Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 418

01/09/2020

Maarifa ya msingi kuhusu kuomba:

1. Usiseme kijinga chochote kinachokuja kwenye akili. Lazima kuwe na mzigo ndani ya moyo wako, ambalo ni kusema, lazima uwe na lengo wakati unapoomba.

2. Sala lazima iwe na maneno ya Mungu; lazima itegemezwe kwa maneno ya Mungu.

3. Wakati unapoomba, ni sharti usitumie tena masuala yaliyopitwa na wakati. Unapaswa kuzingatia maneno ya sasa ya Mungu, na unapoomba, umwambie Mungu mawazo yako ya ndani kabisa.

4. Sala ya kikundi inapaswa kulenga kiini, ambacho lazima kiwe kazi ya Roho Mtakatifu leo.

5. Watu wote lazima wajifunze jinsi ya kuombea kitu. Hii pia ni njia ya kuyadhukuru mapenzi ya Mungu.

Maisha ya maombi ya kibinafsi yanategemea kuelewa umuhimu wa sala na maarifa ya msingi ya sala. Lazima mwanadamu aombee dosari zake mara kwa mara katika maisha yake ya kila siku, omba uwe na mabadiliko katika tabia yako maishani, na omba kwa msingi wa maarifa yako ya maneno ya Mungu. Kila mtu anapaswa kuanzisha maisha yake ya maombi, anapaswa kuombea maarifa kutegemea maneno ya Mungu, anapaswa kuomba ili kutafuta maarifa ya kazi ya Mungu. Weka hali zako za kweli mbele ya Mungu, na uwe wa vitendo, na usitilie maanani mbinu; la muhimu ni kupata maarifa ya kweli, na kupata maneno ya Mungu kwa kweli. Yeyote anayefuatilia kuingia katika maisha ya kiroho lazima aweze kuomba kwa njia nyingi. Sala ya kimya, kutafakari maneno ya Mungu, kuja kuijua kazi ya Mungu, na kadhalika—kazi hii inayolengwa ya kuwasiliana kwa karibu, ni ili kutimiza kuingia katika maisha ya kawaida ya kiroho, kuifanya hali yako mwenyewe mbele za Mungu iwe bora zaidi, na kusababisha maendeleo makubwa zaidi katika maisha yako. Kwa kifupi, yote unayoyafanya—kama ni kula na kunywa maneno ya Mungu, au kuomba kimya au kutangaza kwa sauti—ni ili kuona wazi maneno ya Mungu, na kazi Yake, na kile Anachotaka kutimiza ndani yako. La muhimu zaidi, ni ili kufikia viwango ambavyo Mungu anahitaji na kuyapeleka maisha yako kwa kiwango kinachofuata. Kiwango cha chini zaidi ambacho Mungu anahitaji kwa watu ni kwamba waweze kufungua mioyo yao Kwake. Ikiwa mwanadamu atautoa moyo wake wa kweli kwa Mungu na kusema kile kilicho ndani ya moyo wake kwa Mungu, basi Mungu yuko tayari kufanya kazi ndani ya mwanadamu; Mungu hataki moyo wa mwanadamu uliopotoka, lakini moyo wake ulio safi na mwaminifu. Ikiwa mwanadamu hasemi yaliyo moyoni mwake kwa Mungu kwa kweli, basi Mungu haugusi moyo wa mwanadamu, au kufanya kazi ndani yake. Hivyo, jambo muhimu sana kuhusu kuomba ni kusema maneno ya moyo wako wa kweli kwa Mungu, kumwambia Mungu kuhusu dosari zako au tabia ya kuasi na kujifungua kabisa kwa Mungu. Wakati huo tu ndipo Mungu atakuwa na hamu ya sala zako; la sivyo, basi Mungu atauficha uso Wake kutoka kwako. Kigezo cha chini kabisa cha sala ni kwamba lazima uweze kuuweka moyo wako kwa amani mbele za Mungu, na hupaswi kuondoka kwa Mungu. Pengine, wakati huu, hujapata mtazamo mpya au wa juu, lakini lazima utumie sala ili mambo yaendelee kama yalivyo—huwezi kurudi nyuma. Hili ndilo jambo dogo zaidi ambalo unapaswa kutimiza. Ikiwa huwezi kufanikisha hata hili, basi inathibitisha kwamba maisha yako ya kiroho hayajaingia katika njia sahihi; kwa hiyo, huwezi kushikilia maono yako ya mwanzo, na kuondolea imani kwa Mungu, na uamuzi wako hatimaye hutoweka. Kuingia kwako katika maisha ya kiroho kunadhihirishwa na iwapo sala zako zimeingia katika njia sahihi au la. Watu wote lazima waingie katika uhalisi huu, lazima wafanye kazi ya kujifunza wenyewe kwa kufahamu katika sala, sio kusubiri kwa kukaa tu, lakini kwa ufahamu watafute kuguswa na Roho Mtakatifu. Wakati huo tu ndipo watakuwa watu wanaomtafuta Mungu kwa kweli.

Unapoanza kuomba, lazima uwe mwenye uhalisi, na usitake kufanya kupita kiasi; huwezi kufanya madai ya ubadhirifu, ukitumaini kwamba mara tu utakapofungua kinywa chako utaguswa na Roho Mtakatifu, utapata nuru na mwangaza, na kupewa neema nyingi. Hilo haliwezekani—Mungu hafanyi mambo yaliyo ya rohoni. Mungu hutimiza sala za watu kwa wakati Wake mwenyewe na wakati mwingine Yeye hujaribu imani yako kuona kama wewe ni mwaminifu mbele Zake. Unapoomba lazima uwe na imani, uvumilivu, na azimio. Watu wengi wanapoanza kujifunza kuomba, hawahisi kuwa wameguswa na Roho Mtakatifu na hivyo huvunjika moyo. Hili halikubaliki! Lazima uwe na nia ya kutobadili msimamo, lazima ulenge kuhisi mguso wa Roho Mtakatifu, na kutafuta na kuchunguza. Wakati mwingine, njia unayofuata ni ile isiyo sahihi; wakati mwingine, misukumo na dhana zako haviwezi kusimama imara mbele za Mungu, na hivyo Roho wa Mungu hakusisimui; vivyo pia kuna nyakati ambapo Mungu huangalia kama wewe ni mwaminifu au la. Kwa kifupi, lazima ujitahidi zaidi katika kujifunza. Ikiwa utatambua kuwa njia unayoifuata ni ya kuacha maadili, unaweza kubadilisha jinsi unavyoomba. Maadamu unatafuta kwa kweli, na unatamani kupokea, basi Roho Mtakatifu atakuingiza kwenye ukweli huu. Wakati mwingine unasali kwa moyo wa ukweli lakini huhisi kama umeguswa hasa. Katika nyakati kama hizi lazima utegemee imani yako, na uamini kwamba Mungu anayaangalia maombi yako; lazima uwe na uvumilivu katika sala zako.

Lazima uwe mwaminifu, na lazima uombe ili uondoe ujanja ndani ya moyo wako. Unapotumia maombi ili kujitakasa wakati wowote inapohitajika, na kuyatumia ili uguswe na Roho wa Mungu, tabia yako itabadilika polepole. Maisha ya kweli ya kiroho ni maisha ya sala, na ni maisha ambayo yanaguswa na Roho Mtakatifu. Mchakato wa kuguswa na Roho Mtakatifu ni mchakato wa kubadilisha tabia ya mwanadamu. Maisha ambayo hayajaguswa na Roho Mtakatifu si maisha ya kiroho, bado ni ibada ya kidini; wale tu ambao huguswa na Roho Mtakatifu mara kwa mara, na wamepewa nuru na kuangazwa na Roho Mtakatifu, ndio watu ambao wameingia katika maisha ya kiroho. Tabia ya mwanadamu hubadilika kwa uthabiti wakati anapoomba, na kadri anavyosisimuliwa na Roho wa Mungu, ndivyo anavyozidi kuwa hai na mtiifu. Kwa hiyo, pia, moyo wake utatakaswa polepole, baada ya hapo tabia yake itabadilika polepole. Hayo ndiyo matokeo ya sala ya kweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Desturi ya Sala

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp