na uwezo wa kuvumilia kunamaanisha maisha ya mtu yamekua, basi hii ina maana kuwa bado huelewi maana kamili ya maisha, na huelewi kusudi la Mungu la Kufanya kazi kwa mwanadamu. Siku moja, ukiwa katika makanisa ya kidini, miongoni mwa wanachama wa Kanisa la Toba au Kanisa la Uzima, utakutana na watu wengi wenye imani ambao maombi yao yana maono, na wanaohisi kuguzwa na walio na maneno ya kuwaongoza katika kuendelea kwao na maisha. La ziada, kwa mambo mengi wanaweza kuvumilia, na kujitelekeza wenyewe, bila kuongozwa na mwili. Wakati huo, huwezi kujua tofauti: Utaamini kuwa kila wanachofanya ni sawa, kuwa ni udhihirisho wa kawaida wa maisha, lakini huruma ilioje kuwa jina wanaloamini ndani yake si sahihi. Je imani kama hizi si pumbavu? Ni kwa nini inasemekana kuwa watu wengi hawana maisha? Ni kwa sababu hawamjui Mungu, na hivyo inasemekana kuwa hawana Mungu, na hawana uhai. Iwapo imani yako kwa Mungu imefikia kiwango fulani ambapo unaweza kwa kikamilifu kuyafahamu matendo ya Mungu, ukweli wa Mungu, na kila hatua ya kazi ya Mungu, basi umejawa na ukweli. Iwapo hujui kazi na tabia ya Mungu, basi uzoefu wako bado ni wa chini. Jinsi Yesu Aliifanya hatua ile ya kazi Yake, jinsi hatua hii inavyoendelezwa, jinsi Mungu Alifanya kazi Yake katika enzi ya Neema na ni kazi ipi iliyofanywa, ni kazi ipi inafanyika katika hatua hii—iwapo huna ufahamu kamilifu wa mambo haya, basi hutawahi kuondokewa na wasiwasi na utakuwa na shaka. Iwapo, baada ya kipindi cha uzoefu, wewe unaweza kujua kazi inayofanywa na Mungu na kila hatua ya kazi ya Mungu, na unao ufahamu mkuu wa malengo ya maneno ya Mungu, na ni kwa nini maneno mengi yaliyozungumzwa na Yeye hayajatimika bado, basi unaweza kutulia na kuendelea katika safari iliyo mbele yako, ukiwa huru kutokana na wasiwasi na kusafishwa. Mnapaswa kuona kile Mungu anatumia wingi wa kazi Yake. Yeye hutumia maneno Anayozungumza, akimsafisha mwanadamu na kuyabadilisha mawazo ya mwanadamu kupitia maneno mengi tofauti. Mateso yote ambayo mmestahimili, kusafishwa kwote ambako mmepitia, kushughulikiwa ambako mmekukubali ndani yenu, kupata nuru ambako mmeona—yote yamefanikishwa kutumia maneno Aliyozungumza Mungu. Ni kwa sababu ya nini ndio mwanadamu anamfuata Mungu. Ni kwa sababu ya maneno ya Mungu! Maneno ya Mungu ni yenye mafumbo makuu, na yanaweza kuuguza moyo wa mwanadamu, kufunua vitu vilivyo ndani ya moyo wa mwanadamu, yanaweza kumfanya ajue vitu vilivyotendeka zamani, na kumruhusu kuona katika siku za usoni. Na kwa hivyo mwanadamu anavumilia mateso kwa sababu ya maneno ya Mungu, na anafanywa mkamilifu kwa sababu ya maneno ya Mungu, na ni baada ya hapo tu ndipo mwanadamu anamfuata Mungu. Anachostahili kufanya mwanadamu katika hatua hii ni kukubali maneno ya Mungu, na haijalishi kama amefanywa mkamilifu, au kusafishwa, kilicho cha muhimu ni maneno ya Mungu; hii ni kazi ya Mungu, na ni maono ambayo mwanadamu lazima ayajue leo hii.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi