Wimbo wa Kusifu | Yote Ambayo Kazi na Maneno ya Mungu Yamletea Mwanadamu ni Uzima (Music Video)

29/08/2020

Mungu hashikilii ya kale au kutumia njia isiyotumika na wengi;

Anapofanya kazi na kuongea sio njia ya kutilia mipaka kama vile watu wanavyofikiria.

Ndani ya Mungu, vyote ni huru na vimekombolewa,

na hakuna hali ya kukinga, hakuna vizuizi—

kile Anachomletea mwanadamu vyote ni uhuru na ukombozi.

Yeye ni Mungu aliye hai,

Mungu ambaye kwa kweli, na kwa hakika yupo.

Yeye si kikaragosi au sanamu ya udongo,

na Yeye ni tofauti kabisa na sanamu ambazo watu huhifadhi na kuabudu.

Yeye yuko hai na mwenye nguvu na kile ambacho maneno

Yake na kazi Yake humletea binadamu vyote ni uzima na nuru,

uhuru na ukombozi wote,

kwa sababu Yeye anashikilia ukweli, uzima, na njia—

Yeye hajazuiliwa na chochote katika kazi yoyote Yake.

Kwa sababu Yeye anashikilia ukweli, uzima, na njia—

Yeye hajazuiliwa na chochote katika kazi yoyote Yake.

Bila kujali watu wanavyosema na namna wanavyoona

au kukadiria kazi Yake mpya,

Ataitekeleza kazi Yake bila kusita.

Hatakuwa na wasiwasi kuhusu dhana zozote za yeyote

au kazi na maneno Yake kuelekezewa vidole,

au hata upinzani wao mkubwa katika kazi Yake mpya.

Hakuna yeyote miongoni mwa viumbe vyote anayeweza kutumia akili ya binadamu,

au kufikiria kwa binadamu, maarifa au maadili

ya binadamu kupima au kufasili kile ambacho Mungu anafanya,

kutia fedheha, au kutatiza au kukwamiza kazi Yake.

Hakuna kizuizi chochote katika kazi Yake na kile Anachokifanya,

na haitawekewa kizuizi chochote na binadamu yeyote,

kitu chochote, au kifaa chochote,

na haitakatizwa na nguvu zozote za kikatili.

Yeye ni Mfalme anayeshinda daima,

na nguvu zozote za kikatili

na uvumi wote na hoja za uwongo zote kutoka kwa mwanadamu

zimekanyagiwa chini ya kibao Chake cha kuwekea miguu.

Haijalishi ni hatua gani mpya ya kazi Yake ambayo Anatekeleza,

lazima iendelezwe na ipanuliwe katika mwanadamu,

na lazima itekelezwe bila kuzuiliwa kote ulimwenguni

mpaka pale ambapo kazi Yake kubwa imekamilika.

Huu ndio uweza na hekima ya Mungu, na mamlaka na nguvu Zake.

Kwa Mungu hakuna vizuizi.

Mungu anazo kanuni katika maneno na kazi Yake,

lakini hakuna kuzuiliwa,

kwa sababu Mungu Mwenyewe ndiye ukweli, njia na uzima.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp