Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 508

16/09/2020

Watu wakijipata chini ya ushawishi wa Shetani, basi hawana upendo kwa Mungu ndani yao, na maono, upendo na azimio yao ya awali yamepotea. Watu walikuwa wakihisi kwamba walifaa kuteseka kwa ajili ya Mungu, lakini leo wanafikiri kwamba ni aibu na hawakosi malalamiko. Hii ni kazi ya Shetani; inaonyesha kwamba mwanadamu amemilikiwa na Shetani. Ukikabiliwa na hali hii ni sharti uombe, na uibadilishe haraka uwezavyo—hii itakulinda dhidi ya mashambulizi ya Shetani. Ni wakati wa usafishaji mkali ambapo mwanadamu anaweza kujipata chini ya ushawishi wa Shetani kwa urahisi zaidi—kwa hivyo ni jinsi gani unapaswa kumpenda Mungu wakati wa usafishaji kama huu? Unapaswa kuyaita mapenzi yako, kuuweka moyo wako mbele ya Mungu na kutenga muda wako wa mwisho Kwake. Haijalishi jinsi gani Mungu hukusafisha, unafaa kuwa na uwezo wa kutia ukweli katika vitendo kutimiza mapenzi ya Mungu, na unafaa kujitolea kumtafuta Mungu na kutafuta mawasiliano. Nyakati kama hizi, zaidi unavyokaa tu, ndivyo utakuwa mtu hasi zaidi, na ndivyo itakuwa rahisi zaidi kwako kurudi nyuma. Wakati ambapo inakulazimu kutenda kazi yako, ingawa huitendi vyema, unafanya kila unachoweza, na unaifanya kwa kutumia tu upendo wako wa Mungu; bila kujali kile ambacho wengine husema—ikiwa wanasema umetenda vyema, au kwamba umetenda vibaya—motisha zako ni sahihi, na wewe sio wa kujidai, kwani unatenda kwa niaba ya Mungu. Wengine wanapokuelewa vibaya, unaweza kumwomba Mungu na kusema: “Ee Mungu! Siombi kwamba wengine wanivumilie au kunitendea vyema, wala kwamba wanielewe au kunikubali. Naomba tu kwamba niweze kukupenda moyoni mwangu, kwamba niwe na utulivu moyoni mwangu, na kwamba dhamiri yangu ni safi. Siombi kwamba wengine wanisifu, au kuniheshimu, ninatafuta tu kukuridhisha kutoka moyoni mwangu, ninatenda wajibu wangu kwa kufanya kila ninachoweza, na ingawa mimi ni mpumbavu na mjinga, na mwenye ubora wa tabia duni, na kipofu, najua kwamba Unapendeza, na niko tayari kukutolea kila ninacho.” Punde tu unapoomba kwa jinsi hii, upendo wako kwa Mungu huibuka, na unahisi utulivu zaidi moyoni mwako. Hili ndilo linalomaanishwa na kutenda upendo wa Mungu. Unavyopata uzoefu, utashindwa mara mbili na kufaulu mara moja, au pia ushindwe mara tano na kufaulu mara mbili, na unavyopata uzoefu kwa jinsi hii, ni katikati ya kushindwa tu ndipo utaweza kuona uzuri wa Mungu na kugundua kinachokosa ndani yako. Unapopitia hali kama hizi tena, unafaa kujitahadharisha, kutuliza mwendo wako, na kuomba mara nyingi zaidi. Polepole utakuza uwezo wa kushinda katika hali kama hizi. Hilo linapofanyika, maombi yako yamekuwa yenye matokeo yanayotarajiwa. Unapoona umefanikiwa wakati huu, utafurahishwa ndani yako, na unapoomba utaweza kumhisi Mungu, na kuhisi kwamba uwepo wa Roho Mtakatifu haujakutoka—na ni hapo tu ndipo utajua jinsi Mungu hufanya kazi ndani yako. Kutenda kwa njia hii kutakupa njia inayoelekea katika uzoefu. Usipoutia ukweli katika vitendo, basi utakuwa bila uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako. Lakini ukiutia ukweli katika vitendo unapokumbana na mambo jinsi yalivyo, basi, ingawa unaumia ndani, Roho Mtakatifu atakuwa nawe baadaye, utaweza kuhisi uwepo wa Mungu unapoomba, utakuwa na nguvu ya kutenda maneno ya Mungu, na wakati wa mawasiliano na ndugu zako, hakutakuwa na chochote kinachosumbua dhamiri yako, na utahisi amani, na kwa jinsi hii, utaweza kufunua yale ambayo umefanya. Bila kujali yale ambayo wengine husema, utaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, hutazuiliwa na wengine, hutashindwa na lolote—na katika hili, utaonyesha kwamba kutenda kwako maneno ya Mungu kumekuwa kwa matokeo yanayotarajiwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kuwa na Upendo wa Kweli

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp