Filamu za Kikristo | Ni Vigezo Vipi vya Kuingia Kwenye Ufalme wa Mbinguni? (Dondoo Teule)

07/09/2018

Kuhusiana na ni mtu aina gani anayeweza kuingia kwenye ufalme wa mbinguni, Bwana Yesu alisema, "ila yule atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni" (Mathayo 7:21). Kwa hivyo ni mtu aina gani hasa anayefanya mapenzi ya Baba wa mbinguni? Watu wengi husadiki kwamba wale wanaofuata mfano wa Paulo na kufanya kazi kwa uangalifu na bidii nyingi kwa ajili ya Bwana ndio wanaofanya mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kisha kunao wale wanaosadiki kwamba wale ambao wanampenda Mungu pekee kwa moyo wao wote, akili na nafsi, ambao hawatendi dhambi tena na wamefikia utakaso, ndio wanaofanya mapenzi ya Baba wa mbinguni. Hivyo ni nani aliye sahihi na nani asiye sahihi kutokana na mitazamo hii miwili? Tafadhali tazama pande zote mbili zikishiriki katika majadiliano makali!

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp