Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kazi na Kuonekana kwa Mungu | Dondoo 61

05/08/2020

Wakati umeme unatoka Mashariki—ambapo pia ni wakati hasa Naanza kunena—wakati umeme unakuja, mbingu yote inaangaziwa, na nyota zote zinaanza kubadilika. Inaonekana kana kwamba jamii nzima ya binadamu imesafishwa na kupangwa vizuri. Chini ya mng’aro wa mwale huu wa mwangaza kutoka Mashariki, wanadamu wote wanafichuliwa katika maumbo yao ya awali, macho yaking’aa, yakizuiwa kwa kuchanganyikiwa; na hawawezi hata kidogo kuficha sifa zao mbaya. Tena, ni kama wanyama wakitoroka kutoka kwa mwangaza Wangu wakikimbilia usalama katika mapango ya milimani; ilhali, hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kufutiliwa mbali kutoka katika mwanga Wangu. Wanadamu wote wako na hofu na wasiwasi, wote wanangoja, wote wanatazama; na ujio wa mwanga Wangu, wote wanasherekea katika siku waliozaliwa, na vilevile wote wana laani siku waliozaliwa. Hisia zinazopingana haziwezi kueleza; machozi ya kujiadhibu huunda mito, na yanabebwa mbali juu ya mvo unaofagia, kuenda mara moja yasionekane tena. Kwa mara nyingine, siku Yangu inakaribia jamii ya binadamu, mara nyingine ikiamsha jamii ya binadamu, ikiwapa binadamu hatua ya kutengeneza mwanzo mpya. Moyo Wangu unapiga na, kufuatia mdundo wa mpigo wa moyo Wangu, milima inaruka kwa furaha, maji yanacheza kwa furaha, na mawimbi, kwa wakati ufaao, yanagonga juu ya mawe ya mwamba. Ni vigumu kueleza kile kilicho ndani ya moyo Wangu. Nataka vitu vyote visivyo safi vichomeke na kuwa jivu Nikitazama, Nataka wana wote wa kutotii wapotee kutoka mbele ya macho Yangu, wasikawie tena katika uwepo. Sijatengeneza mwanzo mpya pekee katika makao ya joka kubwa jekundu, Nimeanza pia kazi mpya katika ulimwengu. Hivi karibuni falme za dunia zitakuwa falme Zangu; hivi karibuni falme za dunia zitakoma milele kuwepo kwa sababu ya ufalme Wangu, kwa sababu Nimetimiza ushindi tayari, kwa sababu Nimerejea kwa ushindi. Joka kubwa jekundu limetumia njia zote za kuweza kufikiriwa ili kuvuruga mpango Wangu, akitumaini kufuta kazi Yangu duniani, lakini Naweza kukata tamaa kwa sababu ya mbinu zake za udanganyifu? Naweza kutishwa hadi kukosa kujiamini na vitisho vyake? Hakujawahi kuwa na kiumbe hata mmoja mbinguni ama duniani ambaye Simshiki katika kiganja cha mkono Wangu; ni kiwango gani zaidi ambacho huu ni ukweli kuhusu joka kuu jekundu, chombo hiki kinachotumika kama foili Kwangu? Je, pia si kitu cha kutawaliwa na mikono Yangu?

Katika wakati wa kupata mwili Kwangu katika dunia ya binadamu, binadamu alifika pasipo kujua katika siku hii na usaidizi wa uongozi wa mkono Wangu, pasipo kujua akaja kunifahamu. Lakini, kuhusu jinsi ya kutembea katika njia iliyo mbele, hakuna aliye na fununu, hakuna anayejua, na bado hakuna aliye na kidokezo juu ya mwelekeo ambao hiyo njia itampeleka. Mwenyezi pekee akimwangalia ndipo yeyote ataweza kutembea njia hiyo hadi mwisho; akiongozwa tu na umeme kutoka Mashariki ndipo yeyote ataweza kuvuka kizingiti kinachoelekea katika ufalme Wangu. Miongoni mwa wanadamu, hakujawahi kuwa na yeyote ambaye ameuona uso Wangu, ambaye ameona umeme Mashariki; sembuse yule ambaye amesikia sauti inayotoka kwa kiti Changu cha enzi? Kwa kweli, kutoka siku za zamani, hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye amewasiliana na nafsi Yangu moja kwa moja; leo tu, wakati Nimekuja duniani, ndipo wanadamu wana nafasi ya kuniona. Lakini hata sasa, wanadamu bado hawanifahamu, jinsi wanavyouangalia uso Wangu na kuisikia tu sauti Yangu, lakini bila kuelewa Ninachomaanisha. Wanadamu wote wako hivi. Ukiwa mmoja wa watu Wangu, je huhisi fahari ya kina unapoona uso Wangu? Na je, huhisi aibu kwa sababu hunifahamu? Natembea kati ya wanadamu, na Naishi kati ya wanadamu, kwani Nimekuwa mwili na Nimekuja katika ulimwengu wa binadamu. Lengo Langu sio tu kuuwezesha binadamu kuutazamia mwili Wangu; cha maana zaidi, ni kuuwezesha binadamu kunifahamu Mimi. Zaidi, kupitia mwili Wangu uliopatwa, Nitauona binadamu na hatia kwa sababu ya dhambi zake; kupitia mwili Wangu uliopatwa, Nitashinda joka kuu jekundu na kuondoa pango lake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 12

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp