Wimbo wa Kikristo | Upendo wa Mungu Hutuleta Karibu Zaidi Pamoja

07/08/2018

Ingawa tumetengwa na maziwa na milima isiyohesabika,

sisi tuko pamoja, bila mipaka kati yetu,

tukiwa na rangi tofauti za ngozi na kuzungumza ndimi tofauti.

Kwa sababu maneno ya Mwenyezi Mungu yanatuita,

tunainulia juu mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.

I

Kuna wale wakongwe, wenye mvi kila pahali,

na wale vijana, werevu na wanaong’aa.

Mkono kwa mkono, bega kwa bega,

tunatembea pamoja katika upepo na mvua, tukitiana moyo katika dhiki.

Kwa akili moja tunatimiza wajibu wetu.

Mioyo yetu imeungana, tunakuwa wandani maishani.

Upendo wa Mungu hutuleta karibu zaidi pamoja.

II

Maneno ya Mungu ndiyo chemichemi ya kisima cha maji yaishiyo.

Tukifurahia maneno ya Mungu, mioyo yetu imejaa utamu.

Kuadibu kwa maneno Yake, hukumu ya maneno Yake,

hutakasa tabia zetu potovu.

Ni kwa kupogolewa na kushughulikiwa pekee ndiyo tunakuwa na umbo la binadamu.

Katika uhasi na udhaifu, tunasaidiana.

Tuko pamoja katika dhiki.

Tukitoa ushahidi katika ushahidi, tunamshinda Shetani.

Tunaepa giza na kuishi katika mwangaza.

Tukiwa waaminifu na watiifu, sisi ni dhihirisho la utukufu wa Mungu.

Tunajua haki na uzuri wa Mungu.

Tunapitia njia nyingi zisizohesabika ambazo Mungu anatupenda sisi.

Tukiwa tumekumbatiwa kifuani mwa Mungu, maisha yetu duniani ni kama yalivyo mbinguni.

Ni pamoja na Mungu pekee ndio kuna upendo, ni pamoja na upendo ndiyo kuna familia.

Wote wanaompenda Mungu ni familia moja.

Tunakuja pamoja katika upendo wa Mungu.

Maneno ya Mungu yako pamoja nasi tunapokua.

Tukiishi katika ufalme wa kupendeza,

tunamwabudu Mwenyezi Mungu milele na milele.

La la la … La la la … La la la …

tunamwabudu Mwenyezi Mungu milele na milele,

tunamwabudu Mwenyezi Mungu milele na milele,

tunamwabudu Mwenyezi Mungu milele na milele.

kutoka kwa Mfuate Mwanakondoo na Imba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp