Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 422
10/10/2020
Kazi na neno la Mungu vinanuiwa kusababisha badiliko katika tabia yenu; lengo Lake si tu kuwafanya muelewe ama mjue kazi na neno Lake. Hilo halitoshi. Wewe ni mtu aliye na uwezo wa kufahamu, kwa hivyo hupaswi kuona ugumu kuelewa neno la Mungu, kwa sababu maneno mengi ya Mungu yameandikwa katika lugha ya mwanadamu, na Anazungumza kwa uwazi sana. Kwa mfano, unaweza kabisa kujifunza ni nini ambacho Mungu angetaka uelewe na utende; hili ni jambo ambalo mtu wa kawaida aliye na uwezo wa kufahamu anapaswa kuweza kufanya. Hasa, maneno ambayo Mungu anasema katika hatua ya sasa ni ya wazi na dhahiri zaidi, na Mungu anaonyesha mambo mengi ambayo watu hawajayazingatia, na vilvile kila aina ya hali za binadamu. Maneno Yake yanajumuisha yote na ni dhahiri kama mwanga wa mwezi kamili. Kwa hivyo sasa, watu wanaelewa masuala mengi, lakini bado kuna kitu kinachokosa—watu kuweka neno Lake katika vitendo. Ni lazima watu wapitie vipengele vyote vya ukweli kwa utondoti, na wauchunguze na kuutafuta kwa kina zaidi, badala ya kusubiri tu kufyonza chochote wanachopewa; vinginevyo wanakuwa kupe tu. Wanajua neno la Mungu, lakini hawaliweki katika vitendo. Mtu wa aina hii hapendi ukweli na mwishowe ataondolewa. Ili kuwa kama Petro wa miaka ya tisini, hili linamaanisha kwamba nyote mnapaswa kutenda neno la Mungu, muingie kwa kweli katika yale mnayoyapitia na mpate nuru hata zaidi na kubwa zaidi katika ushirikiano wenu na Mungu, ambao utakuwa wa msaada unaozidi daima kwa maisha yenu wenyewe. Ikiwa mmesoma maneno mengi ya Mungu lakini mnaelewa tu maana ya maandiko na hamna maarifa ya moja kwa moja ya neno la Mungu kupitia uzoefu wenu halisi, basi hutajua neno la Mungu. Kwa kadiri inavyokuhusu, neno la Mungu si uzima, bali tu nyaraka zisizovutia. Na ikiwa unaishi tu kwa kufuata nyaraka zisizovutia, basi huwezi kuelewa asili ya neno la Mungu wala hutaelewa mapenzi Yake. Ni wakati tu ambapo unapitia neno Lake katika matukio yako halisi ndipo maana ya kiroho ya neno la Mungu itafichuka kwako, na ni kupitia uzoefu tu ndiyo unaweza kuelewa maana ya kiroho ya ukweli mwingi na ufungue siri za neno la Mungu. Usipouweka katika vitendo, basi bila kujali jinsi neno Lake lilivyo dhahiri, yote uliyoelewa ni nyaraka na mafundisho matupu tu, ambayo yamekuwa kanuni za kidini kwako. Je, Mafarisayo hawakufanya hivi? Mkitenda na kupitia neno la Mungu, linakuwa la utendaji kwenu; usipotafuta kulitenda, basi neno la Mungu kwako ni hekaya ya mbinguni ya tatu tu. Kwa kweli, mchakato wa kumwamini Mungu ni mchakato wa ninyi kupitia neno Lake na vilevile kupatwa na Yeye, ama kuzungumza dhahiri zaidi, kumwamini Mungu ni kuwa na maarifa na ufahamu wa neno Lake na kupitia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake; huu ndio uhalisi wa ninyi kumwamini Mungu. Ikiwa mnamwamini Mungu na mnatumai kupata uzima wa milele bila kutafuta kutenda neno la Mungu kama kitu kilicho ndani yenu, basi ninyi ni wapumbavu. Hii itakuwa sawa na kwenda katika karamu na kuangalia tu chakula na kujua na kuweza kuvikariri vitu vitamu bila kuvionja kwa kweli. Je, mtu kama huyu si mpumbavu?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video