Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili | Dondoo 129

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili | Dondoo 129

95 |13/08/2020

Neno la Mungu | Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili | Dondoo 129

Kila hatua ya kazi iliyofanywa na Mungu ina umuhimu mkubwa. Yesu alipokuja, Alikuwa mwanaume, na wakati huu Yeye ni mwanamke. Kutokana na hili, unaweza kuona kwamba Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke kwa ajili ya kazi Yake na Kwake hakuna tofauti ya jinsia. Roho Wake anapowasili, Anaweza kuchukua umbo la mwili wowote kwa matakwa Yake na mwili unamwakilisha Yeye. Awe mwanamume au mwanamke, wote wanamwakilisha Mungu ili mradi tu ni Mungu mwenye mwili. Kama Yesu angekuja na Angeonekana kama mwanamke, kwa maneno mengine, iwapo mtoto wa kike, sio wa kiume, angezaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, hatua hiyo ya kazi ingeweza kukamilika pia. Kama hali ingekuwa hivyo, hatua hii ya kazi ingeweza kukamilishwa badala yake na mwanaume na kazi ingekuwa imekamilika pia. Kazi inayofanywa katika hatua zote ni muhimu sana; hakuna kazi inayojirudia au kupingana na nyingine. Wakati wa kazi Yake, Yesu alikuwa anaitwa Mwana wa pekee, ikiwa inaashiria jinsia ya kiume. Sasa kwa nini Mwana wa pekee hakutajwa katika hatua hii? Hii ni kwa sababu mahitaji ya kazi yamelazimisha badiliko la jinsia tofauti na ile ya Yesu. Kwa Mungu hakuna tofauti ya jinsia. Kazi Yake inafanywa kama Anavyotaka na haizuiliwi na kitu chochote kile, kimsingi ipo huru, lakini kila hatua ina umuhimu mkubwa. Mungu alifanyika mwili mara mbili, na ni dhahiri kwamba kupata mwili kwake katika siku za mwisho ni mara ya mwisho. Amekuja kufichua matendo Yake yote. Ikiwa katika hatua hii Hakufanyika mwili ili Yeye binafsi afanye kazi kwa ajili ya mwanadamu kushuhudia, mwanadamu milele angeshikilia fikra kwamba Mungu ni wa kuime tu, na sio wa kike. Kabla ya hili, wote waliamini kwamba Mungu anaweza kuwa tu mwanaume na kwamba mwanamke hawezi kuitwa Mungu, maana wote walichukulia kwamba mwanamume ana mamlaka juu ya mwanamke. Waliamini kwamba hakuna mwanamke anayeweza kuchukua mamlaka, bali ni mwanamume tu. Hata walisema kwamba mwanamume alikuwa ni kichwa cha mwanamke na kwamba mwanamke anapaswa kumheshimu mwanaume na asiweze kuwa juu yake. Iliposemwa hapo nyuma kwamba mwanamume alikuwa kichwa cha mwanamke, ilisemwa kwa kurejelea Adamu na Hawa ambao walidanganywa na yule nyoka, na wala sio mwanamume na mwanamke walioumbwa na Yehova hapo mwanzo. Kimsingi, mwanamke anapaswa kumtii na kumpenda mume wake, kama vile ambavyo mwanamume anapaswa kujifunza kuisaidia familia yake. Hizi ni sheria na kanuni zilizowekwa na Yehova ambazo kwazo mwanadamu anapaswa kuzifuata katika maisha yake ya hapa duniani. Yehova alimwambia mwanamke “tamaa yako itakuwa ni kwa mumeo, naye atatawala juu yako.” Hii ilisemwa tu ili kwamba mwanadamu (yaani, mwanamume na mwanamke) waweze kuishi maisha ya kawaida chini ya utawala wa Yehova, ili kwamba maisha ya mwanadamu yawe na mfumo na yasipoteze mwelekeo. Kwa hivyo, Yehova alitengeneza kanuni zinazofaa kwa ajili ya namna ambavyo mwanamume na mwanamke wanavyopaswa kutenda, lakini kanuni hizi zilirejelea tu viumbe wote wanaoishi duniani, na sio kwa Mungu kupata mwili. Inawezekanaje Mungu awe sawa na uumbaji Wake? Maneno Yake yalielekezwa tu kwa mwanadamu wa uumbaji Wake; zilikuwa kanuni zilizowekwa kwa ajili ya mwanamume na mwanamke ili kwamba mwanadamu huyo aweze kuishi maisha ya kawaida. Hapo mwanzo, ambapo Yehova alimuumba mwanadamu, aliwaumba mwanamume na mwanamke; kwa hiyo, kupata Kwake mwili pia kulitofautishwa kuwa ama mwanamume au mwanamke. Hakuamua kazi Yake kulingana na maneno aliyozungumza kwa Adamu na Hawa. Kufanyika mwili mara mbili kuliamuliwa kabisa kwa kuzingatia mawazo Yake alipomuumba mwanadamu kwa mara ya kwanza. Yaani, alikamilisha kazi ya kupata kwake mwili mara mbili, kwa msingi wa mwanamke na mwanamume ambao hawakuwa wameharibiwa na dhambi. Ikiwa mwanadamu atatumia maneno yaliyozungumzwa na Yehova kwa Adamu na Hawa ambao walidanganywa na yule nyoka katika kazi ya Mungu katika mwili, je, si kwamba Yesu pia anapaswa kumpenda mke Wake kama Alivyotakiwa? Je, Mungu bado ni Mungu wakati huo tena? Ikiwa ni hivyo, je, Anaweza kukamilisha kazi Yake? Ikiwa ni vibaya kwa Mungu aliyepata mwili kuwa mwanamke, je, lisingekuwa kosa kubwa Mungu alipomuumba mwanamke? Ikiwa mwanadamu bado anaamini kwamba Mungu kupata mwili kama mwanamke ni vibaya, je, Yesu, ambaye hakuoa na hivyo hakuweza kumpenda mke Wake, hangekuwa na makosa kama kupata mwili kwa sasa? Kwa kuwa unatumia maneno yaliyozungumzwa na Mungu kwa Hawa ili kupima ukweli wa Mungu kupata mwili leo, unapaswa kutumia maneno ya Mungu kwa Adamu kumhukumu Bwana Yesu ambaye alikuwa mwili katika Enzi ya Neema. Je, hawa wawili sio sawa? Kwa kuwa unamhukumu Bwana Yesu kwa kumtumia mwanamume ambaye hakudanganywa na yule nyoka, huwezi kuhukumu ukweli wa kupata mwili leo hii kwa mwanamke ambaye alidanganywa na yule nyoka. Hiyo sio sawa kabisa! Ikiwa unafanya hukumu ya namna hiyo, basi hii inathibitisha kukosa urazini kwako. Yehova alipopata mwili mara mbili, jinsia ya mwili Wake ilikuwa inahusiana na mwanamume na mwanamke ambaye hakudanganywa na yule nyoka. Alipata mwili mara mbili kulingana na mwanamume na mwanamke ambaye hakudanganywa na yule nyoka. Usifikiri kwamba uanaume wa Yesu ulikuwa sawa na uanaume wa Adamu ambaye alidanganywa na yule nyoka. Hahusiani naye kabisa, na ni wanaume wawili wa asili tofauti. Hakika haiwezi kuwa kwamba uanaume wa Yesu unathibitisha yeye ni kichwa cha wanawake wote na sio kichwa cha wanaume wote? Je, yeye si Mfalme wa Wayahudi wote (ikiwa ni pamoja na wanaume na wanawake)? Ni Mungu Mwenyewe, sio tu kichwa cha mwanamke bali ni kichwa cha mwanamume pia. Ni Bwana wa viumbe vyote, na kichwa cha viumbe vyote. Unawezaje kuamua uanaume wa Yesu kuwa ishara ya kichwa cha mwanamke? Hii si kufuru? Yesu ni mwanamume ambaye hajapotoshwa. Yeye ni Mungu; ni Kristo; ni Bwana. Anawezaje kuwa mwanamume kama Adamu ambaye ameharibiwa na dhambi? Yesu ni mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu aliye mtakatifu sana. Unawezaje kusema kuwa Yeye ni Mungu katika uanaume wa Adamu? Je, haingekuwa kwamba kazi yote ya Mungu ingekuwa na makosa? Je, Yehova angeweza kuuweka ndani ya Yesu uanaume wa Adamu ambaye alidanganywa? Sio kwamba kupata mwili kwa wakati huu ni kazi nyingine ya Mungu katika mwili tofauti kijinsia na Yesu lakini wanafanana katika asili? Bado unathubutu kusema kwamba Mungu aliyepata mwili hakuweza kuwa mwanamke kwa kuwa mwanamke ndiye aliyedanganywa kwanza na yule nyoka? Bado unathubutu kusema kwamba mwanamke ni najisi sana na ni chanzo cha upotovu wa mwanadamu, Mungu hawezi kufanyika mwili kama mwanamke? Bado unathubutu kusema kwamba “mwanamke siku zote atamtii mwanamume na hawezi kamwe kudhihirisha au kumwakilisha Mungu moja kwa moja”? Hukuelewa hapo nyuma; sasa bado unaweza kukufuru kazi ya Mungu, hususan Mungu aliyepata mwili? Kama huwezi kuona hili wazi wazi, ni vizuri zaidi ukawa makini na ulimi wako, la sivyo upumbavu na ujinga wako vitawekwa wazi na ubaya wako utadhihirishwa. Usidhani kwamba unaelewa kila kitu. Nakueleza kwamba yote uliyokwishayaona na kuyapitia hayatoshelezi kuelewa hata milenia ya mpango Wangu wa usimamizi. Sasa kwa nini basi unakuwa na kiburi? Talanta ndogo hiyo uliyonayo na maarifa kidogo hayo uliyonayo hayatoshelezi kutumika hata katika sekunde moja ya kazi ya Yesu! Je, una uzoefu mkubwa kiasi gani hasa? Yote uliyoyaona na yote uliyoyasikia katika maisha yako na yote uliyowahi kuyafikiria ni kidogo sana kulinganisha na kazi Ninayoifanya kwa muda mfupi sana! Ni bora usichambue chambue na kutafuta kosa. Haijalishi una kiburi kiasi gani, wewe bado ni kuimbe tu mdogo kuliko sisimizi! Vyote hivyo vilivyomo katika tumbo lako ni vichache zaidi ya vile vilivyomo katika tumbo la sisimizi! Usifikiri kwamba kwa kuwa umepitia mengi na umekuwa mkubwa, unaweza kuzungumza na kutenda kwa majivuno na ujeuri. Je, uzoefu wako na ukuu wako sio matokeo ya maneno Niliyoyazungumza? Je, unaamini kwamba umekuwa hivyo kwa sababu ya kufanya kwako kazi kwa bidii na kutokwa jasho? Siku hii, unaona kupata Kwangu mwili, na matokeo yake ni kwamba unakuwa na dhana nyingi hizo, kutoka kwazo unakuwa na fikira nyingi isiyohesabika. Ikiwa sio kwa kupata mwili Kwangu, bila kujali talanta zako ni za ajabu kiasi gani, usingeweza kuwa na dhana hizi nyingi. Sio kutokana na hili ndipo imeibuka fikira yako? Kama si kupata mwili kwa Yesu kwa mara ya kwanza, je, ungejua nini kuhusu kupata mwili? Je, si kwa sababu ya maarifa yako ya kupata mwili kwa mara ya kwanza ndio maana unathubutu kuhukumu kupata mwili kwa mara ya pili? Kwa nini uchunguze kwa makini badala ya kuwa mfuasi mtiifu? Umeingia katika mkondo huu na umekuja mbele ya Mungu aliyepata mwili. Ungewezaje kuruhusiwa kujifunza? Ni sawa kwako kujifunza historia ya familia yako, lakini ukichunguza “historia ya familia” ya Mungu, inawezekanaje Mungu wa leo akuruhusu kufanya hivyo? Je, wewe sio kipofu? Je, hujiletei dharau kwako mwenyewe?

Umetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi