Wimbo wa Kikristo | Njooni Sayuni Kwa Sifa (Muziki wa Akapela)

07/10/2020

Sifa zimekuja Sayuni.

Sifa zimekuja Sayuni.

Sifa zimekuja Sayuni.

Sifa zimekuja Sayuni!

Sifa zimekuja Sayuni na makazi ya Mungu yameonekana.

Jina tukufu takatifu linasifiwa na watu wote, na linaenea.

Ah, Mwenyezi Mungu!

Mkuu wa ulimwengu, Kristo wa siku za mwisho—

Yeye ni Jua linalong’aa,

na Ameinuka juu ya Mlima Sayuni ulio na uadhimu na mzuri kabisa katika ulimwengu mzima …

Mwenyezi Mungu!

Sisi tunakushangilia; tunacheza ngoma na kuimba.

Kweli Wewe ni Mkombozi wetu, Mfalme mkubwa wa ulimwengu!

Umetengeneza kundi la washindi,

na kutimiza mpango wa usimamizi wa Mungu.

Watu wote wataelekea kwa mlima huu.

Watu wote watapiga magoti mbele ya kiti cha enzi!

Wewe ndiye Mungu mmoja wa kweli na wa pekee na Unastahili utukufu na heshima.

Utukufu wote, sifa, na mamlaka yawe kwa kiti cha enzi!

Chemchemi ya maisha hutiririka kutoka kwenye kiti cha enzi,

ikinyunyizia na kuwalisha watu wa Mungu.

Maisha hubadilika kila siku;

nuru mpya na ufunuo hutufuata sisi,

daima vikitupatia utambuzi mpya wa Mungu.

Kuwa yakini kwa Mungu kupitia uzoefu;

maneno Yake daima huonekana,

yakionekana kwa wale ambao ni waadilifu.

Kwa kweli sisi tumebarikiwa kupita kiasi!

Kuwa ana kwa ana na Mungu kila siku,

kuwasiliana na Mungu katika kila kitu,

na kumpa Mungu mamlaka katika kila kitu.

Kwa umakini sisi tunatafakari neno la Mungu,

mioyo yetu ni mitulivu katika Mungu,

na hivyo sisi tunakuja mbele za Mungu ambapo tunapokea nuru Yake.

Katika maisha yetu ya kila siku,

matendo, maneno, mawazo, na fikira,

tunaishi ndani ya neno la Mungu,

na daima tunao utambuzi.

Neno la Mungu linapenya;

mambo yaliyofichwa ndani kwa ghafula huonekana moja baada ya nyingine.

Ushirika na Mungu hauwezi kucheleweshwa;

mawazo na fikira huonyeshwa kwa uwazi na Mungu.

Kwa kila muda tunaishi mbele ya kiti cha Kristo ambapo sisi hupitia hukumu.

Kila eneo la miili yetu linamilikiwa na Shetani.

Leo, hekalu la Mungu lazima litakaswe ili Apate ukuu Wake tena.

Ili kumilikiwa kabisa na Mungu,

ni lazima tupitie vita vya kufa kupona.

Ni wakati tu nafsi zetu za zamani zimesulubiwa

ndipo maisha ya kufufuliwa ya Kristo yatatawala kwa ukuu.

Sasa Roho Mtakatifu Anafanya shambulio katika kila pembe yetu

ili kuzindua vita vya kurudisha!

Mradi tuko tayari kujinyima wenyewe

na radhi kushirikiana na Mungu,

Mungu kwa wakati wowote Ataangaza na kututakasa ndani zetu,

na kurudisha upya yale ambayo Shetani amemiliki,

ili tuweze kukamilishwa na Mungu haraka iwezekanavyo.

Usipoteze muda, na daima uishi ndani ya neno la Mungu.

Jengwa pamoja na watakatifu, letwa katika ufalme,

na uingie katika utukufu na Mungu.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp