Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kupata Mwili | Dondoo 138

02/08/2020

Mungu haji duniani kufanya ubinadamu Wake wa kawaida uwe mkamilifu. Yeye haji kufanya kazi ya ubinadamu wa kawaida, ila kufanya kazi ya Uungu ndani ya ubinadamu wa kawaida. Kile ambacho Mungu anaona kama ubinadamu wa kawaida si kile ambacho mwanadamu anafikiria. Mwanadamu hufafanua “ubinadamu wa kawaida” kama kuwa na mke, au mume, na watoto. Huu ni ushahidi kwamba mtu ni mwanadamu wa kawaida. Lakini Mungu haoni hivi. Anaona ubinadamu wa kawaida kama kuwa na mawazo ya kawaida ya binadamu na maisha na kuzaliwa na wanadamu wa kawaida. Lakini ukawaida Wake hauhusishi kuwa na mke, au mume na watoto vile ambavyo mwanadamu anaelewa hali ya kawaida. Yaani, kwa mwanadamu, ubinadamu wa kawaida ambao Mungu Anazungumzia ni kile mwanadamu angeona kama kukosekana kwa ubinadamu, karibu ukose kuwa na hisia na kuonekana hauna mahitaji ya kimwili, kama vile Yesu, Ambaye Alikuwa tu nje ya mwanadamu wa kawaida na alichukua umbo la juu la mwanadamu wa kawaida, lakini katika kiini hakuwa kabisa na vitu alivyo navyo mwanadamu wa kawaida. Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba dutu ya Mungu mwenye mwili haihusishi kwa ukamilifu hali ya ubinadamu wa kawaida, lakini sehemu tu ya mambo ambayo wanadamu wanapaswa kuwa nayo, ili kuendeleza kanuni za maisha ya kawaida ya binadamu na akili ya kawaida ya binadamu. Lakini hivi vitu havihusiani na kile ambacho mwanadamu anaona kama ukawaida wa ubinadamu. Hivi ni vile Mungu mwenye mwili Anapaswa kuwa navyo. Hata hivyo baadhi ya wanadamu wanasema kwamba Mungu mwenye mwili Anaweza tu kuwa na ubinadamu wa kawaida iwapo Yeye ana mke, watoto na familia. Bila mambo haya, wanasema, Yeye si mwanadamu wa kawaida. Nakuuliza hivi basi, je, Mungu Ana mke? Je, inawezekana kwa Mungu kuwa na mume? Je, Mungu Anaweza kuwa na watoto? Je, hizi sio dhana zenye kosa tu? Hata hivyo, Mungu katika mwili Hawezi kuchomoka kutoka katika nyufa kwenye miamba au kuanguka chini kutoka mbinguni. Anaweza tu kuzaliwa kwa familia ya kawaida ya binadamu. Hiyo ndio maana Anao wazazi na dada. Haya ni mambo ambayo ubinadamu wa kawaida ndani ya Mungu katika mwili lazima Awe nayo. Hivi ndivyo Yesu alivyokuwa. Yesu Alikuwa na baba na mama, na ndugu. Haya yote yalikuwa ya kawaida. Lakini kama Angekuwa na mke na watoto, basi Wake haungekuwa ubinadamu wa kawaida ambao Mungu alitaka katika Mungu mwenye mwili. Kama ni hivyo, Yeye Hangekuwa na uwezo wa kuwakilisha Uungu katika kazi Yake. Ilikuwa ni kwa sababu Hakuwa na mke au watoto lakini Alizaliwa na wanadamu wa kawaida katika familia ya kawaida ndipo yeye alikuwa na uwezo wa kufanya kazi ya Uungu. Kwa kufafanua, kile ambacho Mungu anaona kama mwanadamu wa kawaida ni mwanadamu aliyezaliwa katika familia ya kawaida. Mwanadamu kama huyo tu ndiye anayeweza kufanya kazi ya Mungu. Kama, kwa upande mwingine, mtu huyo angekuwa na mke, watoto, au mume, mwanadamu huyo basi hangekuwa na uwezo wa kufanya kazi ya Mungu kwa sababu angekuwa tu na ubinadamu wa kawaida ambao binadamu anahitaji lakini si ubinadamu wa kawaida ambao Mungu Anahitaji. Mawazo ya Mungu na ufahamu wa wanadamu mara nyingi huwa na tofauti kubwa na zenye viwango tofauti. Katika hatua hii ya kazi ya Mungu kuna mengi ambayo yanapingana na hutofautiana na fikra za wanadamu. Unaweza kusema kwamba hatua hii ya kazi ya Mungu yote hufanyika kwa mikono ya Uungu moja kwa moja, na ubinadamu ukiwa na jukumu la kusaidia. Kwa sababu Mungu anakuja duniani kufanya kazi Yake mwenyewe badala ya kumwacha mwanadamu aifanye, Yeye Hujiweka Mwenyewe katika mwili (kwa mwanadamu wa kawaida asiye mkamilifu) ili kufanya kazi Yake. Anatumia mwili huu kuwasilisha mwanadamu na enzi mpya, kuwaambia wanadamu hatua inayofuata katika kazi Yake, ili waweze kutenda kwa mujibu wa njia iliyoelezwa na neno Lake. Na hapo Mungu Anakamilisha kazi Yake katika mwili, Anahitaji kuondoka mwanadamu, asiishi tena katika mwili wa ubinadamu wa kawaida, na badala yake kusonga mbali na mwanadamu kufanya sehemu nyingine ya kazi Yake. Yeye kisha Hutumia wanadamu wanaopendeza moyo Wake kuendeleza kazi Yake hapa duniani miongoni mwa kundi hili la wanadamu, lakini katika ubinadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Mwenye Mwili na Watu Wanaotumiwa na Mungu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp