Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 394
20/08/2020
Kosa kubwa sana la binadamu kuwa na imani katika Mungu ni kwamba imani yake ni ya maneno tu, na Mungu hayupo popote katika maisha yake ya utendaji. Watu wote, kwa kweli, wanaamini kuwepo kwa Mungu, lakini Mungu si sehemu ya maisha yao ya kila siku. Maombi mengi kwa Mungu hutoka katika kinywa cha mtu, lakini Mungu amepewa nafasi ndogo sana katika moyo wake, na hivyo Mungu humjaribu binadamu tena na tena. Kwa vile mtu ni mchafu, Mungu hana budi ila kumjaribu mtu, ili aweze kuona aibu na kisha aje kujitambua mwenyewe katika majaribu. La sivyo, mwanadamu atageuka mwana wa malaika mkuu, na kuzidi kuwa mfisadi. Wakati wa imani ya mtu katika Mungu, nia nyingi na malengo ya kibinafsi hutupwa mbali anavyotakaswa na Mungu bila kukoma. La sivyo, hakuna mwanadamu anayeweza kutumiwa na Mungu, na Mungu hana njia ya kufanya ndani ya mtu kazi anayopaswa kufanya. Mungu kwanza humtakasa mwanadamu. Katika mchakato huu, mtu anaweza kuja kujijua mwenyewe na Mungu huenda akambadilisha mwanadamu. Ni baada ya haya ndipo Mungu anaweza kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kwa njia hii pekee ndio moyo wa binadamu unaweza kumgeukia Mungu kwa ukamilifu. Kwa hivyo, kumwamini Mungu si rahisi jinsi mwanadamu anaweza kuona. Mungu anavyoona, ukiwa tu na ufahamu lakini huna neno Lake kama uhai; ikiwa wewe unazingatia tu maarifa yako mwenyewe lakini huwezi kutenda ukweli au kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, basi hii ni dhihirisho kwamba huna moyo wa upendo kwa Mungu, na inaonyesha kwamba moyo wako si mali ya Mungu. Kuja kumjua Mungu kwa kumwamini; hili ndilo lengo la mwisho na ambalo mwanadamu atatafuta. Lazima ufanye juhudi ya kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ili yaweze kuonekana katika matendo yako. Kama unayo maarifa ya mafundisho ya dini pekee, basi imani yako kwa Mungu itakuwa kazi bure. Kama wewe utatenda pia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake basi imani yako inaweza kuchukuliwa kuwa kamili na kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Katika njia hii, wanadamu wengi wanaweza kusema wana maarifa mengi, lakini katika wakati wao wa kufa, macho yao hujawa machozi, nao hujichukia wenyewe kwa kuharibu maisha yao yote na kuishi maisha yasiyo na mazao hadi uzeeni. Walikuwa tu na ufahamu lakini kamwe hawakuwa na nafasi ya kumtukuza Mungu. Walitumia maisha yao yote kwa mapigano na kusafiri huku na kule, lakini saa ya kufa kwao, kuna majuto katika nyoyo zao. Katika saa yao ya kufa tu ndipo watu wengi huja katika fahamu zao kamili na kutambua maana ya maisha. Je, si huku ni kuchelewa mno? Kwa nini usichukue nafasi hii na kutafuta ukweli unaoupenda? Kwa nini usubiri hadi kesho? Iwapo katika maisha huwezi kuteseka kwa ajili ya ukweli au kutafuta kuupata, inaweza kuwa kwamba unataka kujuta katika saa yako ya kufa? Ikiwa hivyo, basi kwa nini umwamini Mungu? Kwa kweli, kuna mambo mengi ambayo mtu, iwapo ataweka juhudi kidogo tu, anaweza kuweka ukweli katika vitendo na hivyo kumridhisha Mungu. Moyo wa binadamu daima umepagawa na mapepo na kwa hivyo hawezi kutenda mambo kwa ajili ya Mungu. Badala yake, yeye daima yumo katika safari ya huku na kule kwa sababu ya mwili, na hafaidiki na chochote mwishowe. Ni kwa sababu hizi ndio mtu hupata matatizo ya mara kwa mara na mateso. Je, haya sio mateso ya Shetani? Je, huu sio ufisadi wa mwili? Hufai kumdanganya Mungu kwa maneno ya mdomo. Badala yake, lazima uchukue hatua inayoonekana. Usijidanganye; ni nini maana katika hilo? Ni faida gani utakayopata kutokana na kuishi kwa ajili ya mwili wako na kufanya bidii kwa ajili ya umaarufu na mali ya dunia?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video