Ngoma ya Kikristo | Furaha katika Nchi Nzuri ya Kanaani

2032 |05/06/2017

Nimerudi kwa familia ya Mungu, mchangamfu na mwenye furaha.

Mikono yangu imemshika mpendwa wangu, moyo wangu ni miliki Yake.

Japo nimepitia Bonde la Machozi, nimeyaona mapenzi ya Mungu.

Mapenzi yangu kwa Mungu hukua siku baada ya siku, Mungu ndiye chanzo cha furaha yangu.

Nikiduwazwa na uzuri wa Mungu, moyo wangu umeshikizwa kwa Mungu.

Siwezi kumpenda Mungu vya kutosha, nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.

Nikiduwazwa na uzuri wa Mungu, nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.

Siwezi kumpenda Mungu vya kutosha, nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.

Katika nchi hii iliyobarikiwa ya Kanaani, yote ni mabichi, yote ni mapya,

yakifurika na nafsi ya uhai ya maisha.

Maji ya uzima hutiririka kutoka kwa Mungu wa vitendo, hunifanya niruzukike na maisha.

Naweza kufurahia baraka kutoka mbinguni, hakuna tena kutafuta, kuchakura, kuwa na uchu.

Nimewasili katika nchi iliyobarikiwa ya Kanaani, furaha yangu haina kifani!

Upendo wangu kwa Mungu huniletea nguvu isiyoisha.

Sauti za kusifu hupaa juu mbinguni, zikimwambia upendo wangu wa ndani.

Ni haiba ilioje mpendwa wangu aliyo nayo! Uzuri Wake huiteka roho yangu.

Manukato ya mpendwa wangu hunifanya nione ugumu wa kumwacha.

Nyota mbinguni zatabasamu kwangu, jua lanikubali kutoka juu.

Pamoja na mwanga wa jua, na mvua na umande, tunda la uzima hukua kwa uthabiti na ubivu.

Maneno ya Mungu, mengi na ya fahari, hutuletea sikukuu tamu.

Riziki nzima na ya kutosha ya Mungu hutufanya tutosheke.

Nchi ya Kanaani, ulimwengu wa maneno ya Mungu; upendo Wake hutuletea furaha isiyokoma.

Nchi ya Kanaani, ulimwengu wa maneno ya Mungu; upendo Wake hutuletea furaha isiyokoma.

Harufu nzuri ya matunda hujaa hewani.

Ukikaa hapa kwa siku chache, utapapenda kuliko chochote kingine.

Hakuna wakati utataka kuondoka.

Mwezi wa fedha hunurisha mwanga wake. Mzuri na mchangamfu, ni maisha yangu.

Uliye mpendwa moyoni mwangu, uzuri Wako umepita maneno yote.

Moyo wangu u katika mapenzi matamu Nawe, siwezi kujizuia kuruka kwa furaha.

Daima Uko moyoni mwangu, nitakuwa nawe maisha yangu yote.

Moyo wangu hukutamani Wewe daima; kukupenda Wewe hufurahisha moyo wangu kila siku.

Ee mpenzi moyoni mwangu! Nimekupa mapenzi yangu yote.

Moyo wangu hukutamani Wewe daima; kukupenda Wewe hufurahisha moyo wangu kila siku.

Ee mpenzi moyoni mwangu! Nimekupa mapenzi yangu yote.

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi