Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatua Tatu za Kazi | Dondoo 20

01/06/2020

Kwenye Enzi ya Sheria, Yehova Aliweza kuweka wazi sheria nyingi kwa Musa kupitisha kwa wana wa Israeli waliomfuata kutoka Misri. Yehova Aliwakabidhi sheria hizi wana wa Israeli ambazo hazikuwa na uhusiano wowote na Wamisri, na zilinuiwa kuwazuia wana wa Israeli, na ndiyo yaliyokuwa mahitaji Yake kwao. Kama mtu alitii sheria ya Sabato, kama mtu aliheshimu wazazi wake, kama mtu aliabudu miungu na kadhalika, hizi ndizo zilizokuwa kanuni ambazo mtu alihukumiwa na kujulikana kama mwenye dhambi au mwenye haki. Kama mtu alichomwa na moto wa Yehova, au kupigwa na mawe hadi kufa, au kupokea baraka za Yehova, vyote hivi viliamuliwa kulingana na kama mtu alitii sheria hizi. Wale ambao hawakutilia maanani Sabato wangepigwa mawe hadi kufa. Wale makuhani ambao hawakutilia maanani Sabato wangeteketezwa na moto wa Yehova. Wale ambao hawakuheshimu wazazi wao wangepigwa mawe pia hadi kufa. Haya yote yalishauriwa na Yehova. Yehova Alianzisha sheria Zake na taratibu ili huku Akiyaongoza maisha yao, watu wangeweza kumsikiliza na kuheshimu neno Lake na wala si kuasi neno Lake. Alitumia sheria hizi kuweza kudhibiti kizazi kipya cha binadamu kilichozaliwa, kuweka msingi wa kazi Yake ambayo ingefuata. Na kwa hivyo, sababu ya kazi ambayo Yehova Alifanya, enzi ya kwanza iliitwa Enzi ya Sheria. Ingawaje Yehova Aliongea sana na Alifanya kazi nyingi, Aliwaongoza tu kwa njia nzuri huku Akiwafunza watu hawa wasiojua namna ya kuwa na wema, namna ya kuishi, namna ya kuelewa njia ya Yehova. Katika sehemu kubwa ya kazi Yake kwa hakika Alinuia kuruhusu watu Wake kufuatilia njia Yake na kufuata sheria Yake. Kazi ilifanyiwa watu ambao walikuwa wamepotoka kidogo; haikujali sana mageuzi ya tabia au ukuzi wa maisha. Alijali tu matumizi ya sheria ya kuzuia na kudhibiti watu. Kwa wana wa Israeli wakati huo, Yehova Alikuwa tu Mungu kwenye hekalu, Mungu kwenye mbingu. Alikuwa mnara wa wingu, mnara wa moto. Kile ambacho Yehova Aliwahitaji kufanya kilikuwa ni kutii kile ambacho watu wanajua leo kama sheria na mafundisho Yake—mtu angeweza hata kusema taratibu—kwa sababu kazi ya Yehova haikunuiwa kuwabadilisha, lakini kuwapatia vitu vingi ambavyo binadamu anastahili kuwa navyo, kuwaambia kutoka kwenye kinywa Chake mwenyewe, kwa sababu baada ya binadamu kuumbwa, binadamu hakujua chochote kuhusu kile alichostahili kumiliki. Na kwa hivyo Yehova Aliwapatia vitu walivyostahili kumiliki katika maisha yao hapa ulimwenguni, Akawafanya watu Aliokuwa Amewaongoza kuzidi vizazi vyao, Adamu na Hawa, kwa sababu kile Yehova Alichowapatia kilizidi kile Alichokuwa Amepatia Adamu na Hawa hapo mwanzo. Licha ya hayo yote, kazi ambayo Yehova Alifanya Israeli ilikuwa tu kuongoza binadamu na kuwafanya kumtambua Muumba wao. Hakuwashinda wala kuwabadilisha, Aliwaongoza tu. Hii ndiyo jumla ya kazi ya Yehova kwenye Enzi ya Sheria. Ndiyo maelezo ya ziada, hadithi ya kweli, kiini cha kazi Yake kwenye nchi nzima ya Israeli na mwanzo wa kazi Yake ya miaka elfu sita—katika kudhibiti mwanadamu kwa mkono wa Yehova. Kutokana na haya yote kazi nyingi zaidi ilijitokeza kwenye mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi katika Enzi ya Sheria

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp