Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 500

16/09/2020

Mungu hutumia uhalisi na ujio wa ukweli kuwafanya watu kuwa wakamilifu; maneno ya Mungu hutimiza sehemu ya kuwafanya watu kuwa wakamilifu, na hii ni kazi ya uelekezaji na kufungua njia. Hivi ni kusema, katika maneno ya Mungu lazima utafute njia ya matendo, na lazima utafute ufahamu wa maono. Kwa kuyaelewa haya mambo, mwanadamu atakuwa na njia na maono anapotenda, na kuweza kupata nuru kupitia maneno ya Mungu, ataweza kuelewa kuwa haya mambo hutoka kwa Mungu, na kuweza kutambua mengi. Baada ya kuelewa, lazima aingie katika uhalisia mara moja, na kutumia maneno ya Mungu kumridhisha Mungu katika maisha yake halisi. Mungu atakuelekeza katika mambo yote, na Atakupa njia ya matendo, na kukufanya uhisi kuwa Mungu anapendeza sana, na kukufanya uone kuwa kila hatua ya kazi ya Mungu ndani yako ni kwa ajili ya kukufanya uwe mkamilifu. Ukitaka kuona upendo wa Mungu, ukitaka kwa kweli kupitia katika upendo wa Mungu, hivyo ni lazima uzame katika uhalisi, ni lazima uzame katika maisha halisi, na kuona kwamba kila kitu afanyacho Mungu ni upendo, na wokovu, na kwamba watu waweze kuacha kile ambacho si safi, na kwa ajili ya kusafisha mambo ndani yao ambayo hayana uwezo wa kuridhisha mapenzi ya Mungu. Mungu hutumia maneno kumkimu mwanadamu na wakati huo huo kutengeneza mazingira katika maisha halisi ambayo huwaruhusu watu kupitia, na kama watu watakula na kunywa maneno mengi ya Mungu, basi wanapoyaweka katika vitendo, wanaweza kutatua matatizo yote katika maisha yao kwa kutumia maneno mengi ya Mungu. Hivi ni kusema, lazima uwe na maneno ya Mungu ili kuzama katika uhalisi; kama huli na hunywi maneno ya Mungu, na huna kazi ya Mungu, basi hutakuwa na njia katika maisha halisi. Kama hujawahi kushiriki maneno ya Mungu, basi utashangaa wakati mambo yatakapokutokea. Unajua kumpenda Mungu pekee, na huwezi kutofautisha chochote, na huna njia ya vitendo; umevurugika na kuchanganyikiwa, na mara nyingine unaamini kuwa kwa kuuridhisha mwili unamridhisha Mungu—yote ambayo ni matokeo ya kutokula na kunywa maneno ya Mungu. Hivi ni kusema, kama huna usaidizi wa maneno ya Mungu, na kutapatapa tu katika uhalisi, basi kimsingi huna uwezo wa kupata njia ya vitendo. Watu kama hawa hawaelewi maana ya kumwamini Mungu, au hata kuelewa kumpenda Mungu kunamaanisha nini. Ikiwa, kwa kutumia nuru na uelekezaji wa maneno ya Mungu, unaomba mara kwa mara, na kuchunguza, na kutafuta, ambayo kwayo unagundua kile unachofaa kuweka katika vitendo, kutafuta fursa ya Kazi ya Roho Mtakatifu, unashirikiana na Mungu kwa kweli, na huvurugiki na kuchanganyikiwa, basi utakuwa na njia katika maisha halisi, na kumridhisha Mungu kwa kweli. Ukimridhisha Mungu, ndani yako kutakuwa na uelekezaji wa Mungu, na hasa kubarikiwa na Mungu, ambako kutakupa hisia za furaha: utahisi hasa umeheshimika kwa kuwa umemridhisha Mungu, na utahisi umeng’aa kwa ndani, na katika moyo wako utakuwa wazi na mwenye amani, dhamiri yako itafarijiwa na haitakuwa na shutuma, utahisi furaha ndani yako uwaonapo ndugu na dada zako. Hii ndio maana ya kufurahia upendo wa Mungu, na kwa kweli huku ndiko kumfurahia Mungu. Furaha ya watu kutokana na upendo wa Mungu inapatikana kwa kupitia matukio: kwa kupitia matatizo, na kupitia uwekaji ukweli katika vitendo, wanapata baraka za Mungu. Kama unasema tu Mungu anakupenda, kuwa Mungu amelipa gharama kubwa kwa watu, kuwa Mungu ameongea maneno mengi kwa uvumilivu na huruma, na Huokoa watu kila mara, utamkaji wako wa maneno haya ni upande mmoja tu wa kumfurahia Mungu. Kufurahia kwa kweli zaidi kungekuwa ni kwa watu kuweka ukweli katika vitendo katika maisha yako halisi, ambapo baadaye watakuwa na amani na kuwa wazi moyoni mwao, watahisi wakiwa wamesisimka, ndani yao, na kuwa Mungu anapendeza sana. Utahisi kuwa gharama uliyoilipa inafaa sana. Baada ya kulipa gharama kubwa katika juhudi zako, utang’aa hasa ndani yako: utahisi kuwa unafurahia upendo wa Mungu kwa kweli, na kuelewa kuwa Mungu amefanya Kazi ya kuwaokoa watu, kuwa kuwasafisha watu ni kwa ajili ya kuwatakasa, na kuwa Mungu anawajaribu watu ili kupima kama wanampenda kwa kweli. Kama utaweka ukweli katika vitendo kwa njia hii, basi hatua kwa hatua utakuza ufahamu wazi zaidi wa kazi ya Mungu, na wakati huo utakuwa unahisi kuwa maneno ya Mungu mbele yako yatakuwa wazi kabisa. Kama unaweza kuelewa waziwazi ukweli mwingi, utahisi kuwa maswala yote ni rahisi kuweka katika vitendo, kuwa utashinda swala hili, na kushinda jaribio hilo, na utaona kuwa hakuna chochote kigumu kwako, ambacho kitakufanya kuwa mtu huru na aliyekombolewa. Kufikia hapa utakuwa ukifurahia upendo wa Mungu, na upendo wa Mungu wa kweli utakuwa umekushukia. Mungu hubariki wale ambao wana maono, ambao wana ukweli, ambao wana ufahamu, na ambao wanampenda kwa kweli. Watu wakitaka kuuona upendo wa Mungu, lazima waweke ukweli katika vitendo katika maisha halisi, lazima wawe tayari kuvumilia mateso na kuacha hicho wanachokipenda na kumridhisha Mungu, mbali na machozi kwenye macho yao, lazima waweze kuuridhisha moyo wa Mungu. Kwa njia hii, kwa hakika Mungu atakubariki, na ukivumilia matatizo kama haya, yatafuatiwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kupitia kwa maisha halisi, na kutokana na kupitia maneno ya Mungu, watu wanaweza kuona upendo wa Mungu, na wanaweza kumpenda Mungu kwa ukweli ikiwa tu wameuonja upendo wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp