Je, Biblia ndiye Bwana, au ni Mungu? | "Bwana Wangu Ni Nani" (Filamu za Injili)
16/11/2017
Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba "Biblia ni ufunuo wa Mungu," "Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu." Moyoni mwake, Biblia ni kuu. Kwa sababu ya upendo na imani yake pofu katika Biblia, hajawahi kutafuta au kuitazama kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Hadi siku moja, alipowazuia waumini kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu mtandaoni, akawa na fursa ya kukutana na wahubiri kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Baada ya kupitia majadiliano makali kuhusu ukweli, aliweza hatimaye kuona wazi uhusiano kati ya Biblia na Mungu? Je, aliweza kusonga mbali na Biblia kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima? Je, atachukuliwa kwenda mbinguni mbele ya Mungu?
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video