Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 464

02/09/2020

Binadamu anayo imani Kwangu Mimi lakini hawezi kunitolea ushuhuda Mimi; kabla ya Mimi Mwenyewe kujitambulisha, binadamu hawezi kunitolea ushuhuda Mimi. Binadamu anaona tu kwamba Mimi ninazidi viumbe na binadamu wote wengine watakatifu, na anaona kwamba kazi ninayofanya haiwezi kufanywa na binadamu wengine. Kwa hivyo, kuanzia kwa Wayahudi hadi kwa binadamu wa siku ya leo, yeyote ambaye ameyaona matendo Yangu yenye utukufu anajawa tu na uchu wa kudadisi mengi kuhusu Mimi, ilhali hakuna kinywa cha kiumbe kimoja ambacho kingeweza kunitolea ushuhuda. Baba Yangu tu ndiye Aliyenitolea ushuhuda Mimi; Alinitengenezea njia Mimi miongoni mwa viumbe vyote. Kwani, haijalishi ni namna gani Nilivyofanya kazi, binadamu asingewahi kujua Mimi ndimi Bwana wa viumbe, binadamu anajua tu kuchukua, na hajui kuwa na imani ndani Yangu Mimi kwa sababu ya kazi Yangu Mimi. Binadamu ananijua Mimi tu kwa sababu Mimi sina hatia wala si mtenda dhambi kwa vyovyote vile, kwa sababu Ninaweza kufafanua mafumbo mengi, kwa sababu Mimi niko juu ya wengine wote, au kwa sababu binadamu amefaidi pakubwa kutoka Kwangu. Ilhali wachache ndio wanaoamini kwamba Mimi ndimi Bwana wa viumbe. Hii ndiyo maana Ninasema ya kwamba binadamu hajui ni kwa nini anayo imani Kwangu mimi; hajui kusudio au umuhimu wa kuwa na imani Kwangu mimi. Uhalisia wa binadamu umekosekana, kiasi cha kwamba karibu hana thamani tena ya kuweza kunitolea ushuhuda Mimi. Unayo imani ya kweli ndogo sana na umefaidi kidogo sana, kwa hivyo una ushuhuda mdogo. Aidha, unaelewa mambo machache sana na unapungukiwa na mambo mengi sana kiasi kwamba hufai kushuhudia matendo Yangu. Azimio lako kwa hakika linaeleweka, lakini je una hakika kwamba utaweza kunitolea ushuhuda kwa ufanisi kuhusu hali halisi ya Mungu? Kile ambacho umepitia na kuona kinazidi kile ambacho watakatifu na manabii wengine wa awali walivyoshuhudia, lakini je unaweza kutoa ushuhuda mkubwa zaidi kuliko maneno ya hawa watakatifu na manabii waliotangulia? Kile Ninachokupa wewe sasa kinazidi kile Nilichompa Musa na ni kikubwa zaidi kuliko kile nilichompa Daudi, kwa hivyo vilevile Ninakuomba ushuhuda wako uzidi ule wa Musa na kwamba maneno yako yawe makubwa zaidi kuliko yale ya Daudi. Ninakupa vyote hivi mara mia moja, kwa hivyo vilevile ninakuomba nawe unilipe tena vivyo hivyo. Lazima ujue kwamba Mimi Ndimi ninayempa maisha mwanadamu, na kwamba wewe ndiwe unayepokea maisha kutoka Kwangu na lazima unitolee ushuhuda Mimi. Huu ndio wajibu wako, ambao Ninashusha kwako na ambao unastahili kunifanyia Mimi. Nimekupa utukufu Wangu wote, na kukupatia maisha ambayo watu wateule, Waisraeli, hawakuwahi kupokea. Bila kukosea, unastahili kunitolea ushuhuda, na kuutoa ujana wako kwa ajili Yangu na kuyatoa maisha yako. Yeyote yule ninayempa Mimi utukufu Wangu ataweza kunitolea Mimi ushuhuda na kunipatia maisha yake. Haya yote yametabiriwa mapema. Ni utajiri wako wewe ambao Ninawekea utukufu Wangu kwako wewe na wajibu wako ni kuutolea ushuhuda utukufu Wangu. Kama unaniamini tu Mimi ili kupata utajiri, basi kazi Yangu haitakuwa yenye umuhimu, na hutakuwa unatimiza wajibu wako. Waisraeli waliona tu huruma Yangu, upendo Wangu na ukubwa Wangu nao Wayahudi walitoa tu ushuhuda wa subira Yangu na ukombozi Wangu. Waliona kazi kidogo sana ya Roho Yangu; huenda ikawa kwamba kiwango chao cha uelewa kilikuwa sehemu ndogo sana ya ile ambayo wewe umesikia na kuona. Kile ulichoona kinazidi hata kile ambacho makuhani wakuu waliona miongoni mwao. Siku hii, ukweli ambao umeelewa umezidi wao; kile ambacho umeona siku hii kinazidi kile kilichoonwa kwenye Enzi ya Sheria pamoja na Enzi ya Neema na kile ambacho umepitia kinazidi hata kile ambacho Musa na Eliya walipitia. Kile ambacho Waisraeli walielewa kilikuwa tu sheria ya Yehova na kile ambacho waliona kilikuwa tu ni mgongo wake Yehova; kile ambacho Wayahudi walielewa kilikuwa tu ukombozi wa Yesu, kile walichopokea kilikuwa neema waliyowekewa na Yesu, na kile walichoona kilikuwa ni taswira ya Yesu ndani ya nyumba ya Wayahudi. Kile utakachoona siku hii ni utukufu wa Yehova, ukombozi wa Yesu na matendo Yangu yote ya siku hii. Umesikia pia maneno ya Roho Yangu, hekima Yangu teule, na ukaja kujua kuhusu maajabu Yangu, na umeweza kujifunza kuhusu tabia Yangu. Nimeweza pia kukuambia kuhusu mpango Wangu wa usimamizi. Kile ambacho umeona si tu Mungu mwenye upendo na huruma, lakini yule aliyejawa na haki. Umeiona kazi Yangu ya maajabu na kujua kwamba Nimejawa na hasira na adhama. Aidha, umejua kwamba Niliwahi kuzishusha hasira Zangu katika nyumba ya Israeli, na kwamba leo hii, umeshushiwa wewe. Umeelewa zaidi kuhusu mafumbo Yangu kule mbinguni kuliko vile alivyoelewa Isaya pamoja na Yohana; unajua zaidi kuhusu uzuri Wangu na kustahiwa Kwangu kuliko watakatifu wote wa vizazi viilivyotangulia. Kile ulichopokea si ukweli Wangu tu, njia Yangu, maisha Yangu, lakini maono na ufunuo ambavyo ni vikubwa zaidi kuliko vile vya Yohana. Umeelewa mafumbo mengine mengi zaidi na pia umeona sura Yangu kamili; umekubali mengi kuhusu hukumu Yangu na tabia Yangu ya haki. Kwa hivyo, ingawaje ulizaliwa kwenye siku za mwisho, uelewa wako ni ule wa siku za awali na za kale; umeweza pia kupitia ni nini kilichomo kwenye siku hii, na kile kilichotimizwa na mkono Wangu. Kile Ninachokuomba kinawezekana, kwani kile Nilichokupa ni kingi mno na ni mengi ambayo umeona Kwangu mimi. Kwa hivyo, Ninakuomba kunishuhudia Mimi kama vile watakatifu wa awali walivyofanya na hili ndilo tamanio tu la moyo Wangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unajua Nini Kuhusu Imani?

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp