Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Tabia ya Mungu na Kile Anacho na Alicho | Dondoo 240

09/11/2020

Leo, sababu Nimewaongoza hadi hapa, Nimefanya mipango ya kufaa, na Nina malengo Yangu Mwenyewe. Ningewaeleza kuyahusu leo, mngeweza kweli kuyajua? Nayajua vizuri mawazo ya akili ya mwanadamu na matakwa ya moyo wa mwanadamu: Nani hajawahi kutafuta njia ya kujitoa mwenyewe? Nani hajawahi fikiria matarajio yake mwenyewe? Lakini hata kama mwanadamu ana akili tajiri na wa mche nani aliweza kutabiri kwamba, kufuatia enzi, sasa kungekuwa kulivyo? Hili kweli ni tunda la juhudi zako binafsi? Haya ni malipo ya kazi yako ya bidii? Hii ndiyo picha nzuri iliyoonwa na akili yako? Nisingewaongoza wanadamu wote, nani angeweza kujitenga na mipango Yangu na kupata njia nyingine ya kutoka? Ni mawazo na matakwa ya mwanadamu ambayo yamemleta hadi leo? Watu wengi wanaishi maisha yao yote bila kutimiziwa kwa matakwa yao. Kweli hili ni kwa sababu ya kosa katika fikira zao? Maisha ya watu wengi yamejawa na furaha na ridhaa isiyotarajiwa. Kweli ni kwa sababu wanatarajia kidogo sana? Je, nani kati ya wanadamu wote hatunzwi mbele ya macho ya Mwenyezi? Nani haishi maisha kati ya majaaliwa ya Mwenyezi? Kuzaliwa na kufa kwa nani kulitokana na kuchagua kwao? Je, mwanadamu anadhibiti hatima yake? Wanadamu wengi wanalilia kifo, lakini kiko mbali nao; watu wengi wanataka kuwa watu wenye nguvu maishani na wanahofia kifo, lakini bila kujua kwao, siku ya kufa kwao inasongea karibu, ikiwatumbukiza ndani ya dimbwi la kifo; watu wengi wanatazama angani na kutoa pumzi kwa undani; watu wengi wanalia sana, wakiomboleza; watu wengi wanaanguka kuwapo majaribu; na watu wengi wanakuwa wafungwa wa majaribu. Ingawa Sijitokezi binafsi kumruhusu mwanadamu kunitazama vizuri, watu wengi wanaogopa kuona uso Wangu, wanaogopa sana Nitawapiga chini, kwamba Nitawaangamiza. Mwanadamu kweli ananijua Mimi ama hanijui? Hakuna anayeweza kusema kwa hakika. Sivyo? Mnaniogopa na pia kuadibu Kwangu, lakini bado mnasimama na kunipinga wazi na kunihukumu hadharani. Sivyo? Kwamba mwanadamu hajawahi kunijua ni kwa sababu hajawahi kuuona uso Wangu ama kuisikia sauti Yangu. Hivyo, hata kama Niko ndani ya moyo wa mwanadamu, je, kuna wale ambao Sionekani mwenye ukungu na asiye dhahiri katika mioyo yao? Kuna wale Ninaoonekana vizuri ndani ya mioyo yao? Sitamani wale walio watu Wangu pia kutoniona vizuri, na hivyo Naanza kazi hii kubwa.

Nakuja polepole miongoni mwa wanadamu, na Naondoka taratibu. Kuna aliyewahi kuniona? Jua linaweza kuniona kwa sababu ya moto wake unaochoma? Mwezi unaweza kuniona kwa sababu ya uwazi wake unaong’aa? Kundinyota zinaweza kuniona kwa sababu ya mahali zipo angani? Nikujapo, mwanadamu hajui, na mambo yote yanabakia gizani, na Niondokapo, bado mwanadamu hafahamu. Nani anaweza kuwa na ushuhuda Kwangu? Inaweza kuwa sifa ya watu wa dunia? Inaweza kuwa mayungiyungi yanayochanua porini? Inaweza kuwa ndege wanaoruka angani? Inaweza kuwa simba wanaonguruma milimani? Hakuna anayeweza kunishuhudia kikamilifu. Hakuna anayeweza kufanya kazi Nitakayoifanya! Hata kama wangefanya kazi hii, ingekuwa na athari gani? Kila siku Naona vitendo vyote vya watu wengi, na kila siku Nachunguza mioyo na akili za watu wengi; hakuna aliyewahi kutoroka hukumu Yangu, na hakuna aliyewahi kuachana na uhalisi wa hukumu Yangu. Nasimama juu ya mawingu na kuangalia kwa umbali: Nimewaangamiza watu wengi, lakini pia watu wengi wanaishi katika huruma, na wema Wangu. Nyinyi pia hamuishi chini ya hali kama hizi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 11

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp